Mithali 1:20-33
Onyo Dhidi Ya Kukataa Hekima
1:20 Ay 28:12; Mt 7:10-13; 9:1-3, 13-15Hekima huita kwa sauti kuu barabarani,
hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa;
kwenye makutano ya barabara za mji
zenye makelele mengi hupaza sauti,
kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake:
1:22 Mit 6:32; 7:7; 8:5; 9:4, 16; Za 50:17“Enyi wajinga, mtangʼangʼania ujinga wenu hadi lini?
Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha,
na wapumbavu kuchukia maarifa?
1:23 Yoe 2:28; Yn 7:37Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu,
ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu
na kuwafahamisha maneno yangu.
1:24 Isa 65:12; Zek 7:11Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita
na hakuna yeyote aliyekubali
niliponyoosha mkono wangu,
1:25 Lk 7:30kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote
na hamkukubali karipio langu,
1:26 Za 2:4; Kum 28:63; Mit 10:24mimi nami nitawacheka katika maafa yenu,
nitawadhihaki wakati janga litawapata:
1:27 Za 18:18; Mit 5:12-14wakati janga litawapata kama tufani,
wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli,
wakati dhiki na taabu zitawalemea.
1:28 Isa 1:15; Mik 3:4; Eze 8:18; Hos 5:6“Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu;
watanitafuta lakini hawatanipata.
1:29 Ay 21:14; Isa 27:11; Mdo 7:51Kwa kuwa walichukia maarifa,
wala hawakuchagua kumcha Bwana,
1:30 Ay 21:14; Za 81:11kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu,
na kukataa maonyo yangu,
1:31 2Nya 36:16; Yer 14:16watakula matunda ya njia zao,
na watashibishwa matunda ya hila zao.
1:32 Isa 66:4; Yer 2:19Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua,
nako kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza.
1:33 Hes 24:21; Za 25:12; 112:8Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama,
atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.”