Mithali 13:10-19 NEN

Mithali 13:10-19

13:10 Amu 19:30; Mit 9:9Kiburi huzalisha magomvi tu,

bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri.

13:11 Mit 10:2; 9:9; 20:21Fedha isiyo ya halali hupungua,

bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka.

13:12 Mit 10:11Kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua,

bali tumaini lililotimizwa ni mti wa uzima.

13:13 Hes 15:31; Kut 9:20; Mit 16:20; 2Nya 36:16Yeye anayedharau mafundisho anajiletea maangamizi,

bali yeye anayeheshimu agizo hupewa tuzo.

13:14 Mit 10:11; 14:27Mafundisho ya mwenye busara ni chemchemi ya uzima,

ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.

Ufahamu mzuri hupata upendeleo,

bali njia ya asiye mwaminifu ni ngumu.

13:16 Es 5:11; Mit 12:23Kila mwenye busara hutenda kwa maarifa,

bali mpumbavu hudhihirisha upumbavu wake.

13:17 Mit 10:26; 25:13Mjumbe mwovu huanguka kwenye taabu,

bali mjumbe mwaminifu huleta uponyaji.

13:18 Mit 15:31-32; Za 141:5Yeye anayedharau maonyo hupata umaskini na aibu,

bali yeye anayekubali maonyo huheshimiwa.

13:19 Mit 10:11Tarajio lililotimizwa ni tamu kwa nafsi,

bali wapumbavu huchukia sana kuacha ubaya.

Read More of Mithali 13