Hesabu 4:1-49, Hesabu 5:1-10 NEN

Hesabu 4:1-49

Wakohathi

Bwana akawaambia Mose na Aroni, 4:2 Kut 30:12“Wahesabu Wakohathi walio sehemu ya Walawi kwa koo zao na jamaa zao. 4:3 Hes 1:46; 8:25; 1Nya 23:3, 24-27; Mwa 41:46; Ezr 3:8; Lk 3:23Wahesabu wanaume wote wenye umri wa miaka thelathini hadi hamsini wanaokuja kutumika katika kazi ya Hema la Kukutania.

4:4 Hes 3:28; 7:9“Hii ndiyo kazi ya Wakohathi katika Hema la Kukutania: Watatunza vitu vilivyo vitakatifu sana. 4:5 Kut 25:10, 16; 26:31-33; 1Nya 23:26; Law 16:2; 2Nya 3:14; Mt 27:51Wakati kambi inapohamishwa, Aroni na wanawe wataingia ndani na kushusha lile pazia la kuzuilia na kufunika nalo Sanduku la Ushuhuda. 4:6 Kut 25:5, 13-15; 1Fal 8:7; 2Nya 5:8Kisha watafunika juu yake na ngozi za pomboo,4:6 Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili. na kutandaza juu yake kitambaa cha rangi ya buluu iliyokolea na kuingiza mipiko mahali pake.

4:7 Law 24:6; Kut 25:30; 39:36; Yer 52:19“Juu ya meza ya mikate ya Wonyesho watatandaza kitambaa cha buluu na waweke sahani juu yake, masinia, bakuli na magudulia kwa ajili ya sadaka za kinywaji; mkate ule ambao upo hapa daima utabaki juu yake. 4:8 Kut 26:26-28Juu ya hivyo vitu watatandaza kitambaa chekundu na kufunika kwa ngozi za pomboo na kuweka mipiko yake mahali pake.

4:9 Kut 25:38“Watachukua kitambaa cha buluu na kufunika kinara cha taa kilicho kwa ajili ya nuru, pamoja na taa zake, mikasi yake, sinia zake, magudulia yake yote yaliyotumika kuwekea mafuta. Kisha watakisokotea pamoja na vifaa vyake vyote katika ngozi za pomboo na kukiweka kwenye jukwaa lake.

4:11 Kut 30:1-4“Juu ya madhabahu ya dhahabu watatandaza kitambaa cha buluu na kukifunika kwa ngozi za pomboo na kuweka mipiko yake mahali pake.

4:12 Hes 3:31“Watavichukua vyombo vyote vinavyotumika kuhudumia mahali patakatifu, watavisokotea kwenye kitambaa cha buluu na kufunika kwa ngozi za pomboo, na kuviweka juu ya miti ya kuchukulia.

4:13 Law 1:16; Kut 27:1-8; Hes 3:31“Wataondoa majivu kutoka madhabahu ya shaba na kutandaza kitambaa cha zambarau juu yake. 4:14 Kut 31:9; 27:3, 6; 1Nya 28:17; 2Nya 4:8, 11-16; Hes 7:84; Yer 52:6Kisha wataweka vyombo vyote juu yake vinavyotumika kwa kuhudumia madhabahuni pamoja na vyombo vya kutolea moto, nyuma, miiko na mabakuli ya kunyunyizia. Juu yake watatandaza ngozi za pomboo ya kufunika, na kuweka mipiko mahali pake.

4:15 Hes 3:27; 7:9; Kut 28:43; Hes 1:51; 2Sam 6:6, 7; Kum 31:9; 2Sam 6:6-7, 13; 1Nya 28:12-13“Baada ya Aroni na wanawe kumaliza kazi ya kufunika samani takatifu na vyombo vyake vyote, watu watakapokuwa tayari kungʼoa kambi, Wakohathi watakuja kufanya kazi ya kubeba. Lakini wasije wakagusa vitu vitakatifu la sivyo watakufa. Wakohathi ndio watakaobeba vile vitu vilivyomo katika Hema la Kukutania.

