Hesabu 5:11-31, Hesabu 6:1-27 NEN

Hesabu 5:11-31

Jaribio Kwa Ajili Ya Mke Asiye Mwaminifu

Kisha Bwana akamwambia Mose, 5:12 Kut 20:14; Mit 2:16; 7:10-27; Hos 4:13“Nena na Waisraeli uwaambie: ‘Ikiwa mke wa mtu amepotoka na si mwaminifu kwa mumewe, 5:13 Kut 20:14; Law 18:20; 18:20; 20:10; Mit 30:20kwa kukutana kimwili na mwanaume mwingine, tendo hili likafichika kwa mumewe na unajisi wake usigundulike (kwa kuwa hakuna ushahidi dhidi yake, naye hakukamatwa katika tendo hilo), 5:14 Mit 6:34; 27:4; Wim 8:6; Isa 19:14nazo hisia za wivu zikamjia mumewe na kumshuku mkewe, naye mke yule ni najisi, au mumewe ana wivu na akamshuku ingawa si najisi, 5:15 Kut 16:36; Law 6:20; Eze 21:23; 29:16; Law 5:11; 1Fal 17:18basi atampeleka mkewe kwa kuhani. Huyo mume itampasa apeleke pia sadaka ya unga wa shayiri kiasi cha sehemu ya kumi ya efa5:15 Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja. kwa niaba ya mkewe. Huyo mwanaume kamwe asimimine mafuta juu ya huo unga wala asiweke uvumba juu yake, kwa sababu ni sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu, sadaka ya ukumbusho ili kukumbushia uovu.

5:16 Yer 17:10; 1Nya 28:9; Ebr 13:4“ ‘Kuhani atamleta huyo mwanamke na kumsimamisha mbele za Bwana. Kisha kuhani atachukua sehemu ya maji matakatifu ndani ya gudulia la udongo na kuchanganya na baadhi ya vumbi kutoka sakafu ya Maskani. 5:18 Law 10:6; 1Kor 11:6Baada ya kuhani kumsimamisha huyo mwanamke mbele za Bwana, atazifungua nywele za huyo mwanamke na kuweka sadaka ya ukumbusho mikononi mwake, ile sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu, huku kuhani mwenyewe akishikilia yale maji machungu yaletayo laana. Kisha kuhani atamwapiza huyo mwanamke, akimwambia, “Ikiwa hakuna mwanaume mwingine aliyekutana kimwili nawe, wala hujapotoka na kuwa najisi wakati ukiwa umeolewa na mumeo, maji haya machungu yaletayo laana na yasikudhuru. Lakini ikiwa umepotoka wakati ukiwa umeolewa na mume wako na umejinajisi mwenyewe kwa kukutana kimwili na mwanaume mwingine asiyekuwa mumeo”; 5:21 Yos 6:26; 1Sam 14:24; Neh 10:29; Mwa 9:25; Isa 65:15; Yer 29:22hapa kuhani atamweka huyo mwanamke chini ya laana ya kiapo akisema: “Bwana na awafanye watu wako wakulaani na kukukataa, wakati Bwana atakapolifanya paja lako kupooza na tumbo lako kuvimba. 5:22 Za 109:18; Kum 27:15Maji haya yaletayo laana na yaingie ndani ya mwili wako ili tumbo lako livimbe na paja lako lipooze.”5:22 Paja lipooze hapa ina maana ya kuwa tasa au kuharibu mimba.

“ ‘Kisha mwanamke atasema, “Amen. Iwe hivyo.”

