Mithali 14:4-14
14:4 Za 12:2; Mit 12:17Pale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu,
bali kutokana na nguvu za fahali huja mavuno mengi.
14:5 Kut 20:16; Za 12:2; Mit 6:19Shahidi mwaminifu hadanganyi,
bali shahidi wa uongo humimina uongo.
14:6 Mit 9:9; 17:24Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati,
bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua.
Kaa mbali na mtu mpumbavu,
kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake.
14:8 Lk 12:20; 1Kor 3:19; Mit 15:28; 21:29Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake,
bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.
14:9 Mit 1:22; 10:23Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka dhambi,
bali wema hupatikana miongoni mwa wanyofu.
Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe,
wala hakuna yeyote awezaye kushiriki furaha yake.
14:11 Za 72:7; Ay 8:15; Mit 3:33Nyumba ya mwovu itaangamizwa,
bali hema la mnyofu litastawi.
14:12 Rum 6:21; Mit 12:15; 16:25Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu,
bali mwisho wake huelekeza mautini.
14:13 Mhu 2:2; 7:3-6Hata katika kicheko moyo waweza kuuma,
nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi.
14:14 2Nya 15:7; Mit 12:14Wasio na imani watapatilizwa kikamilifu kwa ajili ya njia zao,
naye mtu mwema atapewa thawabu kwa ajili ya njia yake.