Hesabu 27:12-23, Hesabu 28:1-31, Hesabu 29:1-11 NEN

Hesabu 27:12-23

Yoshua Kuchukua Nafasi Ya Mose

(Kumbukumbu 31:1-8)

27:12 Hes 23:14; 33:47; Yer 22:20; Kum 3:23; 32:48-52; Law 14:34Kisha Bwana akamwambia Mose, “Panda juu ya mlima huu katika kilele cha Abarimu uione nchi ambayo nimewapa Waisraeli. 27:13 Hes 20:12; 31:2; Kum 4:22; 31:14; 32:50; 1Fal 2:1; Hes 20:28Baada ya kuiona, wewe pia utakusanywa pamoja na watu wako kama ndugu yako Aroni alivyokusanywa, 27:14 Hes 20:1; 20:12; Kut 17:7; Kum 1:37; 32:51; Za 106:32kwa kuwa jumuiya ilipoasi amri yangu kwenye maji katika Jangwa la Sini, wakati jumuiya ilipogombana nami, nyote wawili mliacha kuitii amri yangu ya kuniheshimu kama mtakatifu mbele ya macho yao.” (Haya yalikuwa maji ya Meriba huko Kadeshi, katika Jangwa la Sini.)

Mose akamwambia Bwana, 27:16 Hes 16:22; Ay 21:10; Ebr 12:9; Zek 12:1Bwana, Mungu wa roho zote za wanadamu, na amteue mtu juu ya jumuiya hii 27:17 1Fal 22:17; 2Nya 18:16; Eze 34:5; Zek 10:2; Mt 9:36; Kum 31:2; 1Sam 8:20; 18:13; 2Nya 1:10; 18:16; Amu 3:10ili atoke na kuingia mbele yao, atakayewaongoza katika kutoka kwao na kuingia kwao, ili watu wa Bwana wasiwe kama kondoo wasio na mchungaji.”

27:18 Mwa 41:38; Hes 11:25; Kum 34:9; Mdo 6:6; Amu 3:10Kwa hiyo Bwana akamwambia Mose, “Mchukue Yoshua mwana wa Nuni, mtu ambaye Roho yuko ndani yake, uweke mkono juu yake. 27:19 Kum 3:28; 31:14; 31:7Msimamishe mbele ya kuhani Eleazari pamoja na kusanyiko lote, umpe maagizo mbele yao. 27:20 Ay 1:16; Hes 11:17; 1Sam 10:6; 2Fal 2:15Mpe sehemu ya mamlaka yako ili jumuiya yote ya Waisraeli ipate kumtii. 27:21 Mwa 25:22; Ay 9:14; Za 106:13; Isa 8:19; 1:13; Mal 2:7; 3:1; Kut 28:30; Yos 9:14; Amu 1:1; 20:18; Law 8:8; Kum 33:8; 1Sam 28:6Atasimama mbele ya kuhani Eleazari, ambaye atapokea maamuzi kwa ajili yake, kwa kuuliza mbele za Bwana kwa ile Urimu.27:21 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha. Kwa amri yake, yeye na jumuiya yote ya Waisraeli watatoka, na kwa amri yake, wataingia.”

Mose akafanya kama Bwana alivyomwagiza. Akamtwaa Yoshua na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na kusanyiko lote. 27:23 Kum 3:28; Isa 55:4Kisha akaweka mikono yake juu ya kichwa cha Yoshua na kumpa maagizo, kama vile Bwana alivyoelekeza kupitia kwa Mose.

