Hesabu 16:36-50, Hesabu 17:1-13, Hesabu 18:1-32 NEN

Hesabu 16:36-50

Bwana akamwambia Mose, 16:37 Kut 6:23“Mwambie Eleazari mwana wa kuhani Aroni, atoe vyetezo kwenye mabaki ya moto na kutawanya makaa mbali kiasi, kwa maana vyetezo ni vitakatifu: 16:38 Law 10:1; Mit 20:2; Kut 20:24; 38:1-7; Hes 26:10; Kum 28:46; Yer 44:29; Eze 14:8; 2Pet 2:6vyetezo vya watu waliofanya dhambi iliyowagharimu maisha yao. Fua vyetezo hivyo kuwa bamba ili kufunika madhabahu, kwa maana vimeletwa mbele za Bwana na vimekuwa vitakatifu. Navyo viwe ishara kwa Waisraeli.”

16:39 2Nya 26:18; Law 20:14Hivyo kuhani Eleazari akavikusanya vile vyetezo vya shaba vilivyoletwa na wale waliokuwa wameteketezwa kwa moto, naye akavifua kufunika madhabahu, 16:40 Kut 30:1, 9; Isa 1:13; 66:3; Yer 41:5; 44:3; 2Nya 26:18; Hes 3:10kama vile Bwana alivyomwelekeza kupitia Mose. Hili lilikuwa kuwakumbusha Waisraeli kwamba hakuna mtu hata mmoja, isipokuwa mzao wa Aroni, awezaye kuja kufukiza uvumba mbele za Bwana, la sivyo, angekuwa kama Kora na wafuasi wake.

16:41 Hes 14:2; Za 106:13; Mdo 21:28Siku iliyofuata jumuiya yote ya Kiisraeli wakanungʼunika dhidi ya Mose na Aroni, wakisema, “Mmewaua watu wa Bwana.”

16:42 Kut 16:7; Hes 14:10; 20:6; Law 9:23Lakini wakati kusanyiko lilipokusanyika kupingana na Mose na Aroni, nalo likageuka kuelekea Hema la Kukutania, ghafula wingu likafunika Hema, nao utukufu wa Bwana ukatokea. Ndipo Mose na Aroni wakaenda mbele ya Hema la Kukutania, naye Bwana akamwambia Mose, 16:45 Kut 32:10; 1Nya 16:21; Mt 26:39“Jitenge mbali na kusanyiko hili ili niweze kuwaangamiza mara moja.” Wakaanguka chini kifudifudi.

16:46 Law 10:1-6; 26:25; Kut 29:36; Hes 1:53; 8:19; Za 106:29; Yos 7:1; 22:18; 1Sam 6:19; 2Sam 24:1; 1Nya 17:24Kisha Mose akamwambia Aroni, “Chukua chetezo chako na uweke uvumba ndani yake, pamoja na moto kutoka madhabahuni, nawe uende haraka kwenye kusanyiko ili kufanya upatanisho kwa ajili yao. Ghadhabu imekuja kutoka kwa Bwana, na tauni imeanza.” 16:47 Hes 25:6-8Hivyo Aroni akafanya kama Mose alivyosema, akakimbilia katikati ya kusanyiko. Tauni ilikuwa tayari imeanza miongoni mwa watu, lakini Aroni akafukiza uvumba na kufanya upatanisho kwa ajili yao. 16:48 Hes 25:8; Za 106:30; 2Sam 24:16-17; Ay 33:24; Yak 5:16; 1The 1:10; Ebr 7:24Aroni akasimama kati ya waliokuwa hai na waliokufa, nayo tauni ikakoma. Lakini walikufa watu 14,700 kutokana na tauni hiyo, licha ya wale waliokuwa wamekufa kwa sababu ya Kora. Ndipo Aroni akamrudia Mose kwenye mlango wa Hema la Kukutania, kwa maana tauni ilikuwa imekoma.

