Mithali 16:28-33
16:28 Mit 14:17; 17:9Mtu mpotovu huchochea ugomvi,
nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu.
Mtu mkali humvuta jirani yake
na kumwongoza katika mapito yale mabaya.
16:30 Mit 6:13Yeye akonyezaye kwa jicho lake anapanga upotovu;
naye akazaye midomo yake amenuia mabaya.
16:31 Mit 20:29Mvi ni taji ya utukufu;
hupatikana kwa maisha ya uadilifu.
16:32 Mit 19:11Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa,
mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji.
16:33 Yos 7:14; Yn 1:7Kura hupigwa kwa siri,
lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana.
Mithali 17:1-4
17:1 Mit 15:16, 17; 16:8Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu
kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi.
17:2 Mit 10:5; 19:26Mtumishi mwenye hekima atatawala juu ya mwana aaibishaye,
naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu.
17:3 Mit 27:21; Yer 17:10; 1Pet 1:7; Za 26:2Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu,
bali Bwana huujaribu moyo.
Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya;
mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara.