Hesabu 33:1-56, Hesabu 34:1-29 NEN

Hesabu 33:1-56

Vituo Katika Safari Ya Waisraeli

33:1 Kut 17:1; 40:36; Hes 1:1; Kut 4:16; 6:26Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Mose na Aroni. 33:2 Kut 17:4Kwa agizo la Bwana, Mose aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao:

33:3 Hes 10:2; Mwa 47:11; Yos 5:10; Kut 14:8; 1:11; 12:37; 12:2; 13:4; Za 105:38; Isa 52:12; Kut 14:8Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote, 33:4 Kut 4:23; 2Nya 24:24; Yer 15:3; Eze 14:21; Kut 12:12; Isa 19:1; Sef 2:11; Ufu 12:8waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Bwana alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa Bwana alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.

33:5 Kut 12:37Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi.

33:6 Kut 13:20; Mwa 33:17; Yos 13:27; Za 60:6Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.

33:7 Kut 13:17, 18; 14:2, 9Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.

33:8 Kut 14:2; 14:22; 15:23Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara.

33:9 Kut 15:27Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi.

33:10 Kut 16:1Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu.

33:11 Kut 16:1; 17:1Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini.

Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka.

Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi.

33:14 Kut 15:22; 17:2Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa.

33:15 Kut 17:1; 19:1Wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai.

33:16 Hes 11:34Wakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava.

33:17 Hes 11; 35; Kum 9:22Wakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi.

33:18 Hes 12:16; Kum 1:1Wakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma.

Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi.

33:20 Yos 10:29; 12:15; 15:42; 21:13; 2Fal 8:22; 19:8; 23:31; 1Nya 6:57; 2Nya 21:10; Isa 37:8; Yer 52:1Wakaondoka Rimon-Peresi na kupiga kambi huko Libna.

Wakaondoka Libna na kupiga kambi huko Risa.

Wakaondoka Risa na kupiga kambi huko Kehelatha.

Wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye mlima Sheferi.

Wakaondoka kwenye mlima Sheferi na kupiga kambi huko Harada.

Wakaondoka Harada na kupiga kambi huko Makelothi.

Wakaondoka Makelothi na kupiga kambi huko Tahathi.

Wakaondoka Tahathi na kupiga kambi huko Tera.

Wakaondoka Tera na kupiga kambi huko Mithka.

Wakaondoka Mithka na kupiga kambi huko Hashmona.

33:30 Kum 10:6Wakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi.

33:31 Kum 10:6Wakaondoka Moserothi na kupiga kambi huko Bene-Yakani.

33:32 Mwa 36:27; Kum 10:6; 1Nya 1:42Wakaondoka Bene-Yakani na kupiga kambi huko Hor-Hagidgadi.

33:33 Kum 10:7Wakaondoka Hor-Hagidgadi na kupiga kambi huko Yotbatha.

Wakaondoka Yotbatha na kupiga kambi huko Abrona.

33:35 Kum 2:8; 1Fal 9:26; 22:48Wakaondoka Abrona na kupiga kambi huko Esion-Geberi.

33:36 Hes 13:21; 20:1; Kum 32:51; Yos 15:1Wakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini.

33:37 Hes 20:22; Mwa 36:16; Hes 20:16Wakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu. 33:38 Hes 27:13; Kut 16:35; Hes 20:25-28; Kum 10:6; 32:50Kwa amri ya Bwana, kuhani Aroni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri. Aroni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka 123.

33:40 Mwa 10:18; Hes 21:1; Mwa 12:9; Amu 1:16Mfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja.

Wakaondoka kwenye mlima Hori na kupiga kambi huko Salmona.

Wakaondoka Salmona, wakapiga kambi huko Punoni.

33:43 Hes 21:10Wakaondoka Punoni, wakapiga kambi huko Obothi.

33:44 Hes 21:11Wakaondoka Obothi, wakapiga kambi huko Iye-Abarimu, mipakani mwa Moabu.

33:45 Hes 32:34Wakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Dibon-Gadi.

33:46 Yer 48:22; Eze 6:14Wakaondoka Dibon-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu.

33:47 Hes 27:12; 32:3; Kum 32:49Wakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo.

33:48 Hes 27:12; 26:3; Mwa 13:10; Hes 22:1; Yos 12:9Wakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko. 33:49 Yos 12:3; 13:20; Eze 25:9; Hes 21:16Huko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi mpaka Abel-Shitimu.

33:50 Hes 33:48; 34:2Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani kuvukia Yeriko, Bwana akamwambia Mose, 33:51 Kum 7:1; 9:1; Yos 3:17“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani, 33:52 Law 26:1; Za 106:34-36; Kut 23:24; 34:12-17; Kum 7:2-5, 25, 26; Yos 11:12; 23:7; Amu 2:2wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kuyeyusha chuma, na kupabomoa mahali pao pa ibada. 33:53 Kum 11:31; 17:14; Yos 1:11; 21:43; Za 24:1; Ay 14:11; Dan 4:35Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki. 33:54 Law 16:8; Hes 36:2; 26:54; 35:8; Yos 18:10Mtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Chochote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu.

