Mithali 17:25-28
17:25 Mit 10:1Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake
na uchungu kwa yeye aliyemzaa.
17:26 Za 94:21; Mit 18:5Si vizuri kumwadhibu mtu asiye na hatia,
au kuwapiga sana maafisa kwa ajili ya uadilifu wao.
17:27 Ay 6:24; Mit 14:29Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia,
naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu.
17:28 Ay 2:13; Mit 10:19Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima kama akinyamaza,
na mwenye ufahamu kama akiuzuia ulimi wake.
Mithali 18:1-6
Mtu ajitengaye na wengine
hufuata matakwa yake mwenyewe;
hupiga vita kila shauri jema.
18:2 Mit 12:23Mpumbavu hafurahii ufahamu,
bali hufurahia kutangaza
maoni yake mwenyewe.
Wakati uovu unapokuja, dharau huja pia,
pamoja na aibu huja lawama.
18:4 Za 18:16Maneno ya kinywa cha mwanadamu ni kina cha maji,
bali chemchemi ya hekima ni kijito kinachobubujika.
18:5 Law 19:15; Mit 28:21; Za 82:2; Ay 13:7-8Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu,
au kumnyima haki asiye na hatia.
18:6 Mit 10:14Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi
na kinywa chake hualika kipigo.