Mithali 15:11-20 NEN

Mithali 15:11-20

15:11 Ay 26:6; Za 139:8; Isa 2:3; Yn 2:24; Ufu 2:23Mauti15:11 Yaani Sheol, maana yake ni Kuzimu. na Uharibifu15:11 Kwa Kiebrania ni Abadon. viko wazi mbele za Bwana:

je, si zaidi sana mioyo ya wanadamu!

Mwenye mzaha huchukia maonyo;

hatataka shauri kwa mwenye hekima.

Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke,

bali maumivu ya moyoni huponda roho.

Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa,

bali kinywa cha mpumbavu hujilisha upumbavu.

Siku zote za wanaoonewa ni za taabu,

bali moyo mchangamfu una karamu ya kudumu.

15:16 Za 18:17; 1Tim 6:6; Mit 16:8Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana,

kuliko mali nyingi pamoja na ghasia.

15:17 Mit 17:1; Mhu 4:6Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo

kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki.

15:18 Mit 14:17; 26:21; Mwa 13:8; Mit 6:16-19; 14:17; Mwa 13:8Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi,

bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi.

15:19 Mit 22:5Njia ya mvivu imezibwa na miiba,

bali njia ya mwenye haki ni barabara kuu.

15:20 Mit 10:1Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake,

bali mtu mpumbavu humdharau mama yake.

Read More of Mithali 15