33:55 Yos 23:13; Amu 2:3; Za 106:36; Isa 55:13; Eze 2:6; 28:24; Mik 7:4; 2Kor 12:7; Kut 23:33; Mwa 17:8; Kum 1:7; Za 78:55; 105:11“ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi. 33:56 Hes 14:28Kisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’ ”

Read More of Hesabu 33

Hesabu 34:1-29

Mipaka Ya Kanaani

Bwana akamwambia Mose, 34:2 Hes 33:51; Mwa 17:8; Kum 1:7-8; Yos 23:4; Za 78:54-55; 105:11; Eze 47:15“Waamuru Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia nchi ya Kanaani, nchi ambayo itagawanywa kwenu kama urithi itakuwa na mipaka ifuatayo:

34:3 Hes 15:21; Yos 15:1-3; Mwa 14:3; Eze 47:13; Mwa 14:3; Yos 3:16“ ‘Upande wenu wa kusini utajumuisha sehemu ya Jangwa la Sini kufuata mpaka wa Edomu. Upande wa mashariki mpaka wenu wa kusini utaanzia mwisho wa Bahari ya Chumvi,34:3 Yaani Bahari Mfu. 34:4 Yos 15:3; Amu 1:36; Hes 32:8; Yos 15:4katiza kusini mwa Pito la Akrabimu, endelea mpaka Sini na kwenda kusini ya Kadesh-Barnea. Kisha mpaka huo utaenda hadi Hasar-Adari hadi Azmoni, 34:5 Mwa 15:18; 1Fal 8:65; Isa 27:12mahali ambapo utapinda, na kuunganika na Kijito cha Misri na kumalizikia kwenye Bahari ya Kati.34:5 Yaani Mediterania.

34:6 Yos 1:4; 9:1; 15:12; 23:4; Eze 47:10; 48:28; 47:9-20“ ‘Mpaka wenu wa magharibi utakuwa Bahari ya Kati. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa magharibi.

34:7 Eze 47:15-17; Hes 20:22“ ‘Kwa mpaka wenu wa kaskazini, wekeni alama kuanzia Bahari ya Kati hadi mlima Hori, 34:8 Hes 13:21; Yos 13:5; 2Sam 8:9; 2Fal 18:25; Isa 10:9; Yer 39:5; Eze 47:15-20na kutoka mlima Hori hadi Pito la Hamathi. Kisha mpaka utaenda hadi Sedadi, 34:9 Eze 47:17kuendelea hadi Zifroni, na kuishia Hasar-Enani. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa kaskazini.

34:10 Yos 15:5“ ‘Kwa mpaka wenu wa mashariki, wekeni alama kuanzia Hasar-Enani hadi Shefamu. 34:11 2Fal 23:33; 25:6; Yer 39:5; 52:9; Yos 15:32; 21:16; 1Nya 4:32; Kum 3:17; Yos 11:2; 13:27Mpaka utaelekea kusini kuanzia Shefamu hadi Ribla upande wa mashariki wa Aini, na kuendelea kwenye miteremko mashariki mwa Bahari ya Kinerethi.34:11 Yaani Bahari ya Galilaya. Kisha mpaka utashuka kuelekea Mto Yordani na kuishia katika Bahari ya Chumvi.

“ ‘Hii itakuwa nchi yenu, ikiwa na mipaka yake kila upande.’ ”

34:13 Law 16:8; Yos 18:10; Mik 2:5; Yos 13:6; 14:1-5; Isa 49:8Mose akawaamuru Waisraeli: “Gawanyeni nchi hii kwa kura kama urithi. Bwana ameagiza kwamba itolewe kwa yale makabila tisa na nusu, 34:14 Hes 32:19; Kum 33:21; Yos 14:3kwa sababu jamaa ya kabila la Reubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase wamekwishapokea urithi wao. Haya makabila mawili na nusu wamekwishapokea urithi wao upande wa mashariki wa Yordani ngʼambo ya Yeriko, kuelekea mawio ya jua.”

Bwana akamwambia Mose, 34:17 Hes 11:28; Kum 1:38; Kut 6:23-25“Haya ndiyo majina ya watu ambao watakusaidia kugawanya nchi kama urithi: Eleazari kuhani na Yoshua mwana wa Nuni. 34:18 Hes 1:4; Yos 14:1Tena uteue kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia kuigawanya nchi. 34:19 Hes 26:65; Mwa 29:35; Kum 33:7; Za 60:7; 108:8; Hes 13:6, 30; Kum 1:36Haya ndiyo majina yao:

“Kalebu mwana wa Yefune,

kutoka kabila la Yuda;

34:20 Mwa 29:33; 49:5; Eze 48:24Shemueli mwana wa Amihudi,

kutoka kabila la Simeoni;

34:21 Mwa 49:27; Amu 5:14; Za 68:27Elidadi mwana wa Kisloni,

kutoka kabila la Benyamini;

Buki mwana wa Yogli,

kiongozi kutoka kabila la Dani;

34:23 Hes 1:34; Mwa 48:8-22; Kum 33:13; Mwa 49:22; Za 80:1Hanieli mwana wa Efodi,

kiongozi kutoka kabila la Manase mwana wa Yosefu;

34:24 Hes 1:32Kemueli mwana wa Shiftani,

kiongozi kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yosefu;

34:25 Mwa 30:20Elisafani mwana wa Parnaki,

kiongozi kutoka kabila la Zabuloni;

Paltieli mwana wa Azani,

kiongozi kutoka kabila la Isakari;

34:27 Hes 1:40Ahihudi mwana wa Shelomi,

kiongozi kutoka kabila la Asheri;

Pedaheli mwana wa Amihudi,

kiongozi kutoka kabila la Naftali.”

34:29 Kum 32:8; Mdo 17:26Hawa ndio watu ambao Bwana aliamuru wagawanye urithi kwa Waisraeli katika nchi ya Kanaani.

Read More of Hesabu 34