Hesabu 7:1-65 NEN

Hesabu 7:1-65

Sadaka Wakati Wa Kuweka Wakfu Maskani Ya Bwana

7:1 Kut 40:9, 10, 17; 30:26; 2Nya 7:9; 1Fal 8:64Mose alipomaliza kuisimamisha Maskani, aliitia mafuta na kuiweka wakfu pamoja na samani zake zote. Pia alitia madhabahu mafuta na kuiweka wakfu, pamoja na vyombo vyake vyote. 7:2 Hes 1:5-16, 19; Kut 35:27; 1Nya 29:6-8; Ezr 2:68-69; Neh 7:70-72Ndipo viongozi wa Israeli, wale wakuu wa jamaa waliokuwa viongozi wa kabila wasimamizi wa wale waliohesabiwa, wakatoa sadaka. 7:3 Mwa 45:19; 1Sam 6:7-14; 1Nya 13:6-7Walizileta kama matoleo yao mbele za Bwana: magari sita ya kukokotwa yaliyofunikwa, pamoja na maksai kumi na wawili; yaani maksai mmoja kutoka kwa kila kiongozi, na gari moja la kukokotwa kutoka kwa kila viongozi wawili. Haya waliyaleta mbele ya Maskani.

Bwana akamwambia Mose, “Vikubali vitu hivi kutoka kwao, ili viweze kutumika katika kazi kwenye Hema la Kukutania. Wapatie Walawi kama kazi ya kila mtu itakavyohitaji.”

Hivyo Mose akachukua yale magari ya kukokotwa pamoja na maksai, na kuwapa Walawi. 7:7 Hes 4:24-28Aliwapa Wagershoni magari mawili ya kukokotwa na maksai wanne, kama walivyohitaji kwa kazi yao, 7:8 Hes 4:31-33na pia aliwapa Wamerari magari manne ya kukokotwa na maksai wanane, kama kazi yao ilivyohitaji. Wote walikuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani, Aroni. 7:9 Hes 4:4, 15; 1Nya 23:26; 2Sam 6:13Lakini Mose hakuwapa Wakohathi chochote kati ya hivyo, kwa sababu walitakiwa kubeba vitu vitakatifu mabegani mwao, vile walikuwa wanawajibika.

7:10 Hes 7:1; Kut 29:36; 2Nya 7:9; Kum 20:5; Ezr 6:16Wakati madhabahu yalitiwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu. 7:11 1Kor 14:33Kwa maana Bwana alikuwa amemwambia Mose, “Kila siku kiongozi mmoja ataleta sadaka yake ili kuwekwa wakfu madhabahu.”

7:12 Hes 1:7Yule ambaye alileta sadaka yake siku ya kwanza alikuwa Nashoni, mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda.

7:13 Kut 27:3; 30:13; Law 27:3-7; 2:1; Hes 6:15; 15:14; Ezr 8:25; Yer 52:19Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130,7:13 Shekeli 130 za fedha ni sawa na kilo 1.5. na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini,7:13 Shekeli 70 za fedha ni sawa gramu 800. vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 7:14 1Fal 7:50; 2Fal 25:14; 2Nya 4:22; 24:14; Kut 25:6; 30:34; Eze 18:16; Mal 1:11; Ufu 5:8sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi,7:14 Shekeli 10 za dhahabu ni sawa na gramu 110. likiwa limejazwa uvumba; 7:15 Kut 24:5; 29:3; Hes 28:11; Law 1:3fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 7:16 Law 4:3mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 7:17 Law 3:1; Hes 1:77:17 Lk 3:32maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.

7:18 Hes 1:8Siku ya pili yake Nethaneli mwana wa Suari, kiongozi wa kabila la Isakari, alileta sadaka yake.

Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 7:21 Mwa 8:20; Za 20:1-3; 50:19; Efe 5:2; Ebr 9:13fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 7:23 1Fal 8:63; Law 7:11-13; Mit 7:14; Kol 1:20maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Nethaneli mwana wa Suari.

7:24 Hes 1:9Siku ya tatu Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa kabila la Zabuloni, alileta sadaka yake.

7:25 Isa 53:7; Mdo 8:32; Ufu 5:6-11; 13:8Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Eliabu mwana wa Heloni.

7:30 Hes 1:5Siku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, kiongozi wa kabila la Reubeni, alileta sadaka yake.

Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Elisuri mwana wa Shedeuri.

7:36 Hes 1:6Siku ya tano Shelumieli mwana wa Surishadai, kiongozi wa watu wa Simeoni, alileta sadaka yake.

Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 7:39 Kut 12:5; Ebr 9:28; 1Pet 3:18fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Shelumieli mwana wa Surishadai.

7:42 Hes 1:14Siku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, kiongozi wa watu wa Gadi, alileta sadaka yake.

7:43 Law 2:5; 14:10Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 7:45 Za 40:6; 51:16; Isa 53:4; Yer 7:22; Amo 5:22fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Eliasafu mwana wa Deueli.

7:48 Hes 1:10; 2:18; 1Nya 7:26Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa watu wa Efraimu, alileta sadaka yake.

Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 7:50 Kum 33:10; Za 66:15; Lk 1:10sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 7:51 Mik 6:6-8fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Elishama mwana wa Amihudi.

7:54 Hes 1:10Siku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, kiongozi wa watu wa Manase, alileta sadaka yake.

Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 7:56 Kut 30:7sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 7:57 Kut 12:5; Mdo 8:32; 1Pet 1:19fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Gamalieli mwana wa Pedasuri.

7:60 Hes 1:11Siku ya tisa Abidani mwana wa Gideoni, kiongozi wa watu wa Benyamini, alileta sadaka yake.

Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 7:62 Isa 66:20; Dan 9:27; Rum 15:16; Ebr 13:15; Ufu 8:3-4sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 7:63 Za 40:6; Isa 53:4; 2Kor 5:21fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 7:65 Mit 7:14; Eze 45:17; Kol 1:20maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Abidani mwana wa Gideoni.

Read More of Hesabu 7