Read More of Hesabu 16

Hesabu 17:1-13

Kuchipuka Kwa Fimbo Ya Aroni

Bwana akamwambia Mose, 17:2 Mwa 32:10; Kut 4:2; Hes 1:4“Sema na Waisraeli, na ujipatie fimbo kumi na mbili kutoka kwao, moja kutoka kwa kila mmoja wa viongozi wa kabila za baba zao. Andika jina la kila mtu kwenye fimbo yake. 17:3 Hes 1:3Kwenye fimbo ya Lawi andika jina la Aroni, kwa maana ni lazima iwepo fimbo moja kwa kila kiongozi kwa ajili ya kila kabila la baba zao. 17:4 Kut 1:3; 16:34; 25:22Ziweke hizo fimbo ndani ya Hema la Kukutania mbele ya Sanduku la Ushuhuda, mahali nikutanapo nawe. 17:5 Hes 16:5; Kut 16:7Fimbo ya mtu nitakayemchagua itachipuka, nami mwenyewe nitayakomesha haya manungʼuniko ya mara kwa mara ya Waisraeli dhidi yako.”

Hivyo Mose akasema na Waisraeli, nao viongozi wao wakampa fimbo kumi na mbili, fimbo moja kwa ajili ya kila kabila la baba zao, nayo fimbo ya Aroni ikiwa miongoni mwa hizo. 17:7 Kut 38:21; Mdo 7:44Mose akaziweka hizo fimbo mbele za Bwana ndani ya Hema la Ushuhuda.

17:8 Hes 1:50; Eze 17:24; Ebr 9:4Siku iliyofuata Mose aliingia kwenye Hema la Ushuhuda akaona ile fimbo ya Aroni ambayo iliwakilisha jamaa ya Lawi haikuwa tu imechipuka, bali pia ilikuwa imetoa machipukizi, kuchanua maua na kuzaa malozi. Ndipo Mose akaleta zile fimbo zote kwa Waisraeli wote kutoka mbele za Bwana. Wakaziangalia, na kila mtu akaichukua fimbo yake mwenyewe.

17:10 Kut 23:21; Za 66:7; 68:18; Mit 24:21Bwana akamwambia Mose, “Rudisha fimbo ya Aroni mbele ya Sanduku la Ushuhuda, ili ihifadhiwe kama alama kwa waasi. Hili litakomesha manungʼuniko yao dhidi yangu, ili kwamba wasife.” Mose akafanya kama Bwana alivyomwamuru.

17:12 Amu 13:22; Isa 6:5; 15:1Waisraeli wakamwambia Mose, “Tutakufa! Tumepotea, sote tumepotea! 17:13 Hes 1:51Yeyote akaribiaye Maskani ya Bwana atakufa. Je, sisi sote tutakufa?”

Read More of Hesabu 17

Hesabu 18:1-32

Wajibu Wa Makuhani Na Walawi

18:1 Kut 28:38Bwana akamwambia Aroni, “Wewe, wanao na jamaa ya baba yako mtawajibika kwa makosa dhidi ya mahali patakatifu, na wewe na wanao peke yenu ndio mtakaowajibika kwa makosa dhidi ya ukuhani. 18:2 Hes 3:10Walete Walawi wenzako kutoka kabila la baba zako ili waungane nanyi na kuwasaidia wakati wewe na wanao mnapohudumu mbele ya Hema la Ushuhuda. 18:3 Hes 3:32; 1:51Watawajibika kwenu na watafanya kazi zote za Hema, lakini kamwe wasisogelee vifaa vya patakatifu au madhabahu, la sivyo wao na ninyi mtakufa. 18:4 Hes 3:34Watajiunga nanyi na watawajibika kwa utunzaji wa Hema la Kukutania, yaani kazi zote kwenye Hema, wala hakuna mtu mwingine yeyote atakayeweza kusogea karibu hapo mlipo.

