Mithali 15:1-10 NEN

Mithali 15:1-10

15:1 Mit 25:15; 2Nya 10:7; 1Fal 12:7Jawabu la upole hugeuza ghadhabu,

bali neno liumizalo huchochea hasira.

15:2 Mit 12:23; Mhu 10:12; Za 59:7Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa,

bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu.

15:3 2Nya 16:9; Ay 34:21; Ebr 4:13; Mit 5:21; Yer 16:17Macho ya Bwana yako kila mahali,

yakiwaangalia waovu na wema.

15:4 Za 5:9; Mit 10:11; 12:18Ulimi uletao uponyaji ni mti wa uzima,

bali ulimi udanganyao huponda roho.

Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake,

bali yeyote akubaliye maonyo huonyesha busara.

15:6 Mit 8:21; 10:16Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa,

bali mapato ya waovu huwaletea taabu.

15:7 Mit 15:2; 10:13Midomo ya mwenye hekima hueneza maarifa,

bali sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu.

15:8 Isa 61:8; Yer 6:20; Ay 35:13; Yn 9:31; Amo 5:22Bwana huchukia sana dhabihu za waovu,

bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu.

15:9 Kum 7:13; 1Tim 6:11; Isa 51:1-7Bwana huchukia sana njia ya waovu,

bali huwapenda wale wafuatao haki.

15:10 Mit 15:13; 17:22Adhabu kali humngoja yeye aachaye njia;

yeye achukiaye maonyo atakufa.

Read More of Mithali 15