Mithali 12:8-17 NEN

Mithali 12:8-17

12:8 1Sam 13:13; Mal 2:8-9; Mt 27:4-5Mtu husifiwa kulingana na hekima yake,

bali watu wenye akili zilizopotoka hudharauliwa.

Heri mtu wa hali ya chini mwenye mtumishi,

kuliko kujifanya mtu wa hali ya juu nawe huna chakula.

12:10 Kum 25:4; Hes 22:29Mtu mwenye haki hujali mahitaji ya mnyama wake,

bali matendo ya huruma ya mwovu ni ukatili.

12:11 Mwa 3:19; Efe 4:28Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,

bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili.

12:12 Za 1:3; Lk 8:15Waovu hutamani mateka ya watu wabaya,

bali shina la mwenye haki hustawi.

12:13 Za 59:12; Mit 10:6; 21:23; 2Pet 2:9Mtu mwovu hunaswa kwa mazungumzo yake ya dhambi,

bali mwenye haki huepuka taabu.

12:14 Mit 15:23; 14:14; Isa 3:10-11Kutokana na tunda la midomo yake

mtu hujazwa na mambo mema,

hakika kama ilivyo kazi ya mikono yake humtunza.

12:15 Mit 16:2, 25; Lk 18:11Njia ya mpumbavu huonekana sawa

machoni pake mwenyewe,

bali mtu mwenye hekima husikiliza ushauri.

12:16 1Sam 25:25; Ay 5:2; Mit 29:11Mpumbavu huonyesha kuudhika kwake mara moja,

bali mtu wa busara hupuuza matukano.

12:17 Za 12:2; Mit 14:5, 25Shahidi wa kweli hutoa ushuhuda wa kuaminika,

bali shahidi wa uongo husema uongo.

Read More of Mithali 12