4:16 Law 6:14-23; 10:6; Hes 3:32; Kut 25:6; 29:41“Eleazari mwana wa Aroni, kuhani, ndiye atakayesimamia mafuta kwa ajili ya taa, uvumba wenye harufu nzuri, sadaka za kila siku za nafaka na mafuta ya upako. Ndiye atakayekuwa msimamizi wa maskani yote ya Bwana na kila kitu kilichomo ndani mwake pamoja na samani takatifu na vyombo vyake.”

Bwana akawaambia Mose na Aroni, “Hakikisheni kwamba koo za kabila la Wakohathi hawatengwi kutoka Walawi. 4:19 Hes 3:32Ili wapate kuishi wala wasife wanapokaribia vitu vitakatifu sana, uwafanyie hivi: Aroni na wanawe watakwenda mahali patakatifu na kumgawia kila mtu kazi yake, na kwamba ni nini atakachochukua. 4:20 Kut 19:21; 1Sam 6:19Lakini Wakohathi hawaruhusiwi kuingia ndani ili kuangalia vitu vitakatifu, hata kwa kitambo kidogo, la sivyo watakufa.”

Wagershoni

Bwana akamwambia Mose, “Wahesabu pia Wagershoni kwa jamaa zao na koo zao. 4:23 Hes 4:3; 1Nya 23:3; 24:27Wahesabu wanaume wote wenye umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao huja kutumika katika Hema la Kukutania.

“Hii ndiyo huduma ya koo za Wagershoni wakati wanapofanya kazi na kubeba mizigo. 4:25 Kut 26:14; 27:10-18; Hes 3:25Watabeba mapazia ya maskani. Hema la Kukutania, kifuniko chake na kifuniko cha nje cha ngozi za pomboo, mapazia ya maingilio ya Hema la Kukutania, 4:26 Kut 27:9, 16; Hes 3:26mapazia ya ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pazia la maingilio, kamba na vifaa vyote vinavyotumika katika huduma yake. Wagershoni watafanya yote yatakiwayo kufanyika na vitu hivi. Utumishi wao wote ukiwa ni kuchukua au wa kufanya kazi nyingine, utafanyika chini ya maelekezo ya Aroni na wanawe. Mtawapangia kama wajibu wao yote watakayoyafanya. 4:28 Hes 7:7; Kut 6:23Hii ndiyo huduma ya koo za Wagershoni katika Hema la Kukutania. Wajibu wao utakuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani Aroni.

Wamerari

4:29 Kut 30:12; Mwa 46:11“Wahesabu Wamerari kwa koo zao na jamaa zao. Wahesabu wanaume wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao watakuja kutumika katika Hema la Kukutania. 4:31 Hes 3:36; Kut 26:15; 27:9-19Huu ndio wajibu wao wanapofanya huduma katika Hema la Kukutania: kubeba miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo na vitako, 4:32 Hes 3:37; Kut 25:9; 1Nya 9:29; Ezr 8:24-30nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema, kamba, vifaa vyake vyote na kila kitu kinachohusiana na matumizi yake. Kila mtu mpangie vitu maalum vya kubeba. 4:33 Kut 28:21Huu ndio utumishi wa koo za Merari kama watakavyofanya kazi katika Hema la Kukutania, chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani, Aroni.”

Kuhesabiwa Kwa Koo Za Walawi

4:34 Hes 4:35-40; 1Kor 12:8-12; Kum 33:25Mose, Aroni na viongozi wa jumuiya wakawahesabu Wakohathi kwa koo zao na jamaa zao. Wanaume wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania, waliohesabiwa kwa koo zao, walikuwa 2,750. 4:37 Hes 3:27Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wote wale wa koo za Wakohathi ambao walitumika katika Hema la Kukutania. Mose na Aroni waliwahesabu kufuatana na amri ya Bwana kupitia kwa Mose.

