Mithali 30:11-23
30:11 Mit 20:20“Wako watu wale ambao huwalaani baba zao
na wala hawawabariki mama zao;
30:12 Lk 18:11; Mit 16:2; Yer 2:23-35wale ambao ni safi machoni pao wenyewe
kumbe hawakuoshwa uchafu wao;
30:13 Ay 41:34wale ambao daima macho yao ni ya kiburi,
ambao kutazama kwao ni kwa dharau;
30:14 Ay 24:9; 29:17; Za 14:4; 57:4; Amo 8:4; Mik 2:2wale ambao meno yao ni panga
na ambao mataya yao yamewekwa visu
kuwaangamiza maskini katika nchi,
na wahitaji kutoka miongoni mwa wanadamu.
30:15 Mit 27:20“Mruba anao binti wawili waliao,
‘Nipe! Nipe!’
“Kuna vitu vitatu visivyotosheka kamwe,
naam, viko vinne visivyosema, ‘Yatosha!’:
30:16 Isa 5:14; Hab 2:5Ni kaburi, tumbo lisilozaa,
nchi isiyoshiba maji kamwe,
na moto, usiosema kamwe, ‘Yatosha!’
30:17 Kum 21:18-21; Mit 20:20; Law 20:9; Ay 15:23“Jicho lile limdhihakilo baba,
lile linalodharau kumtii mama,
litangʼolewa na kunguru wa bondeni,
litaliwa na tai.
“Kuna vitu vitatu vinavyonishangaza sana,
naam, vinne nisivyovielewa:
Ni mwendo wa tai katika anga,
mwendo wa nyoka juu ya mwamba,
mwendo wa meli katika maji makuu ya bahari,
nao mwendo wa mtu pamoja na msichana.
30:20 Mit 5:6“Huu ndio mwendo wa mwanamke mzinzi,
hula akapangusa kinywa chake na kusema,
‘Sikufanya chochote kibaya.’
“Kwa mambo matatu nchi hutetemeka,
naam, kwa mambo manne haiwezi kuvumilia:
30:22 Mit 19:10; 29:2; Mhu 10:7Mtumwa awapo mfalme,
mpumbavu ashibapo chakula,
mwanamke asiyependwa aolewapo,
naye mtumishi wa kike achukuapo nafasi ya bibi yake.