Hesabu 23:27-30, Hesabu 24:1-25, Hesabu 25:1-18 NEN

Hesabu 23:27-30

Ujumbe Wa Tatu Wa Balaamu

Basi Balaki akamwambia Balaamu, “Njoo, nikupeleke mahali pengine. Huenda itampendeza Mungu kukuruhusu unilaanie hao watu kutoka mahali hapo.” Balaki akamchukua Balaamu juu ya Mlima Peori, unaotazamana na nyika.

Balaamu akasema, “Nijengee hapa madhabahu saba, uandae mafahali saba na kondoo dume saba kwa ajili yangu.” Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema, kisha akatoa sadaka ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.

Read More of Hesabu 23

Hesabu 24:1-25

24:1 Hes 23:20, 23, 28Basi Balaamu alipoona imempendeza Bwana kubariki Israeli, hakuendelea tena kutafuta uchawi kama nyakati nyingine, bali aligeuza uso wake kuelekea nyikani. 24:2 Hes 11:25; 1Sam 19:20; 2Nya 15:1; Mt 7:21-22; 1Kor 12:8-10Balaamu alipotazama nje na kuona Israeli amepiga kambi kabila kwa kabila, Roho wa Mungu akawa juu yake, 24:3 Hes 23:7naye akatoa ujumbe wake:

“Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori,

ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri;

24:4 Hes 22:9; Mwa 15:1; 1Sam 19:24; Eze 1:28; Dan 8:18; 10:15; 2Kor 12:2ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,

ambaye huona maono kutoka kwa Mwenyezi,24:4 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania (pia 24:16).

ambaye huanguka kifudifudi, na ambaye macho yake yamefunguka:

24:5 Yer 4:20; 30:18; Mal 2:12“Tazama jinsi yalivyo mazuri mahema yako, ee Yakobo,

maskani yako, ee Israeli!

24:6 Mwa 2:10; Za 1:3; 45:8; 104:16; Wim 4:14; Ay 29:19; Eze 31:5“Kama mabonde, yanaenea,

kama bustani kando ya mto,

kama miti ya udi iliyopandwa na Bwana,

kama mierezi kando ya maji.

24:7 Kut 17:8-16; Kum 28:1; 2Sam 5:12; 1Nya 14:2; Za 89:27; 145:11-13Maji yatatiririka kutoka ndoo zake;

mbegu yake itakuwa na maji tele.

“Mfalme wake atakuwa mkuu kuliko Mfalme Agagi;

ufalme wake utatukuka.

24:8 Kut 15:6; Yer 50:17; 2Sam 18:14; Za 45:5“Mungu alimleta kutoka Misri;

yeye ana nguvu kama nyati.

Anayararua mataifa yaliyo adui zake,

na kuvunja mifupa yao vipande vipande;

huwachoma kwa mishale yake.

24:9 Kut 23:23; Hes 23:24; Mwa 12:2, 3; 27:29; Za 122:6Hujikunyata na kuvizia kama simba,

kama simba jike; nani anayethubutu kumwamsha?

“Abarikiwe kila akubarikiye,

na alaaniwe kila akulaaniye!”

24:10 Kut 4:14; Ay 27:23; 34:37; Mao 2:15; Eze 21:14; 22:13; 25:6; Hes 22:6; 23:7-11, 18-24; Kum 23:5Ndipo hasira ya Balaki ikawaka dhidi ya Balaamu. Akapiga mikono yake pamoja, akamwambia Balaamu, “Nilikuita uje kuwalaani adui zangu, lakini umewabariki mara hizi tatu. 24:11 Hes 22:17Sasa ondoka upesi uende nyumbani! Mimi nilisema nitakuzawadia vizuri sana, lakini Bwana amekuzuia usizawadiwe.”

