Mithali 10:31-32
10:31 Mit 10:13; 15:2; 31:26; Za 52:4Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima,
bali ulimi wa upotovu utakatwa.
10:32 Mhu 10:12; Za 59:7Midomo ya wenye haki inajua kile kinachofaa,
bali kinywa cha mwovu hujua kile kilichopotoka tu.
Mithali 11:1-8
11:1 Law 19:36; Ay 6:2; Mit 16:11; Eze 45:10Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu,
bali vipimo sahihi ni furaha yake.
11:2 Dan 4:30; Mit 16:18; 18:12Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu,
bali unyenyekevu huja na hekima.
11:3 Mit 13:6Uadilifu wa wenye haki huwaongoza,
bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.
11:4 Ay 20:20; Eze 7:19; Sef 1:18Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu,
bali haki huokoa kutoka mautini.
11:5 1Fal 8:36; Mit 5:21-23; 13:6; 21:7Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka,
bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe.
11:6 Es 7:9; 1Tim 4:8; Mhu 10:8Haki ya wanyofu huwaokoa,
bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya.
11:7 Ay 8:13; Mit 10:28Wakati mtu mwovu anapokufa, matumaini yake hutoweka;
yote aliyoyatazamia kutokana na nguvu zake huwa si kitu.
11:8 Mit 21:8Mtu mwenye haki huokolewa kutoka taabu,
naye mtu mwovu huingia humo badala yake.