Hesabu 19:1-22, Hesabu 20:1-29, Hesabu 21:1-3 NEN

Hesabu 19:1-22

Maji Ya Utakaso

Bwana akamwambia Mose na Aroni: 19:2 Mwa 15:9; Ebr 9:13; Law 22:19-25; Kum 21:3; 1Sam 6:7“Hivi ndivyo sheria ambayo Bwana ameagiza itakavyo: Waambie Waisraeli wakuletee mtamba mwekundu asiye na dosari wala waa, na ambaye hajapata kufungwa nira. 19:3 Hes 3:4; Kut 29:14Mpeni kuhani Eleazari huyo mtamba; naye atatolewa nje ya kambi na kuchinjwa mbele yake huyo kuhani. 19:4 Law 4:17Kisha kuhani Eleazari atachukua baadhi ya damu yake kwenye kidole chake na kuinyunyiza mara saba kuelekea upande wa mbele ya Hema la Kukutania. 19:5 Kut 29:14Wakati angali akitazama, mtamba huyo atateketezwa: ngozi yake, nyama yake, damu na sehemu zake za ndani. 19:6 Za 51:7; Law 14:4Kuhani atachukua kuni za mti wa mwerezi, hisopo na sufu nyekundu, na kuvitupa kwenye huyo mtamba anayeungua. 19:7 Law 11:25; 14:8Baada ya hayo, kuhani lazima afue nguo zake, na aoge mwili wake kwa maji. Kisha anaweza kurudi kambini, lakini atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada mpaka jioni. Mtu amchomaye huyo mtamba lazima naye pia afue nguo zake na kuoga kwa maji, naye pia atakuwa najisi mpaka jioni.

19:9 Ebr 9:13; Kut 29:31; Law 4:12; Hes 8:1; Mwa 35:2“Mtu ambaye ni safi atakusanya majivu ya mtamba huyo na kuyaweka mahali ambapo ni safi nje ya kambi kwa taratibu za kiibada. Yatahifadhiwa na jumuiya ya Kiisraeli kwa matumizi katika maji ya utakaso; ni kwa ajili ya kutakasa kutoka dhambini. 19:10 Law 15:10; 14:46; 3:17; 22:18Mtu akusanyaye majivu ya huyo mtamba ni lazima pia afue nguo zake, kadhalika naye pia atakuwa najisi hadi jioni. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa Waisraeli na kwa wageni wanaoishi miongoni mwao.

19:11 Law 21:1; 8:33; Hes 31:19“Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote atakuwa najisi kwa siku saba. 19:12 Hes 31:19; 2Nya 26:21Ni lazima ajitakase mwenyewe kwa maji katika siku ya tatu na siku ya saba, ndipo atakuwa safi. Lakini kama hatajitakasa mwenyewe katika siku ya tatu na ya saba, hatakuwa safi. 19:13 Law 21:11; 15:31; 2Nya 36:14; Za 79:1; Law 22:3; 7:20; Hag 2:13Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote na kushindwa kujitakasa mwenyewe hunajisi Maskani ya Bwana. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na Israeli. Kwa sababu hajanyunyiziwa maji ya utakaso, yeye ni najisi; unajisi wake unabaki juu yake.

“Hii ndiyo sheria itumikayo wakati mtu amekufa ndani ya hema: Yeyote aingiaye ndani ya hema hilo na yeyote aliye ndani yake watakuwa najisi kwa muda wa siku saba, 19:15 Law 6:28nacho kila chombo kisicho na kifuniko juu yake kitakuwa najisi.

19:16 Hes 31:19; 1Fal 13:2; 2Fal 23:14; Eze 6:5; 2Fal 23:6; Mt 23:27; Law 5:3“Mtu yeyote aliyeko nje mahali pa wazi agusaye mtu aliyeuawa kwa upanga au mtu aliyekufa kwa kifo cha kawaida, au mtu yeyote agusaye mfupa wa mtu aliyekufa au kaburi, atakuwa najisi kwa siku saba.

19:17 Hes 8:7“Kwa mtu aliye najisi, weka majivu ya sadaka ya utakaso wa dhambi ndani ya chombo, umimine maji safi juu yao. 19:18 Kut 12:22; Law 4:17Kisha mtu aliye safi kwa kawaida za kiibada atachukua hisopo, achovye ndani ya maji, na kunyunyizia hema na vifaa vyote pamoja na watu ambao walikuwamo. Pia ni lazima amnyunyizie mtu yeyote ambaye amegusa mfupa wa mtu aliyekufa, au kaburi, au mtu ambaye ameuawa, au mtu ambaye amekufa kifo cha kawaida. 19:19 Law 16:14-15; Hes 31:19; Eze 36:25; Ebr 10:22; Mwa 35:2Mtu ambaye ni safi ndiye atakayemnyunyizia yeyote ambaye ni najisi siku ya tatu na siku ya saba, na katika siku ya saba atamtakasa mtu huyo. Mtu ambaye ametakaswa lazima afue nguo zake na kuoga kwa maji, na jioni ile atakuwa safi. 19:20 Za 14:7; Law 15:31; 14:8Lakini ikiwa mtu ambaye ni najisi hakujitakasa mwenyewe, ni lazima akatiliwe mbali na jumuiya, kwa sababu ameinajisi Maskani ya Bwana. Maji ya utakaso hayajanyunyizwa juu yake, naye ni najisi. 19:21 Kut 27:21Hii ni sheria ya kudumu kwao.

