Mithali 18:17-24
Yeye aliye wa kwanza kuleta mashtaka huonekana sahihi,
hadi mwingine ajitokezapo na kumuuliza maswali.
Kupiga kura hukomesha mashindano
na kutenganisha wapinzani wakuu wanaopingana.
18:19 1Sam 17:28Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuridhika
kuliko mji uliozungushiwa ngome,
nayo mabishano ni kama malango
ya ngome yenye makomeo.
18:20 Mit 12:14Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake,
atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake.
18:21 Mit 13:2-3; Mt 12:37Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi,
nao waupendao watakula matunda yake.
18:22 Mit 12:4; 31:10; Ay 33:26Apataye mke apata kitu chema
naye ajipatia kibali kwa Bwana.
18:23 Mwa 42:13-16; Yak 2:3Mtu maskini huomba kuhurumiwa
bali tajiri hujibu kwa ukali.
18:24 1Sam 20:42; Yn 15:13-15Mtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu,
bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu.
Mithali 19:1-2
19:1 Mit 28:6Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama,
kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka.
19:2 Hos 4:6; Yn 16:3; Rum 10:2Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa,
wala kufanya haraka na kuikosa njia.