4:38 Mwa 46:11Wagershoni walihesabiwa kwa koo zao na jamaa zao. Watu wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania, waliohesabiwa kwa koo zao na jamaa zao, walikuwa 2,630. Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wale wa koo za Gershoni ambao walitumika katika Hema la Kukutania. Mose na Aroni waliwahesabu kufuatana na amri ya Bwana.

Wamerari walihesabiwa kwa koo zao na jamaa zao. Wanaume wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania, waliohesabiwa kwa koo zao, walikuwa 3,200. Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wale wa koo za Wamerari. Mose na Aroni waliwahesabu kufuatia amri ya Bwana kupitia kwa Mose.

Hivyo Mose, Aroni na viongozi wa Israeli waliwahesabu Walawi wote kwa koo zao na jamaa zao. 4:47 Rum 12:6-8Wanaume wote wenye umri kuanzia miaka thelathini hadi hamsini waliokuja kufanya kazi ya kuhudumu na kubeba Hema la Kukutania 4:48 Hes 3:39walikuwa watu 8,580. 4:49 Hes 1:47; Rum 12:6-8Kwa amri ya Bwana kupitia Mose, kila mmoja aligawiwa kazi yake na kuambiwa kitu cha kubeba.

Hivyo ndivyo walivyohesabiwa kama Bwana alivyomwamuru Mose.

Read More of Hesabu 4

Hesabu 5:1-10

Utakaso Wa Kambi

Bwana akamwambia Mose, 5:2 Law 13:2, 3; 15:2; 21:11; Mt 9:20; Hes 9:6-10; 12:14; Kum 23:10; 2Fal 5:27; 2Nya 26:20; Isa 52:11; Lk 17:12“Waamuru Waisraeli kumtoa nje ya kambi mtu yeyote ambaye ana ugonjwa wa ngozi uambukizao,5:2 Ugonjwa wa ngozi uambukizao hapa ina maana ya ukoma. au anayetokwa na majimaji ya aina yoyote, au ambaye ni najisi kwa utaratibu wa ibada kwa sababu ya maiti. 5:3 Kut 29:45; Law 26:12; 2Kor 6:16; Kut 25:8; Yos 22:19; Eze 37:26-28; Zek 2:10Hii itakuwa ni kwa wote, yaani, wanaume na wanawake; watoeni nje ya kambi ili wasije wakanajisi kambi yao, ambamo ninaishi miongoni mwao.” Waisraeli wakafanya hivyo; wakawatoa nje ya kambi. Wakafanya kama vile Bwana alivyokuwa amemwelekeza Mose.

Malipo Kwa Ajili Ya Makosa

Bwana akamwambia Mose, 5:6 Law 6:2; 5:14–6:7“Waambie Waisraeli, ‘Wakati mwanaume au mwanamke akimkosea mwenzake kwa njia yoyote, na kwa hivyo akawa si mwaminifu kwa Bwana, mtu huyo ana hatia, 5:7 Law 5:5, 16; 6:5; Lk 19:8; Yos 7:19na ni lazima atubu dhambi aliyoifanya. Ni lazima atoe malipo kamili kwa ajili ya kosa lake, aongeze sehemu ya tano juu ya malipo hayo na kutoa yote kwa mtu aliyemkosea. 5:8 Law 5:15; 6:6-7Lakini ikiwa mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye malipo yanaweza kufanywa kwa ajili ya kosa, malipo yatakuwa mali ya Bwana, nayo ni lazima apewe kuhani, pamoja na kondoo dume ambaye anatumika kufanyia upatanisho kwa ajili yake. 5:9 Law 6:17; 7:6-14; Kut 29:28Matoleo yote matakatifu ya Waisraeli wanayoleta kwa kuhani yatakuwa yake. 5:10 Law 7:29-34; 10:13Kila kitu cha mtu kilichowekwa wakfu ni chake mwenyewe, lakini kile atoacho kwa kuhani kitakuwa cha kuhani.’ ”

Read More of Hesabu 5