Hesabu 31:25-54, Hesabu 32:1-42 NEN

Hesabu 31:25-54

Kugawanya Mateka

Bwana akamwambia Mose, 31:26 Hes 1:4; 1:19“Wewe na kuhani Eleazari pamoja na viongozi wa jamaa ya jumuiya mtahesabu watu wote na wanyama ambao walitekwa. 31:27 Yos 22:8; 1Sam 25:13; 30:24; Za 68:12Gawanyeni hizo nyara kati ya askari ambao walishiriki katika vita na kwa jumuiya. 31:28 Hes 18:21; 2Sam 8:11; 1Nya 8:11; 26:27; Isa 18:7; 23:18; Mt 22:21Kutoka fungu la wale waliokwenda kupigana vitani, tenga kama ushuru kwa ajili ya Bwana kitu kimoja kati ya kila mia tano, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo au mbuzi. Chukua ushuru huu kutoka fungu lao, umpe kuhani Eleazari kama sehemu ya Bwana. 31:30 Hes 3:7; 16:3Kutoka fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani ya Bwana.” Kwa hiyo Mose na kuhani Eleazari wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Mose.

Nyara zilizobaki kutoka mateka ambayo askari walichukua ni kondoo 675,000, ngʼombe 72,000, punda 61,000, na wanawake 32,000 ambao hawakumjua mume kwa kufanya tendo la ndoa.

Nusu ya fungu la wale waliokwenda kupigana vitani lilikuwa:

Kondoo 337,500 31:37 Law 25:23; Kum 10:14; Za 50:12; Mk 12:17; Lk 20:25; 1Kor 10:26ambayo ushuru kwa ajili ya Bwana ilikuwa kondoo 675;

ngʼombe 36,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa ngʼombe 72;

punda 30,500 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa punda 61;

Watu 16,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa watu 32.

31:41 Hes 5:9; 18:8, 19Mose alimpa kuhani Eleazari ushuru kama sehemu ya Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

Ile nusu iliyokuwa ya Waisraeli, ambayo Mose aliitenga kutoka kwa ile ya watu waliokwenda vitani, nusu iliyokuwa ya jumuiya, ilikuwa kondoo 337,500, ngʼombe 36,000, punda 30,500, na wanadamu 16,000. Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Mose alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kama Bwana alivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani ya Bwana.

Kisha maafisa waliokuwa juu ya vikosi vya jeshi, wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, walimwendea Mose 31:49 Hes 1:19; Yer 23:4; Kut 23:7; Law 26:7-9; Za 72:14; 116:15; 1Sam 30:19na kumwambia, “Watumishi wako wamehesabu askari walio chini ya amri yetu na hakuna hata mmoja aliyekosekana. 31:50 Kut 30:16; Law 17:11; Mt 20:28; Rum 3:25Kwa hiyo tumeleta kama sadaka kwa Bwana vyombo vya dhahabu kila mmoja wetu alivyopata, yaani vikuku, bangili, pete za muhuri, vipuli na mikufu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu mbele za Bwana.”

Mose na kuhani Eleazari wakapokea kutoka kwao dhahabu, yaani vyombo vyote vilivyonakshiwa. Dhahabu yote kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia ambavyo Mose na kuhani Eleazari walimletea Bwana kama zawadi ilikuwa shekeli 16,75031:52 Shekeli 16,750 ni sawa na kilo 200. 31:53 Mwa 34:29; Kum 20:14Kila askari alikuwa amejichukulia nyara zake binafsi. 31:54 Kut 27:21; 40:2; 28:12; Hes 16:40; Kut 30:16; Yos 4:7; Zek 6:14; Lk 22:19; Mdo 1:4Mose na kuhani Eleazari walipokea dhahabu kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, wakazileta katika Hema la Kukutania kama ukumbusho kwa Waisraeli mbele za Bwana.

Read More of Hesabu 31

Hesabu 32:1-42

Makabila Ngʼambo Ya Yordani

(Kumbukumbu 3:12-22)

32:1 Amu 5:16; Hes 21:32; Mwa 31:21; Kut 12:38Kabila la Wareubeni na Wagadi, waliokuwa na makundi makubwa ya ngʼombe, kondoo na mbuzi, waliona kuwa nchi ya Yazeri na nchi ya Gileadi ni nzuri kwa mifugo. 32:2 Law 4:22; Hes 27:2; 2Sam 24:5; Isa 16:8-9Hivyo walimjia Mose, na kuhani Eleazari na viongozi wa jumuiya, na kuwaambia, 32:3 Yos 16:2; 18:13; Hes 21:30; Yos 13:27; Hes 21:25; Isa 15:4; 16:9; Yer 48:34; Yos 13:19; Isa 16:8; Yer 48:32; Hes 33:47“Atarothi, Diboni, Yazeri, Nimra, Heshboni, Eleale, Sebamu, Nebo na Beoni, 32:4 Hes 21:34; Kut 12:38nchi ambayo Bwana ameishinda mbele ya wana wa Israeli, inafaa kwa mifugo, nao watumishi wako wana mifugo. 32:5 Hes 13:29Kama tumepata kibali mbele ya macho yako, nchi hii na ipewe watumishi wako kama milki yetu. Usitufanye tuvuke Yordani.”

