Mithali 10:21-30 NEN

Mithali 10:21-30

10:21 Isa 5:13; Yer 5:4Midomo ya mwenye haki hulisha wengi,

lakini wapumbavu hufa kwa kukosa ufahamu.

10:22 Mwa 12:2; 13:2; Za 37:22; Kum 8:17-18Baraka ya Bwana hutajirisha,

wala haichanganyi huzuni.

10:23 Mit 2:14Mpumbavu hufurahia tabia mbaya,

lakini mtu mwenye ufahamu hupendezwa na hekima.

10:24 Isa 66:4; Mt 5:6; Ay 15:21Kile anachoogopa mwovu ndicho kitakachompata;

kile anachoonea shauku mwenye haki atapewa.

10:25 Za 20:8; Mt 7:24-27Tufani inapopita, waovu hutoweka,

lakini wenye haki husimama imara milele.

10:26 Isa 65:5; Mit 13:17; 25:13; 26:6Kama siki ilivyo kwa meno na moshi kwa macho,

ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma.

10:27 Kum 11:9; Mit 22:4; Mhu 7:17; Ay 15:32Kumcha Bwana huongeza urefu wa maisha,

lakini miaka ya mwovu inafupishwa.

10:28 Es 7:10; Ay 8:13; Za 16:9Tarajio la mwenye haki ni furaha,

bali matumaini ya mwovu huwa si kitu.

10:29 Za 10:12; Mit 21:15; Hos 14:9Njia ya Bwana ni kimbilio kwa wenye haki,

lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya.

10:30 Za 37:28-29; Mit 2:20-22Kamwe wenye haki hawataondolewa,

bali waovu hawatasalia katika nchi.

Read More of Mithali 10