5:23 Yer 45:1“ ‘Kuhani ataandika laana hizi kwenye kitabu, kisha atazioshea laana hizo kwenye yale maji machungu. Kuhani atamnywesha yule mwanamke yale maji machungu yaletayo laana, nayo maji haya yatamwingia na kumsababishia maumivu makali. 5:25 Law 8:27; Kum 29:24Kuhani atachukua sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu kutoka mikononi mwa huyo mwanamke, naye ataipunga mbele za Bwana na kuileta madhabahuni. Kisha kuhani atachota sadaka ya nafaka mkono uliojaa kama sehemu ya kumbukumbu na kuiteketeza juu ya madhabahu, baada ya hayo, atamtaka huyo mwanamke anywe yale maji. 5:27 Isa 43:28; 65:15; Yer 26:6; 29:18; 42:18; 44:12, 22; Zek 8:13Kama amejitia unajisi na kukosa uaminifu kwa mumewe, wakati anapotakiwa anywe maji yale yaletayo laana, yatamwingia na kusababisha maumivu makali; tumbo lake litavimba na paja lake litapooza, naye atakuwa amelaaniwa miongoni mwa watu wake. 5:28 Ay 17:8-9; Za 47:5-6; Rum 5:3-5Hata hivyo, ikiwa huyo mwanamke hakujitia unajisi, naye ni safi, atasafishwa hatia na ataweza kuzaa watoto.

“ ‘Basi, hii ndiyo sheria ya wivu mwanamke anapopotoka na kujitia unajisi akiwa ameolewa na mumewe, au hisia za wivu zinapomjia mwanaume kwa sababu ya kumshuku mkewe. Kuhani atamfanya huyo mwanamke kusimama mbele za Bwana na atatumia sheria hii yote kwa huyo mwanamke. 5:31 Law 5:1; 20:17; Eze 18:4; Rum 2:8-9Mume atakuwa hana hatia ya kosa lolote, bali mwanamke atayachukua matokeo ya dhambi yake.’ ”

Read More of Hesabu 5

Hesabu 6:1-27

Mnadhiri

Bwana akamwambia Mose, 6:2 Hes 6:5, 6; Mwa 28:20; Mdo 21:23; Amu 13:5; 16:17“Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Ikiwa mwanaume au mwanamke anataka kuweka nadhiri maalum, nadhiri ya kutengwa kwa ajili ya Bwana kama Mnadhiri, 6:3 Law 10:9; 25:5; Lk 1:15; Rut 2:14; Za 69:21; Mit 10:26ni lazima ajitenge na mvinyo na kinywaji kingine chochote chenye chachu, na kamwe asinywe siki itokanayo na mvinyo au itokanayo na kinywaji kingine chenye chachu. Kamwe asinywe maji ya zabibu wala kula zabibu mbichi au kavu. Kwa muda wote atakaokuwa Mnadhiri, kamwe hatakula chochote kitokanacho na mzabibu, sio mbegu wala maganda.

6:5 Za 52:2; 57:4; 59:7; Isa 7:20; Eze 5:1; 1Sam 1:11; Mao 4:7“ ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili ya Bwana, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu mpaka kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili ya Bwana kiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke. 6:6 Law 21:1-3; Hes 19:11-22; Law 19:28; Yer 16:5-6; Eze 24:18; Mt 8:21Kwa kipindi chochote cha kujitenga kwa ajili ya Bwana hatakaribia maiti. 6:7 Hes 9:6Hata kama baba yake mwenyewe au mama au kaka au dada akifa, hatajinajisi mwenyewe kwa taratibu za ibada kwa ajili yao, kwa sababu ishara ya kujiweka wakfu kwake kwa Mungu ipo katika kichwa chake. Kwa kipindi chote cha kujitenga kwake yeye ni wakfu kwa Bwana.

6:9 Law 14:9; Hes 6:18“ ‘Kama mtu yeyote akifa ghafula karibu naye, atakuwa ametiwa unajisi nywele zake alizoziweka wakfu, hivyo ni lazima anyoe nywele zake siku ya utakaso wake, yaani siku ya saba. 6:10 Law 14:10-11; 5:7; 14:22Kisha siku ya nane ni lazima alete hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa kuhani katika mlango wa Hema la Kukutania. 6:11 Kut 29:36; 30:10; Mwa 8:20Kuhani atatoa mmoja kama sadaka ya dhambi, na mwingine kama sadaka ya kuteketezwa ili kufanya upatanisho kwa ajili yake kwa sababu ametenda dhambi kwa kuwepo mbele ya maiti. Siku iyo hiyo atakiweka wakfu kichwa chake. 6:12 Law 12:6; 5:15Ni lazima ajitoe kabisa kwa Bwana kwa kipindi cha kujitenga kwake, na ni lazima atoe mwana-kondoo wa mwaka mmoja kama sadaka ya hatia. Siku zilizopita hazitahesabiwa kwa sababu alijitia unajisi katika siku zake za kujitenga.