“Mtu yeyote ambaye ananyunyiza yale maji ya utakaso lazima pia afue nguo zake, na yeyote ambaye hugusa maji ya utakaso atakuwa najisi mpaka jioni. 19:22 Law 5:2; 15:4-12Kitu chochote anachogusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi, na yeyote akigusaye huwa najisi mpaka jioni.”

Read More of Hesabu 19

Hesabu 20:1-29

Maji Kutoka Kwenye Mwamba

(Kutoka 17:1-7)

20:1 Hes 13:21; 13:26; 33:36; Kum 1:46; Amu 11:17; Za 29:8; Kut 15:20Katika mwezi wa kwanza jumuiya yote ya Kiisraeli ilifika kwenye Jangwa la Sini, nao wakakaa Kadeshi. Miriamu akafa huko na kuzikwa.

20:2 Kut 15:22; 17:1; Hes 16:19Mahali hapo hapakuwa na maji kwa ajili ya jumuiya hiyo, nao wakakusanyika ili kumpinga Mose na Aroni. 20:3 Mwa 13:7; Kut 17:2; 21:18; 5:21; Hes 14:2; 16:31-35Watu wakagombana na Mose, na kusema, “Laiti tungelikufa wakati ndugu zetu walipoanguka na kufa mbele za Bwana! 20:4 Hes 14:2; Kut 14:11; Hes 14:3; 16:13Kwa nini mmeileta jumuiya ya Bwana kwenye jangwa hili, ili tufe humu, sisi na mifugo yetu? 20:5 Hes 13:23; 16:14; Kut 17:1Kwa nini mmetupandisha kutoka Misri mpaka mahali hapa pa kutisha? Hapa hakuna nafaka wala tini, zabibu au makomamanga. Wala hapa hakuna maji ya kunywa!”

20:6 Kut 40:2; Hes 14:5; 16:19Mose na Aroni wakaondoka pale kwenye kusanyiko mpaka kwenye mlango wa Hema la Kukutania na kuanguka kifudifudi, nao utukufu wa Bwana ukawatokea. Bwana akamwambia Mose, 20:8 Kut 4:2; 10:12-13; 17:6; Isa 41:18; 43:20; Yer 31:9“Chukua ile fimbo, na wewe na ndugu yako Aroni mkusanye kusanyiko pamoja. Nena na ule mwamba mbele ya macho yao, nao utatoa maji yake. Utatoa maji kutoka huo mwamba kwa ajili ya jumuiya ili wao na mifugo yao waweze kunywa.”

20:9 Hes 17:2; 17:10Kwa hiyo Mose akaichukua hiyo fimbo kutoka pale ilipokuwa mbele za Bwana kama alivyomwagiza. 20:10 Za 106:32-33Mose na Aroni wakakusanya kusanyiko pamoja mbele ya huo mwamba, naye Mose akawaambia, “Sikilizeni, enyi waasi. Je, ni lazima tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?” 20:11 Kut 17:6; Isa 33:21Ndipo Mose akainua mkono wake na kuupiga mwamba mara mbili kwa fimbo yake. Maji yakabubujika, nayo jumuiya na mifugo yao wakanywa.

20:12 Hes 27:14; Kum 32:51; Isa 5:16; 8:13; Kum 3:27Lakini Bwana akamwambia Mose na Aroni, “Kwa sababu hamkuniamini mimi kiasi cha kuniheshimu kama mtakatifu machoni pa Waisraeli, hamtaiingiza jumuiya hii katika nchi ninayowapa.”

20:13 Kut 17:7; Law 10:3Haya yalikuwa maji ya Meriba,20:13 Meriba maana yake Kugombana. mahali pale ambapo Waisraeli waligombana na Bwana, naye akajionyesha mwenyewe huko kuwa mtakatifu katikati yao.

