Mithali 16:8-17
16:8 Za 37:16; Mit 15:16; 17:1; Mhu 4:6Afadhali kitu kidogo pamoja na haki
kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
16:9 Yer 10:23Moyo wa mtu huifikiri njia yake,
bali Bwana huelekeza hatua zake.
16:10 Mit 17:7Midomo ya mfalme huzungumza kwa hekima ya kiungu,
wala kinywa chake hakipotoshi haki.
16:11 Law 19:36; Mit 11:1; Eze 45:10Vipimo na mizani za halali hutoka kwa Bwana;
mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye.
16:12 Mit 26:28; 25:5; 29:14; 31:5Wafalme huchukia sana kutenda maovu,
kwa maana kiti cha ufalme hufanywa imara kwa njia ya haki.
16:13 Mit 22:11Wafalme hufurahia midomo ya uaminifu;
humthamini mtu asemaye kweli.
16:14 Mwa 40:2; Ay 29:24Ghadhabu ya mfalme ni mjumbe wa mauti,
bali mtu mwenye hekima ataituliza.
16:15 2Nya 36:16; Mit 29:1; Yer 19:1116:15 Mwa 40:2; Ay 29:24; Mit 19:12; 25:2-7Uso wa mfalme ungʼaapo, inamaanisha uhai;
upendeleo wake ni kama wingu la mvua wakati wa vuli.
16:16 Za 49:20; Ay 28:15; Mit 3:13-14Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu,
kuchagua ufahamu kuliko fedha!
16:17 Mit 4:24-27; Isa 35:8; Mdo 24:16Njia kuu ya wanyofu huepuka ubaya;
yeye aichungaye njia yake, huchunga maisha yake.