Mithali 6:30-35
Watu hawamdharau mwizi kama akiiba
kukidhi njaa yake wakati ana njaa.
6:31 Kut 22:1-14Pamoja na hayo, kama akikamatwa,
lazima alipe mara saba,
ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake.
6:32 Kut 20:14; Mit 7:7; 9:4, 16Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.
6:33 Mit 5:9-14Mapigo na aibu ni fungu lake
na aibu yake haitafutika kamwe;
6:34 Hes 5:14; Mwa 34:7kwa maana wivu huamsha ghadhabu ya mume,
naye hataonyesha huruma alipizapo kisasi.
6:35 Ay 31:9-11; Wim 8:7Hatakubali fidia yoyote;
atakataa malipo, hata yakiwa makubwa kiasi gani.