Mose akawaambia Wagadi na Wareubeni, “Je, watu wa nchi yenu watakwenda vitani wakati ninyi mmeketi hapa? 32:7 Hes 13:27–14:4Kwa nini mmewakatisha Waisraeli tamaa wasivuke katika nchi ambayo Bwana amewapa? 32:8 Hes 13:3; Kum 1:19-25; 1:22Hivi ndivyo baba zenu walivyofanya wakati nilipowatuma kutoka Kadesh-Barnea kuipeleleza nchi. 32:9 Hes 13:23; Kum 1:24Baada ya kufika kwenye Bonde la Eshkoli na kuitazama nchi, waliwakatisha tamaa Waisraeli wasiingie katika nchi ambayo Bwana alikuwa amewapa. 32:10 Hes 11:1; 14:20-23; 14:11; Za 95:11; Eze 20:15; Ebr 3:8-19Siku ile hasira ya Bwana iliwaka naye akaapa kiapo hiki: 32:11 Kut 30:14; Hes 1:1; 14:23; Kum 1:35; Hes 14:24; 14:28‘Kwa kuwa hawakunifuata kwa moyo wote, hakuna mtu yeyote mwenye miaka ishirini au zaidi ambaye alikuja kutoka Misri atakayeona nchi niliyoahidi kwa kiapo kwa Abrahamu, Isaki na Yakobo; 32:12 Hes 14:24; Za 63:8; Kum 1:35; Yos 14:8, 9; Ay 4:7; Za 37:29; Mit 11:31hakuna hata mmoja isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni, kwa sababu walimfuata Bwana kwa moyo wote.’ 32:13 Kut 4:14; Hes 14:28-35; 26:64, 65Hasira ya Bwana iliwaka dhidi ya Waisraeli na akawafanya watangetange katika jangwa kwa miaka arobaini, mpaka kizazi chote cha wale waliofanya maovu mbele yake kimeangamia.

32:14 Kum 1:34; Za 78:59“Nanyi mko hapa, uzao wa wenye dhambi, mkisimamia mahali pa baba zenu na mkimfanya Bwana kuwakasirikia Waisraeli hata zaidi. 32:15 Kum 30:17-18; 2Nya 7:20; Yos 22:16, 18; 2Nya 15:2Kama mkigeuka na mkiacha kumfuata, atawaacha tena watu hawa wote jangwani, na mtakuwa sababu ya maangamizi yao.”

32:16 1Sam 24:3; Za 50:9; 78:70; Kut 12:38; Kum 3:19Ndipo wakamjia Mose na kumwambia, “Tungalitaka kujenga mazizi hapa kwa ajili ya mifugo yetu na miji kwa ajili ya wanawake wetu na watoto. 32:17 Kum 3:18; Yos 4:12, 13; Hes 22:4; Kum 3:20Lakini sisi tuko tayari kuchukua silaha zetu na kutangulia mbele ya Waisraeli mpaka tutakapowaleta mahali pao. Wakati huo wanawake wetu na watoto wataishi katika miji yenye ngome, kwa ajili ya ulinzi dhidi ya wenyeji wa nchi. 32:18 Yos 22:1-4Hatutarudi nyumbani mwetu mpaka kila Mwisraeli apokee urithi wake. 32:19 Hes 21:33; Yos 12:1; 22:7Hatutapokea urithi wowote pamoja nao ngʼambo ya Yordani, kwa sababu urithi wetu umekuja kwetu upande wa mashariki ya Yordani.”

32:20 Kum 3:18; Yos 4:12-13Kisha Mose akawaambia, “Kama mtafanya jambo hili, kama mtajivika silaha mbele za Bwana kwa ajili ya vita, na kama ninyi nyote mtakwenda mmejivika silaha ngʼambo ya Yordani mbele za Bwana mpaka awe amewafukuza adui zake mbele zake, 32:22 Yos 22:4; Law 14:34; Kum 3:18-20hadi wakati nchi itakapokuwa imeshindwa mbele za Bwana, ndipo mtaweza kurudi na kuwa huru kutoka masharti yenu kwa Bwana na Israeli. Nayo nchi hii itakuwa milki yenu mbele za Bwana.

