Mithali 11:29-31, Mithali 12:1-7 NEN

Mithali 11:29-31

11:29 Mhu 5:16; Mit 14:19Yeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo,

naye mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye hekima.

11:30 Mwa 2:9; Yak 5:20Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima,

naye mwenye hekima huvuta roho za watu.

11:31 Yer 25:29; 49:12; 1Pet 4:18Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani,

si zaidi sana yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?

Read More of Mithali 11

Mithali 12:1-7

Mafundisho Ya Kifamilia Na Ya Kijamii

12:1 Mit 5:11-14; 9:7-9; 13:1, 18; 15:5, 10Yeyote apendaye kuadibishwa hupenda maarifa,

bali yeye achukiaye kuonywa ni mpumbavu.

12:2 Ay 33:26; Za 84:11; 2Sam 15:3; Mit 11:20Mtu mwema hupata kibali kutoka kwa Bwana,

bali Bwana humhukumu mwenye hila.

12:3 Mit 10:25Mtu hathibitiki kutokana na uovu,

bali mwenye haki hataondolewa.

12:4 Mit 14:30; 31:23; 1Kor 11:7; Rum 3:11Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe,

bali aaibishaye ni kama uozo

katika mifupa ya mumewe.

Mipango ya mtu mwadilifu ni ya haki,

bali ushauri wa mwovu ni udanganyifu.

12:6 Mit 11:9; 14:3Maneno ya waovu huotea kumwaga damu,

bali maneno ya waadilifu huwaokoa.

12:7 Mt 7:24; Za 37:34; Mit 14:11; 15:25Watu waovu huondolewa na kutoweka,

bali nyumba ya mwenye haki husimama imara.

Read More of Mithali 12