24:12 Hes 22:18Balaamu akamwambia Balaki, “Je, hukumbuki jinsi nilivyowaambia wajumbe uliowatuma kwangu? Niliwaambia hivi, 24:13 Hes 22:18, 20‘Hata ikiwa Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, nisingeweza kufanya kitu chochote kwa matakwa yangu, kikiwa kizuri au kibaya, kwenda kinyume na agizo la Bwana, nami imenipasa kusema tu kile Bwana atakachosema’? 24:14 Mwa 49:1; Hes 31:8; Mik 6:5Sasa ninarudi kwa watu wangu. Lakini njoo, nikuonye kuhusu kile watu hawa watakachowatenda watu wako siku zijazo.”

Ujumbe Wa Nne Wa Balaamu

Kisha Balaamu akatoa ujumbe wake:

“Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori,

ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri;

24:16 Hes 22:9; Mwa 14:18; Isa 14:14ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,

ambaye ana maarifa kutoka kwa Aliye Juu Sana,

huona maono kutoka Mwenyezi,

ambaye huanguka kifudifudi

na ambaye macho yake yamefunguka:

24:17 Ufu 1:7; Mt 2:2; Mwa 49:10; 19:37; Hes 21:29; Kum 23:6; Isa 15:1–16:14; Yer 48:45“Namwona yeye, lakini si sasa;

namtazama yeye, lakini si karibu.

Nyota itatoka kwa Yakobo,

fimbo ya ufalme itainuka kutoka kwa Israeli.

Atawaponda Wamoabu vipaji vya nyuso

na mafuvu yote ya wana wa Shethi.

24:18 2Sam 8:12; 1Nya 18:11; Za 60:8; Isa 11:14; Amo 9:12; Mwa 9:25; 14:6; Kum 1:44; Yos 12:7; 15:10; Amu 5:4; Oba 1:2Edomu itamilikiwa,

Seiri, adui wake, itamilikiwa,

lakini Israeli atakuwa na nguvu.

24:19 Mwa 49:10; Mik 5:2Mtawala atakuja kutoka kwa Yakobo

na kuangamiza walionusurika katika mji.”

Ujumbe Wa Mwisho Wa Balaamu

24:20 Mwa 14:7; Kut 17:14; Kum 25:19; 1Sam 15:20; 30:17-20; 2Sam 8:12; 1Nya 18:11Kisha Balaamu akawaona watu wa Amaleki, na kutoa ujumbe wake:

“Amaleki ilikuwa ya kwanza miongoni mwa mataifa,

lakini mwisho wake itaangamizwa milele.”

24:21 Mwa 15:19; Za 37:27; Mit 1:33; Isa 32:18; Eze 34:27Kisha akawaona Wakeni, akatoa ujumbe wake:

“Makao yenu ni salama,

kiota chenu kiko kwenye mwamba.

24:22 Mwa 10:22Hata hivyo ninyi Wakeni mtaangamizwa

Ashuru atakapowachukua mateka.”

Ndipo akatoa ujumbe wake:

“Lo, ni nani atakayeweza kuishi wakati Mungu atakapofanya hili?

24:24 Mwa 10:4, 21; Hes 22:5; Isa 23:1; Dan 11:30; Law 26:28; Kum 28:36; Mt 23:37Meli zitakuja kutoka pwani za Kitimu,

zitaitiisha Ashuru na Eberi,

lakini nao pia wataangamizwa.”

Kisha Balaamu akainuka na kurudi nyumbani kwake, naye Balaki akashika njia yake.

Read More of Hesabu 24

Hesabu 25:1-18

Moabu Yashawishi Israeli

25:1 Hes 21:16; Yos 2:1; Isa 66:11; Yoe 3:18; Mik 6:5; Yer 5:7; 7:9; 9:2; 1Kor 10:8; Ufu 2:14; Mwa 19:37; Hes 31:16Israeli alipokuwa akikaa Shitimu, wanaume wa Israeli walianza kuzini na wanawake wa Kimoabu, 25:2 Kut 32:6; 20:5; Kum 32:38; 1Kor 10:20; Yos 22:17; Hos 9:10; Kut 34:15; 20:5ambao waliwaalika kushiriki katika kutoa kafara kwa miungu yao. Watu wakala na kusujudu mbele ya miungu hii. 25:3 Kum 4:19; Amu 2:19; 1Fal 9:9; Yer 1:16; 44:3; Hes 23:26Kwa hiyo Israeli akaungana katika kumwabudu Baali wa Peori. Hasira ya Bwana ikawaka dhidi yao.