32:23 Mwa 4:7; Isa 3:9; Mwa 44:16; Za 140:11; Mit 13:21; Isa 59:12; Rum 2:9“Lakini mkishindwa kufanya hili, mtakuwa mnatenda dhambi dhidi ya Bwana; nanyi kuweni na hakika kuwa dhambi yenu itawapata. 32:24 Hes 30:2; 32:16, 34Jengeni miji kwa ajili ya wanawake na watoto wenu, na mazizi kwa ajili ya mbuzi na kondoo zenu, lakini fanyeni yale mliyoahidi.”

32:25 Yos 1:16; 22:2Wagadi na Wareubeni wakamwambia Mose, “Sisi watumishi wako tutafanya kama bwana wetu anavyotuagiza. 32:26 Yos 1:14; 12:2; 22:9; 2Sam 2:9; 1Nya 5:9Watoto na wake zetu, makundi ya mbuzi na kondoo, na makundi ya ngʼombe zetu, watabaki hapa katika miji ya Gileadi. 32:27 Yos 4:12Lakini watumishi wenu, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, watavuka ngʼambo kupigana mbele za Bwana, sawa kama bwana wetu anavyosema.”

32:28 Kum 3:18; Yos 1:13; Hes 11:28; 1:16Kisha Mose akatoa amri kuhusu wao kwa kuhani Eleazari, na Yoshua mwana wa Nuni na viongozi wa jamaa za makabila ya Waisraeli. 32:29 Hes 22:4Mose akawaambia, “Ikiwa Wagadi na Wareubeni, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, atavuka Yordani pamoja nanyi mbele za Bwana, basi wakati mtakapoishinda nchi iliyoko mbele yenu, wapeni nchi ya Gileadi kama milki yao. Lakini kama hawatavuka pamoja nanyi wakiwa wamevaa silaha za vita, lazima wakubali kupokea milki yao pamoja nanyi katika nchi ya Kanaani.”

Wagadi na Wareubeni wakajibu, “Watumishi wako watafanya lile Bwana alilosema. 32:32 Yos 12:6Tutavuka mbele za Bwana kuingia Kanaani tukiwa tumevaa silaha za vita, lakini mali tutakayoirithi itakuwa ngʼambo hii ya Yordani.”

32:33 Yos 13:24-28; 1Sam 13:7; Yos 1:12; Hes 21:21; Kum 2:26; Yos 12:5; Hes 21:24; 34:24; Kum 2:36; Yos 12:6Kisha Mose akawapa Wagadi, Wareubeni, na nusu ya kabila la Manase mwana wa Yosefu ufalme wa Sihoni mfalme wa Waamori, na ufalme wa Ogu mfalme wa Bashani, nchi yote pamoja na miji yake, na nchi inayowazunguka.

32:34 Kum 2:36; 3:13; 4:48; Yos 12:2; 13:9; Amu 11:26; 1Sam 30:28; 1Nya 5:8; Yer 48:19; Hes 33:45Wagadi wakajenga Diboni, Atarothi, Aroeri, 32:35 Amu 8:11Atroth-Shofani, Yazeri, Yogbeha, Beth-Nimra na Beth-Harani kama miji iliyozungushiwa ngome, tena wakajenga mazizi kwa ajili ya makundi yao ya mbuzi na kondoo. 32:37 Hes 21:25; Yos 13; 19; 1Nya 6:76; Yer 48:1; Eze 25:9Nao Wareubeni wakajenga upya miji ya Heshboni, Eleale na Kiriathaimu, 32:38 Isa 15:2; 46:1; Yer 48:1, 22; Hes 32:3; Kut 23:13pia Nebo na Baal-Meoni (majina ya hiyo miji yalibadilishwa) na Sibma. Miji waliyoijenga upya waliipa majina.

32:39 Mwa 50:23; Hes 26:29; Kum 2:36; Mwa 10:16; Yos 17:1Wazao wa Makiri mwana wa Manase walikwenda Gileadi, wakaiteka nchi na kuwafukuza Waamori waliokuwa huko. 32:40 Mwa 50:23; Kum 3:15Kwa hiyo Mose akawapa Wamakiri, wazao wa Manase, nchi ya Gileadi, nao wakakaa huko. 32:41 Kum 3:14; Yos 13:30; Amu 10:4; 1Nya 2:23Yairi, mzao wa Manase, akateka makao yao, akayaita Hawoth-Yairi. 32:42 1Nya 2:23; Amu 8:11; 1Sam 15:12; 2Sam 18:18Naye Noba akateka Kenathi na makao yaliyoizunguka, akayaita Noba kwa jina lake.

Read More of Hesabu 32