Read More of Hesabu 27

Hesabu 28:1-31

Sadaka Za Kila Siku

(Kutoka 29:38-46)

Bwana akamwambia Mose, 28:2 Law 23:1-44; 3:11; 1:9; Mal 1:7-12“Wape Waisraeli agizo hili na uwaambie: ‘Hakikisheni kwamba mnaniletea mimi kwa wakati uliowekwa chakula kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, kama harufu nzuri ya kupendeza.’ 28:3 Kut 12:3; 29:38; Amo 4:4; Kut 29:38Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtolea Bwana: wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku. 28:4 Kut 29:39; 12:6Andaa mwana-kondoo mmoja asubuhi na mwingine jioni, 28:5 Hes 29:6; Law 6:20; 2:1; Kut 16:36; 29:38-42; Hes 15:4kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa28:5 Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja. ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini28:5 Robo ya hini ni sawa na lita moja. ya mafuta ya zeituni. 28:6 Law 1:3; Kut 19:3; Law 1:9Hii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. 28:7 Hes 6:15; Law 10:9; 3:7; Hes 3:28; Kut 29:42; 30:9; Law 23:13; Hes 15:5-10; Isa 57:1Sadaka ya kinywaji itakayotolewa pamoja na kila mwana-kondoo ni robo ya hini ya kinywaji kilichochachuka. Mimina sadaka ya kinywaji kwa Bwana mahali patakatifu. 28:8 Kut 29:39; Law 23:7; 1:9Andaa yule mwana-kondoo wa pili jioni, pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka ya kinywaji kama ulivyofanya kwa ile sadaka nyingine ya asubuhi. Hii ni sadaka iliyotolewa kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

Sadaka Za Sabato

28:9 Kut 20:10; Mt 12:5; Law 23:13; Eze 46:4; 40:4“ ‘Siku ya Sabato, utatoa sadaka ya wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari pamoja na sadaka yake ya kinywaji na sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu mbili za kumi za efa28:9 Sehemu mbili za kumi za efa ni sawa na kilo 2. za unga laini uliochanganywa na mafuta. 28:10 Law 23:38; 1Sam 20:5; 1Nya 23:31; Neh 10:33; Isa 1:13-14; Eze 45:17; Hos 2:11; Kol 2:16Hii ni sadaka ya kuteketezwa itakayotolewa kwa ajili ya kila Sabato, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya kinywaji.

Sadaka Za Kila Mwezi

28:11 Hes 10:10; 7:15; Law 5:15; 1:3“ ‘Siku ya kwanza ya kila mwezi, mtamletea Bwana sadaka ya kuteketezwa ya fahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasiokuwa na dosari. 28:12 Hes 15:6; 29:3; 15:9Pamoja na kila fahali, kutakuwa na sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa,28:12 Sehemu tatu za kumi za efa ni sawa na kilo 3. uliochanganywa na mafuta, pamoja na kondoo dume mmoja, sadaka ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta; 28:13 Law 6:14; Hes 15:3; Law 1:9pamoja na kila mwana-kondoo, sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta. Hii ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri, sadaka ya kuteketezwa iliyotolewa kwa moto kwa Bwana. 28:14 Hes 15:11; 2Nya 2:4; Eze 3:5Pamoja na kila fahali kutakuwa na sadaka ya kinywaji nusu ya hini28:14 Nusu ya hini ni sawa na lita 2. ya divai; pamoja na kila kondoo dume, theluthi moja ya hini,28:14 Theluthi moja ya hini ni sawa na lita 1.2. na pamoja na kila mwana-kondoo robo hini. Hii ni sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi itakayotolewa kila mwandamo wa mwezi kwa mwaka. 28:15 Hes 4:3; 29:16Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwa Bwana kama sadaka ya dhambi.

Pasaka

(Walawi 23:5-14)