25:4 Hes 7:2; 13:3; 2Sam 21:6; Kum 4:3; Kut 32:12; Kum 13:17; Yos 7:26; 2Fal 23:26; 2Nya 28:11; 29:10; 30:8; Eze 10:14; Yer 44:3Bwana akamwambia Mose, “Uwachukue viongozi wote wa watu hawa, uwaue na uwaweke hadharani mchana peupe mbele za Bwana, ili hasira kali ya Bwana iweze kuondoka kwa Israeli.”

25:5 Kut 32:27; Hos 9:10Kwa hiyo Mose akawaambia waamuzi wa Israeli, “Kila mmoja wenu lazima awaue wale wanaume wenu, walioshiriki katika kumwabudu Baali wa Peori.”

25:6 Mwa 25:2; Hes 14:1; Amu 2:4; Rut 1:9; 1Sam 11:4; 2Sam 15:30; Ezr 10:1; Za 126:6; Yer 41:6Ndipo mwanaume wa Kiisraeli akamleta mwanamke wa Kimidiani katika jamaa yake palepale mbele ya Mose na mkutano wote wa Israeli walipokuwa wakilia kwenye lango la Hema la Kukutania. 25:7 Kut 6:25; Yos 22:13; Amu 20:28; 5:8; 1Sam 13:19; 1Fal 18:28; Za 35:3; 46:9; Yoe 3:10; Mik 4:3Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, alipoona jambo hili, akaondoka kwenye kusanyiko, akachukua mkuki mkononi mwake, 25:8 Za 106:30akamfuata yule Mwisraeli ndani ya hema. Akawachoma mkuki wote wawili kwa pamoja, ukapenya kwenye mwili wa yule Mwisraeli na mwili wa yule mwanamke. Ndipo tauni iliyokuwepo dhidi ya Waisraeli ikakoma. 25:9 Hes 14:37; 1Kor 10:8; Hes 31:16Lakini wale waliokufa kwa hiyo tauni walikuwa watu 24,000.

Bwana akamwambia Mose, 25:11 Za 106:30; Kut 20:5; Kum 32:16; Za 78:58; Nah 1:3; Sef 1:13“Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, amegeuza hasira yangu mbali na Waisraeli, kwa sababu alikuwa na wivu kama nilio nao kwa heshima yangu miongoni mwao, hata kwamba kwa wivu wangu sikuwaangamiza. 25:12 Isa 11:9; 54:10; Eze 34:25; 37:26; Mal 2:4Kwa hiyo mwambie Finehasi ninafanya Agano langu la amani naye. 25:13 Kut 29:9; 1Fal 19:10; 2Fal 10:16; Kut 29:36; Rum 3:26; Za 106:31; Yer 33:18Yeye pamoja na wazao wake watakuwa na Agano la ukuhani milele, kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya heshima ya Mungu wake, na akafanya upatanisho kwa Waisraeli.”

25:14 Hes 1:6; 25:6Jina la Mwisraeli ambaye aliuawa pamoja na mwanamke wa Kimidiani ni Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa ya Simeoni. 25:15 Hes 31:8; Yos 13:21; Hab 3:7Jina la mwanamke wa Kimidiani aliyeuawa ni Kozbi binti wa Suri, aliyekuwa mkuu wa kabila la jamaa ya Wamidiani.

25:16 Hes 31:7Bwana akamwambia Mose, 25:17 Hes 31:1-3; Kut 23:22; Amu 2:16-18; Neh 9:27; Za 8:2; 21:8; 74:23; Kum 21:1; 1Sam 17:9; 2Fal 9:27; 10:25“Watendeeni Wamidiani kama adui na mwaue, 25:18 Hes 23:28kwa sababu wao waliwatendea kama adui wakati waliwadanganya katika tukio la Peori na dada yao Kozbi, binti wa kiongozi wa Kimidiani, mwanamke ambaye aliuawa wakati tauni ilikuja kama matokeo ya tukio la Peori.”

Read More of Hesabu 25