18:5 Law 6:12“Mtawajibika katika utunzaji wa mahali patakatifu na madhabahu, ili kwamba ghadhabu isiwaangukie Waisraeli tena. 18:6 Hes 3:8-9Mimi mwenyewe nimewachagua Walawi wenzenu kutoka miongoni mwa Waisraeli kama zawadi kwenu, waliowekwa wakfu kwa Bwana ili kufanya kazi katika Hema la Kukutania. 18:7 Ebr 9:3, 6; Kut 29:9; 40:13; Ebr 5:4; Hes 3:10Lakini ni wewe tu na wanao mtakaoweza kutumika kama makuhani kuhusiana na kila kitu kwenye madhabahu na ndani ya pazia. Ninawapa utumishi wa ukuhani kama zawadi. Mtu mwingine yeyote atakayekaribia mahali patakatifu ni lazima auawe.”

Sadaka Kwa Ajili Ya Makuhani Na Walawi

18:8 Law 2:2; 6:16; 7:6, 31-34; Kum 18:1; 2Nya 31:4Kisha Bwana akamwambia Aroni, “Mimi mwenyewe nimekuweka kuwa mwangalizi wa sadaka zote zitakazotolewa kwangu; matoleo yote matakatifu Waisraeli wanayonipa ninakupa wewe na wanao kama sehemu yenu na fungu lenu la kawaida. 18:9 Law 6:17; 2:1; 6:25; 5:15Mtachukua sehemu ya yale matoleo matakatifu sana ambayo hayateketezwi kwa moto. Kutoka kwa matoleo yote wanayoniletea kama sadaka takatifu sana, ziwe za nafaka, au za dhambi, au za makosa, sehemu ile itakuwa yako na wanao. 18:10 Law 6:16; 6:17-18Mtaila kama kitu kilicho kitakatifu sana; kila mwanaume ataila. Ni lazima mtaiheshimu kama takatifu.

18:11 Kut 29:26; Law 7:30; Hes 6:20; Law 7:31-34; 13:3; 22:1-16“Hiki pia ni chako: chochote kilichotengwa kutoka kwenye matoleo yote ya sadaka za kuinuliwa za Waisraeli. Ninakupa wewe haya, wana na binti zako kama sehemu yenu ya kawaida. Kila mmoja wa nyumba yako ambaye ni safi kwa taratibu za ibada anaweza kuyala.

18:12 Kum 7:13; 11:14; 12:17; 28:51; 2Fal 18:32; 2Nya 31:5; Neh 10:35, 37; Law 23:19; Kut 34:26“Ninawapa mafuta ya zeituni yaliyo bora kuliko yote, na divai mpya iliyo bora kuliko zote na nafaka wanazompa Bwana kama malimbuko katika mavuno yao. 18:13 Kut 29:27Malimbuko yote ya nchi ambayo wanamletea Bwana yatakuwa yenu. Kila mmoja nyumbani kwako ambaye ni safi kwa taratibu za Ibada anaweza kula.

18:14 Law 27:21; Yos 6:17-19“Kila kitu katika Israeli ambacho kimetolewa kwa Bwana ni chenu. 18:15 Kut 13:2; Hes 3:46; Mwa 10:15; Kut 13:13Kila mzaliwa wa kwanza wa mwanadamu na wa mnyama, ambaye ametolewa kwa Bwana ni wenu. Lakini ni lazima mtamkomboa kila mwana mzaliwa wa kwanza na kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa wanyama wasio safi. 18:16 Hes 3:15; Law 27:6; Kut 30:13; Hes 3:47Watakapokuwa na umri wa mwezi mmoja, ni lazima mtawakomboa kwa bei ya ukombozi iliyowekwa, kwa shekeli tano18:16 Shekeli tano za fedha ni sawa na gramu 55. za fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, yenye uzito wa gera ishirini.18:16 Gera 20 ni sawa na gramu 55.

