Mithali 12:18-27 NEN

Mithali 12:18-27

12:18 Za 57:4; Mit 25:18; 15:4Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga,

bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.

12:19 Zek 1:5, 6Midomo isemayo kweli hudumu milele,

bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu.

12:20 Rum 14:19Upo udanganyifu katika mioyo

ya wale ambao hupanga mabaya,

bali kuna furaha kwa wale wanaoleta amani.

12:21 Ay 4:7; Za 91:10; Rum 8:28Hakuna dhara linalompata mwenye haki,

bali waovu wana taabu nyingi.

12:22 1Fal 13:18; Ufu 22:15; Mit 11:20Bwana anachukia sana midomo idanganyayo,

bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.

12:23 Mit 10:14; Za 38:5; 59:7; Mit 18:2Mtu mwenye busara hujihifadhia maarifa yeye mwenyewe,

bali moyo wa wapumbavu hububujika upumbavu.

12:24 Mit 10:4; 1Fal 11:28Mikono yenye bidii itatawala,

bali uvivu huishia katika kazi za utumwa.

12:25 Mit 15:13; Isa 50:4Moyo wa wasiwasi humlemea mtu,

bali neno la huruma humfurahisha.

12:26 Za 95:10Mtu mwenye haki ni mwangalifu katika urafiki,

bali njia ya waovu huwapotosha.

Mtu mvivu haoki mawindo yake,

bali mtu mwenye bidii ana mali za thamani.

Read More of Mithali 12