Mithali 13:20-25
13:20 2Nya 10:8Yeye atembeaye na mwenye hekima atapata hekima,
bali rafiki wa mpumbavu hupata madhara.
13:21 Za 32:10; Mit 19:17; 11:12Balaa humwandama mtenda dhambi,
bali mafanikio ni thawabu kwa mwenye haki.
13:22 Es 8:2; Mhu 2:26Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi,
bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa
kwa ajili ya wenye haki.
13:23 Mit 12:11Shamba la mtu maskini laweza kuzalisha chakula kingi,
bali dhuluma hukifutilia mbali.
13:24 Mit 29:15-17; Efe 6:4Yeye aizuiaye fimbo yake hampendi mwanawe,
bali yeye ampendaye
huwa mwangalifu kumwadibisha.
13:25 Za 34:10; Mit 10:3Mwenye haki hula mpaka akaridhisha moyo wake,
bali tumbo la mwovu hutaabika kwa njaa.
Mithali 14:1-4
14:1 Rut 3:11; Mit 24:3Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake,
bali mpumbavu huibomoa nyumba yake
kwa mikono yake mwenyewe.
14:2 Ay 12:4Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha Bwana,
bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu.
14:3 Mit 12:6; 10:13Mazungumzo ya mpumbavu huleta fimbo mgongoni mwake,
bali mwenye hekima hulindwa na maneno ya midomo yake.
14:4 Za 12:2; Mit 12:17Pale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu,
bali kutokana na nguvu za fahali huja mavuno mengi.