Mithali 17:5-14 NEN

Mithali 17:5-14

17:5 Mit 14:31; Ay 31:39; Eze 25:3; Oba 1:12Yeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake;

yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa.

17:6 Za 125:5; Mit 13:22Wana wa wana ni taji la wazee,

nao wazazi ni fahari ya watoto wao.

17:7 Mit 16:10Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu:

je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala!

17:8 Mwa 39:21; Dan 6:3Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho;

kokote kigeukiapo, hufanikiwa.

17:9 Mit 10:12; 16:28Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo,

bali yeyote arudiaye jambo hutenganisha marafiki wa karibu.

Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua

kuliko mapigo mia kwa mpumbavu.

Mtu mbaya hupenda kuasi tu;

mjumbe asiye na huruma atatumwa dhidi yake.

17:12 1Sam 25:25Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyangʼanywa watoto wake,

kuliko mpumbavu katika upumbavu wake.

17:13 Yer 18:20; 1Sam 19:4; Rum 12:17; Za 109:4-5Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema,

kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake.

17:14 Mit 20:3; Mt 5:25-26; Mdo 6:1Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji;

kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza.

Read More of Mithali 17