Mithali 10:1-10
Mithali Za Solomoni
10:1 1Fal 4:32; Mit 1:1; 15:20; 17:21; 19:13; 23:22; 27:11; 29:3Mithali za Solomoni:
Mwana mwenye hekima
huleta furaha kwa baba yake,
lakini mwana mpumbavu
huleta huzuni kwa mama yake.
10:2 Dan 4:27; Mit 13:11; 21:6; 12:28; Lk 12:29Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai,
lakini uadilifu huokoa kutoka mautini.
10:3 Za 10:14; Mt 6:25-34Bwana hawaachi waadilifu kukaa njaa,
lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu.
10:4 Mit 24:30-34; 13:4Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini
lakini mikono yenye bidii huleta utajiri.
10:5 Mit 24:30-34Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi
ni mwana mwenye hekima,
lakini yeye alalaye wakati wa mavuno
ni mwana mwenye kuaibisha.
10:6 Es 7:8; Mit 13:3; Mhu 10:12Baraka huwa taji kichwani mwa mwenye haki,
lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu.
10:7 Mhu 8:10; Ay 18:17; Za 109:13Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka,
lakini jina la mwovu litaoza.
10:8 Ay 33:33; Mt 7:24-27Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo,
lakini mpumbavu apayukaye huangamia.
10:9 Za 23:4; 25:21; Isa 33:15; Mit 28:18Mtu mwadilifu hutembea salama,
lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.
10:10 Za 35:19Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni,
naye mpumbavu apayukaye huangamia.