Mithali 14:15-24 NEN

Mithali 14:15-24

14:15 Mit 14:8Mtu mjinga huamini kila kitu,

bali mwenye busara hufikiria hatua zake.

14:16 Kut 20:20; Mit 22:3Mtu mwenye hekima humcha Bwana na kuepuka mabaya,

bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe.

14:17 Mit 28:25; 29:22Mtu anayekasirika kwa haraka hufanya mambo ya upumbavu,

naye mtu wa hila huchukiwa.

Mjinga hurithi upumbavu,

bali wenye busara huvikwa maarifa kichwani kama taji.

14:19 Mit 11:29Watu wabaya watasujudu mbele ya watu wema,

nao waovu kwenye malango ya wenye haki.

14:20 Mit 19:4, 7Maskini huepukwa hata na majirani zao,

bali matajiri wana marafiki wengi.

14:21 Mit 11:12; 19:17; Za 41:1Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi,

bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji.

14:22 Mit 4:16-17Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki?

Bali wale wanaopanga kilicho chema

hupata upendo na uaminifu.

Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida,

bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu.

14:24 Mit 14:8Utajiri wa wenye hekima ni taji yao,

bali upumbavu wa wapumbavu huzaa upumbavu.

Read More of Mithali 14