18:17 Law 27:4; 3:2; Kut 29:13; Law 1:4“Lakini kamwe usimkomboe mzaliwa wa kwanza wa maksai, kondoo au mbuzi; hawa ni watakatifu. Nyunyizia damu yao juu ya madhabahu na uchome mafuta yao kama sadaka itolewayo kwa moto, harufu nzuri inayompendeza Bwana. 18:18 Law 7:30Nyama zao zitakuwa chakula chenu, kama ilivyokuwa kidari cha kuinuliwa na paja la mguu wa kulia. 18:19 2Fal 12:4; Law 2:13Chochote kitakachotengwa kutoka sadaka takatifu ambazo Waisraeli wanamtolea Bwana, ninakupa wewe, wanao na binti zako kama fungu lenu la kawaida. Ni Agano la milele la chumvi mbele za Bwana kwako na watoto wako.”

18:20 Hes 26:62; Kum 12:12; 10:9; 14:27; 18:1-2; Yos 13:33; Eze 44:28Bwana akamwambia Aroni, “Hutakuwa na urithi wowote katika nchi yao, wala hutakuwa na sehemu miongoni mwao; Mimi ni fungu lako na urithi wako miongoni mwa Waisraeli.

18:21 Mwa 28:22; Hes 31:28; Kum 14:22; Neh 10:33; 13:5; Mal 3:8; Law 27:30-33; Ebr 7:5; Hes 1:53“Ninawapa Walawi zaka yote katika Israeli kama urithi wao kuwa kama malipo kwa kazi wanayoifanya wakati wanapohudumu katika Hema la Kukutania. 18:22 Kut 28:43Kuanzia sasa, kamwe Waisraeli wasisogelee karibu na Hema la Kukutania, la sivyo watabeba matokeo ya dhambi zao, nao watakufa. 18:23 Kut 12:14; 27:21; Hes 10:8; 26:62; Kum 10:9; Eze 44:10Ni Walawi watakaofanya kazi katika Hema la Kukutania na kubeba wajibu wa makosa dhidi yake. Hili ni agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. Hawatapokea urithi wowote miongoni mwa Waisraeli. 18:24 Law 27:30; Kum 26:12Badala yake, ninawapa Walawi zaka zote zinazotolewa na Waisraeli kama sadaka kwa Bwana kuwa urithi wao. Hiyo ndiyo sababu nimesema hivi kuhusu wao: ‘Hawatakuwa na urithi miongoni mwa Waisraeli.’ ”

Bwana akamwambia Mose, 18:26 Neh 10:38“Sema na Walawi na uwaambie: ‘Mtakapopokea zaka kutoka kwa Waisraeli ambayo ninawapa kama urithi wenu kutoka kwao, ni lazima mtoe sehemu ya kumi ya hiyo zaka kama sadaka kwa Bwana, iwe zaka ya hiyo zaka. 18:27 Law 7:18; Mwa 50:10; Kum 15:14; Amu 6:37; Rut 3:3, 6, 14; 1Sam 23:1Sadaka yenu itahesabiwa kwenu kama nafaka kutoka sakafu ya kupuria, au divai kutoka kwenye shinikizo la kukamulia zabibu. 18:28 Mal 3:8Kwa njia hii, ninyi pia mtatoa sadaka kwa Bwana kutoka zaka zote mtakazopokea kutoka kwa Waisraeli. Kutoka kwenye zaka hizi, ni lazima mtoe sehemu ya Bwana kwa Aroni, kuhani. Ni lazima mtoe kama sehemu ya Bwana iliyo nzuri sana tena ile sehemu iliyo takatifu sana kuliko zote ya kile kitu mlichopewa.’

“Waambie Walawi: ‘Mtakapotoa sehemu zilizo bora sana, itahesabiwa kwenu kama mazao ya sakafu ya kupuria nafaka, au ya shinikizo la kukamulia zabibu. Ninyi na watu wa nyumbani mwenu mnaweza kula sehemu iliyobaki mahali popote, kwani ndio ujira wenu kwa ajili ya kazi yenu katika Hema la Kukutania. 18:32 Law 22:15; 19:8Kwa kutoa sehemu zake zilizo bora sana, hamtakuwa na hatia katika jambo hili; ndipo hamtatia unajisi sadaka takatifu za Waisraeli, nanyi hamtakufa.’ ”

Read More of Hesabu 18