6:13 Mdo 21:26; Law 14:11“ ‘Basi hii ndiyo sheria kwa ajili ya Mnadhiri baada ya kipindi chake cha kujitenga kupita. Ataletwa kwenye ingilio la Hema la Kukutania. 6:14 Kut 12:5; Law 4:3; 14:10; 5:15; 3:1Hapo atatoa sadaka zake kwa Bwana: yaani, mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kondoo mke wa mwaka mmoja asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya amani, 6:15 Law 2:1; 6:14; Mwa 35:14; Kut 29:2; Hes 15:1-7; Yn 6:50-53; Isa 62:9; 1Kor 10:31; 11:26pamoja na sadaka zake za nafaka na za vinywaji, na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, yaani maandazi yaliyotengenezwa kwa unga laini uliochanganywa na mafuta, na mikate myembamba iliyopakwa mafuta.

“ ‘Kuhani atavileta vitu hivyo mbele za Bwana na kufanya sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa. 6:17 Kut 29:41; Law 23:13Ataleta pia kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, na atatoa dhabihu kondoo dume kama sadaka ya amani kwa Bwana, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka ya kinywaji.

6:18 Mdo 21:24; Lk 17:10; Rum 6:6; Gal 5:24; Efe 4:23; Kol 3:9“ ‘Kisha kwenye ingilio la Hema la Kukutania, Mnadhiri ni lazima anyoe nywele zake ambazo alikuwa ameziweka wakfu. Atazichukua hizo nywele na kuziweka ndani ya moto ulio chini ya dhabihu ya sadaka ya amani.

6:19 Law 7:12-13“ ‘Baada ya Mnadhiri kunyoa hizo nywele zake za kujitenga kwake, kuhani atampa mikononi mwake bega la kondoo dume lililochemshwa, na pia andazi na mkate mwembamba kutoka kwenye kikapu, vyote vikiwa vimetengenezwa bila kuwekwa chachu. 6:20 Law 7:30; 27:9; 7:34; Mhu 9:7; Isa 35:10; Ufu 14:13Kisha kuhani ataviinua mbele za Bwana kama sadaka ya kuinua; ni vitakatifu na ni mali ya kuhani, pamoja na kile kidari kilichoinuliwa na lile paja lililotolewa. Baada ya hayo, Mnadhiri anaweza kunywa divai.

“ ‘Hii ndiyo sheria ya Mnadhiri ambaye anaweka nadhiri kwa matoleo yake kwa Bwana kufuatana na kujitenga kwake, zaidi ya chochote kile anachoweza kupata. Ni lazima atimize nadhiri aliyoiweka kufuatana na sheria ya Mnadhiri.’ ”

Baraka Ya Kikuhani

Bwana akamwambia Mose, 6:23 Kum 21:5; 1Nya 23:13“Mwambie Aroni na wanawe, ‘Hivi ndivyo mtakavyowabariki Waisraeli. Waambieni:

6:24 Mwa 28:3; Kum 28:3-6; Za 17:9; 28:9; 128:5; 1Sam 2:9“ ‘ “Bwana akubariki

na kukulinda;

6:25 Ay 29:24; Za 4:6; 25:16; 86:16; 31:16; 80:3; 119:29, 135; Mwa 43:29Bwana akuangazie nuru ya uso wake

na kukufadhili;

6:26 Za 4:6; 44:3; 4:8; 29:11; 37:11, 37; 127:2; Isa 14:7; Yer 33:6; Yn 14:27Bwana akugeuzie uso wake

na kukupa amani.” ’

6:27 Kum 28:10; 2Sam 7:23; Neh 9:10; Yer 25:29; Eze 36:23“Hivyo wataliweka Jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.”

Read More of Hesabu 6