Mithali 11:9-18
11:9 Mit 12:6; Yer 45:5; Ay 8:13Kwa kinywa chake mtu asiyemwamini Mungu
humwangamiza jirani yake,
bali kwa maarifa mwenye haki huokolewa.
11:10 2Fal 11:20; Mit 28:12; Es 8:15Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi;
mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha.
11:11 Mit 14:34; 29:8Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa,
bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa.
11:12 Mit 14:21; Ay 6:24Mtu asiye na akili humdharau jirani yake,
bali mtu mwenye ufahamu huuzuia ulimi wake.
11:13 Law 19:16; 1Tim 5:13; Mit 20:19; 10:14Masengenyo husaliti tumaini,
bali mtu mwaminifu hutunza siri.
11:14 Mit 20:18; 24:6; 2Sam 15:34; 1Fal 12:1; Mit 20:18; 2Sam 15:34; Mit 15:22; 24:6; 1Fal 12:1Pasipo ushauri wa hekima taifa huanguka,
bali washauri wengi hufanya ushindi uwe wa hakika.
11:15 Mit 6:1; 17:18; 22:26-27Yeye amdhaminiye mgeni hakika atateseka,
bali yeyote akataaye kuunga mkono dhamana ni salama.
11:16 Mit 31:31Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima,
bali wanaume wakorofi hupata mali tu.
11:17 Mt 25:34Mwenye huruma hujinufaisha mwenyewe,
bali mkatili hujiletea taabu mwenyewe.
11:18 Hos 10:12; Kut 1:20; Ay 4:8Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu,
bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.