28:16 Kut 12:11; 2Nya 30:13; 35:1; Kut 12:6; Law 23:5; Lk 22:7“ ‘Katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, itafanyika Pasaka ya Bwana. 28:17 Kut 12:19; 12:15Katika siku ya kumi na tano ya mwezi huo itakuwa sikukuu; kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu. 28:18 Kut 12:16; Law 23:7Katika siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu, msifanye kazi za kawaida. 28:19 Law 1:9; 22:20; Hes 29:8; Kum 15:21Leteni mbele za Bwana sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo dume saba wenye umri wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 28:20 Law 14:10Pamoja na kila fahali, andaa sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa; pia pamoja na kila mmoja wa wale wana-kondoo saba, andaa sehemu ya kumi ya efa. 28:22 Law 4:2; 8:3; Hes 15:28; Law 16:18; Rum 8:3; Gal 4:4; Ebr 9:12; 10:1Pia mtoe beberu mmoja kama sadaka ya dhambi ambaye atafanya upatanisho kwa ajili yenu. Andaa hizi licha ya zile sadaka za kawaida za kuteketezwa za kila asubuhi. 28:24 Law 1:9; 2Kor 2:15; Efe 5:2Kwa njia hii andaa chakula cha sadaka ya kuteketezwa kila siku, kwa siku saba kama harufu nzuri impendezayo Bwana. Hii itaandaliwa licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa ya kila siku pamoja na sadaka yake ya kinywaji. 28:25 Kut 12:16; 13:6; Law 23:8Siku ya saba mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida.

Sikukuu Ya Majuma

(Walawi 23:15-22)

28:26 Kut 34:2; 23:16; Law 23:10; Kum 16:10; Mit 3:9; Mdo 2:1“ ‘Siku ya malimbuko, mnapomletea Bwana sadaka ya nafaka mpya wakati wa Sikukuu ya Majuma, mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida. 28:27 Law 23:18-19Mlete sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na pia wana-kondoo saba wenye umri wa mwaka mmoja, kama harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. Pamoja na kila fahali itatolewa sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini; na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba. Ongeza beberu mmoja kwa kufanya upatanisho kwa ajili yenu. Andaa hizi sadaka pamoja na sadaka zake za vinywaji, kuwa nyongeza ya sadaka za kawaida za kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka. Hakikisha kuwa wanyama hao hawana dosari.

Read More of Hesabu 28

Hesabu 29:1-11

Sikukuu Ya Tarumbeta

(Walawi 23:23-25)

29:1 Hes 28:18“ ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu na msifanye kazi ya kawaida. Ni siku kwa ajili yenu ya kupiga tarumbeta. 29:2 Hes 28:2; Law 1:9; Hes 28:11; Law 1:3; Hes 28:3Mtatayarisha sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri impendezayo Bwana ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 29:3 Hes 28:12Pamoja na fahali, andaeni sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume, andaa unga sehemu ya kumi mbili za efa; 29:4 Hes 28:13na pamoja na wana-kondoo saba kila mmoja aandaliwe na sehemu ya kumi ya efa ya unga. 29:5 Hes 28:15Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi kufanya upatanisho kwa ajili yenu. 29:6 Hes 28:11; 28:3; 28:5; 28:7; Law 1:9; Hes 28:2; Dan 12:11; Law 6:9; Hes 15:11, 12Hivi ni nyongeza ya sadaka za kuteketezwa kila mwezi na kila siku pamoja na sadaka zake za nafaka na sadaka za vinywaji kama ilivyoainishwa. Ni sadaka zinazotolewa kwa Bwana kwa moto, harufu inayopendeza.

Siku Ya Upatanisho

(Walawi 23:26-32)

29:7 Mdo 27:9; Kut 31:15; Law 16:29; Ezr 8:21; Za 35:13; Isa 58:5; Lk 13:3-4; 1Kor 9:27; Yak 4:9“ ‘Kwenye siku ya kumi ya mwezi huu wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu. Mtajikana wenyewe na msifanye kazi. 29:8 Law 22:20; Hes 28:19; 29:8; Kum 15:21; 17:1Toeni sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza Bwana. 29:9 Hes 28:12Pamoja na fahali, andaeni sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, sehemu ya kumi mbili za efa za unga laini; 29:10 Hes 28:13na kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba andaa sehemu ya kumi ya unga laini kwa kila mmoja. 29:11 Hes 28:12; Law 16:3Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho, na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, na sadaka zake za vinywaji.

Read More of Hesabu 29