Edomu Wakatalia Israeli Kupita

20:14 Hes 20:1, 16; Mwa 36:16; 25:30; 24:3; Kum 4:39; Yos 2:11; 9:9; Kut 18:8Mose akawatuma wajumbe kutoka Kadeshi kwenda kwa mfalme wa Edomu, akisema:

“Hili ndilo ndugu yako Israeli asemalo: Wewe unafahamu juu ya taabu zote ambazo zimetupata. 20:15 Mwa 46:6; 15:13; Kut 1:14Baba zetu walishuka Misri, nasi tumeishi huko miaka mingi. Wamisri walitutesa sisi na baba zetu, 20:16 Mwa 16:11; 21:17; Kut 2:23; 14:19; 12:42; Kum 26:8; Hes 33:37lakini tulipomlilia Bwana, alisikia kilio chetu na akamtuma malaika akatutoa Misri.

“Sasa tupo hapa Kadeshi, mji ulio mpakani mwa nchi yako. 20:17 Hes 21:22; Kum 2:27; Amu 11:17Tafadhali turuhusu tupite katika nchi yako. Hatutapita katika shamba lolote, wala shamba la mizabibu, au kunywa maji kutoka kwenye kisima chochote. Tutasafiri kufuata njia kuu ya mfalme, na hatutageuka kulia wala kushoto mpaka tuwe tumeshapita nchi yako.”

20:18 Hes 21:23Lakini mfalme wa Edomu akajibu:

“Hamtapita hapa; kama mkijaribu kupita, tutatoka na kuwashambulia kwa upanga.”

20:19 Kut 2:23; Kum 2:6, 28Waisraeli wakajibu:

“Sisi tutafuata njia kuu; tena ikiwa sisi au mifugo yetu tutakunywa tone la maji yenu, tutalilipia. Sisi tunataka tu kupita kwa miguu, wala si kitu kingine chochote.”

Watu wa Edomu wakajibu tena:

“Hamwezi kupita hapa.”

Ndipo watu wa Edomu wakatoka dhidi ya Waisraeli, jeshi kubwa lenye nguvu. 20:21 Hes 21:23; 21:4; Kum 2:8; Amu 11:18Kwa kuwa Waedomu waliwakatalia Waisraeli kupita katika nchi yao, Israeli wakageuka, wakawaacha.

Kifo Cha Aroni

20:22 Kum 1:46; Hes 33:37; 34:7; Kum 32:50Jumuiya yote ya Kiisraeli ikaondoka kutoka Kadeshi, wakafika kwenye Mlima Hori. Kwenye Mlima Hori, karibu na mpaka wa Edomu, Bwana akamwambia Mose na Aroni, 20:24 Mwa 25; 8; Kut 17:7“Aroni atakusanywa pamoja na watu wake. Hataingia katika nchi ninayowapa Waisraeli, kwa sababu ninyi wawili mliasi dhidi ya agizo langu kwenye maji ya Meriba. 20:25 Hes 33:38Watwae Aroni na Eleazari mwanawe, na uwapandishe juu katika Mlima wa Hori. 20:26 Kut 28:1-4; 40:13; Law 16:4; Hes 27:13; 31:2Mvue Aroni mavazi yake, na umvike Eleazari mwanawe, kwa maana Aroni atakusanywa pamoja na watu wake; atakufa huko.”

20:27 Hes 33:38Mose akafanya kama Bwana alivyomwagiza: Wakapanda Mlima Hori mbele ya macho ya jumuiya yote ya Kiisraeli. 20:28 Kut 29:29; Hes 33:38; Kum 10:6; 32:50; Mwa 27:41; Law 10:6; Kum 34:8Mose akamvua Aroni mavazi yake na kumvika mwanawe Eleazari mavazi hayo. Naye Aroni akafia pale juu ya mlima. Kisha Mose na Eleazari wakateremka kutoka mlimani. Jumuiya yote ilipofahamu kwamba Aroni amekufa, jamaa yote ya Kiisraeli wakamwomboleza kwa siku thelathini.

Read More of Hesabu 20

Hesabu 21:1-3

Nchi Ya Aradi Yaangamizwa

21:1 Hes 33:40; Yos 12:14; Mwa 12:9; Hes 13:17; Kum 1:7; Amu 1:9Mfalme wa Kikanaani wa Aradi aliyeishi huko Negebu aliposikia kwamba Waisraeli walikuwa wanakuja kwa njia ya Atharimu, aliwashambulia Waisraeli na kuwateka baadhi yao. 21:2 Law 7:16; Kut 22:20; Kum 2:34; Yos 2:10; 8:26; Yer 25:9; 50:21Ndipo Israeli akaweka nadhiri hii kwa Bwana: “Ikiwa utawatia watu hawa mikononi mwetu, tutaiangamiza kabisa miji yao.” 21:3 Mwa 10:18; Hes 14:45Bwana akasikiliza ombi la Waisraeli, naye akawapa ushindi juu ya Wakanaani. Wakawaangamiza kabisa na miji yao; hivyo mahali pale pakaitwa Horma.21:3 Horma maana yake Maangamizi.

Read More of Hesabu 21