Mithali 14:25-35
14:25 Mit 12:17Shahidi wa kweli huokoa maisha,
bali shahidi wa uongo ni mdanganyifu.
14:26 Mit 19:23; Isa 33:6Yeye amchaye Bwana ana ngome salama,
na kwa watoto wake itakuwa kimbilio.
14:27 Za 18:5; Mit 13:14Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima,
ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.
14:28 2Sam 19:7Wingi wa watu ni utukufu wa mfalme,
bali pasipo watu mkuu huangamia.
14:29 Mhu 7:8-9; Mit 15:18; Yak 1:19Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi,
bali anayekasirika haraka huonyesha upumbavu.
14:30 Ay 5:2; Mdo 7:9; Mit 12:4Moyo wenye amani huupa mwili uzima,
bali wivu huozesha mifupa.
14:31 Ay 31:15-16; Mit 17:5Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao,
bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu.
14:32 Za 34:21; Mit 6:15; Ay 13:15; 2Tim 4:18Waovu huangamizwa kwa matendo yao maovu,
bali hata katika kifo wenye haki hupata kimbilio.
14:33 Mit 2:6-10Hekima hukaa katika moyo wa mwenye ufahamu
bali haijulikani miongoni mwa wapumbavu.
14:34 Mit 11:11Haki huinua taifa,
bali dhambi ni aibu kwa watu wote.
14:35 Es 8:2; Mt 25:14-30Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye hekima,
bali ghadhabu yake humwangukia
mtumishi mwenye kuaibisha.