Mithali 15:31-33
15:31 Mit 9:7-9; 12:1Yeye asikilizaye maonyo yatoayo uzima
atakuwa miongoni mwa wenye hekima.
15:32 Mit 1:7; 12:1; Mhu 7:5Yeye anayedharau maonyo hujidharau mwenyewe,
bali yeyote anayekubali maonyo hupata ufahamu.
15:33 Mit 29:23; Isa 66:2Kumcha Bwana humfundisha mtu hekima,
nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.
Mithali 16:1-7
16:1 Mt 10:19; Mit 19:21Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu,
bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.
16:2 1Sam 16:7; 2Nya 6:30; Lk 16:15; Dan 5:27Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe,
bali makusudi hupimwa na Bwana.
16:3 2Nya 20:20; Za 20:4Mkabidhi Bwana lolote ufanyalo,
nayo mipango yako itafanikiwa.
16:4 Isa 43:7; Kut 9:16; 2Nya 34:24; Rum 9:22Bwana hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe;
hata waovu kwa siku ya maangamizi.
16:5 Za 40:4; Mit 6:16; 11:20-21Bwana huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo.
Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa.
16:6 Kut 20:20; Mit 14:16; Dan 4:26Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa;
kwa kumcha Bwana mtu hujiepusha na ubaya.
16:7 Kol 1:10; Mwa 39:21; Za 105:15; Yer 39:12; 40:1; 42:12; Dan 1:9Njia za mtu zinapompendeza Bwana,
huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani.