Hesabu 11:4-35, Hesabu 12:1-16, Hesabu 13:1-25 NEN

Hesabu 11:4-35

Kware Kutoka Kwa Bwana

11:4 Kut 12:38; 16:3; Za 78:18; 1Kor 10:6Umati wa watu wenye zogo waliokuwa miongoni mwao walitamani sana chakula kingine, Waisraeli wakaanza kulia tena na kusema, “Laiti tungekuwa na nyama tule! 11:5 Kut 16:3; Hes 21:5; Flp 3:19; Mt 6:24-34; Rum 8:7Tunakumbuka wale samaki tuliokula huko Misri bila gharama, pia yale matango, matikitimaji, mboga, vitunguu, na vitunguu saumu. 11:6 Kut 16:14Lakini sasa tumepoteza hamu ya chakula; hatuoni kitu kingine chochote isipokuwa hii mana!”

11:7 Kut 16:31; Mwa 2:12; 2:12Mana ilifanana kama mbegu za giligilani, nayo ilikuwa na rangi ya manjano iliyopauka. 11:8 Kut 16:16Hao watu walikwenda kukusanya, kisha waliisaga kwa mawe ya kusagia ya mkono au kuitwanga kwenye vinu. Waliipika vyunguni au kutengeneza maandazi. Ladha yake ilikuwa kama kitu kilichotengenezwa kwa mafuta ya zeituni. 11:9 Kut 16:13Umande ulipoanguka kambini wakati wa usiku, pia mana ilianguka pamoja nao.

Mose akasikia watu wa kila jamaa wakilia, kila mmoja kwenye mlango wa hema lake. Bwana akakasirika mno, naye Mose akafadhaika. 11:11 Mwa 34:30; Kut 5:22; 18:18; 17:4; Kum 1:12; Yer 15:10, 18; 20:7-18; Mal 3:14; 2Kor 11:28Akamuuliza Bwana, “Kwa nini umeleta taabu hii juu ya mtumishi wako? Nimekufanyia nini cha kukuchukiza hata ukaweka mzigo huu wa watu hawa wote juu yangu? 11:12 Isa 40:11; 49:23; 66:11, 12; Hes 14:16; Mwa 12:7; Kut 13:5; Eze 34:23; Yn 10:11; 1The 2:7; Mwa 22:16; 26:3Je, watu hawa wote mimi ndiye niliyewatungisha mimba? Je, ni mimi niliyewazaa? Kwa nini unaniambia niwachukue mikononi mwangu, kama vile mlezi abebavyo mtoto mchanga, hadi kwenye nchi uliyowaahidi baba zao? 11:13 Kut 12:37; Yn 6:5-9; 2Fal 4:43; Mt 15:33; Mk 8:4Nitapata wapi nyama kwa ajili ya watu wote hawa? Wanaendelea kunililia wakisema, ‘Tupe nyama tule!’ 11:14 Kut 18:18Mimi siwezi kuwabeba watu hawa wote peke yangu, mzigo ni mzito sana kwangu. 11:15 Kut 32:32; 1Fal 19:4; Ay 6:9; 7:15-16; 9:21; Isa 38:12; Yn 4:3Kama hivi ndivyo unavyonitendea, uniue sasa hivi, yaani kama nimepata kibali machoni pako, wala usiniache nione maangamizi yangu mwenyewe.”

11:16 Kut 3:16; 18:25; 40:2; 24:1, 9Bwana akamwambia Mose: “Niletee wazee sabini wa Israeli, unaowafahamu kama viongozi na maafisa miongoni mwa watu. Walete katika Hema la Kukutania, ili waweze kusimama huko pamoja nawe. 11:17 Kut 18:18; 19:20; 1Sam 10:6; 2Fal 2:9, 15; 3:12; Isa 32:15; Yoe 2:28; Hag 2:5; Yer 19:1Nami nitashuka na kusema nawe huko. Nami nitachukua sehemu ya Roho iliyo juu yako na kuiweka juu yao. Watakusaidia kubeba mzigo wa watu hao ili usije ukaubeba peke yako.

11:18 Kut 19:10; 16:7; Mdo 7:39; Za 78:20“Waambie hao watu: ‘Jiwekeni wakfu wenyewe kwa ajili ya kesho, wakati mtakapokula nyama. Bwana aliwasikia mlipolia, mkisema, “Laiti tungekuwa na nyama tule! Tulikuwa na hali nzuri zaidi katika nchi ya Misri!” Sasa Bwana atawapa nyama, nanyi mtaila. Hamtaila kwa siku moja tu, au siku mbili, au tano, kumi au siku ishirini, 11:20 Za 78:29; 106:14-15; Law 26:43; Ay 1:14; 20:13, 23; Yos 24:27; Amu 8:23; 1Sam 10:19; Isa 59:13; Hos 13:11bali kwa mwezi mzima mpaka iwatokee puani, nanyi mtaichukia kabisa, kwa kuwa mmemkataa Bwana, ambaye yupo miongoni mwenu, nanyi mmelia mbele zake, mkisema, “Hivi kwa nini tulitoka Misri?” ’ ”

11:21 Kut 12:37Lakini Mose alisema, “Mimi niko hapa miongoni mwa watu 600,000 wanaotembea kwa miguu, nawe umesema, ‘Nitawapa nyama ya kula kwa mwezi mzima!’ 11:22 Mt 15:33; 2Fal 7:2; Mk 6:37Je, wangeweza kupata nyama ya kuwatosha hata kama makundi ya kondoo na ya ngʼombe yangechinjwa kwa ajili yao? Je, wangetosheka hata kama samaki wote wa baharini wangevuliwa kwa ajili yao?”

11:23 Isa 50:2; 59:1; Hes 23:19; 1Sam 15:29; Eze 12:25; 24:14Bwana akamjibu Mose, “Je, mkono wa Bwana ni mfupi sana? Sasa utaona kama jambo nililolisema litatimizwa kwa ajili yako au la.”

Kwa hiyo Mose akatoka na kuwaambia watu lile ambalo Bwana alikuwa amesema. Akawakusanya wazee wao sabini, akawasimamisha kuzunguka Hema. 11:25 Kut 19:9; Hes 12:5; 1Sam 10:6, 10; 19:20, 23; Mdo 2:17; Amu 3:10; Kut 34:5; 40:38; 2Fal 2:15; Yoe 2:29; 1Kor 14:1Kisha Bwana akashuka katika wingu na kunena na Mose, naye akachukua sehemu ya Roho iliyokuwa juu ya Mose na kuiweka juu ya wale wazee sabini. Roho aliposhuka juu yao, wakatoa unabii, lakini hawakufanya hivyo tena.

11:26 1Nya 12:18; Ufu 1:10; 1Sam 20:26; Yer 36:5Lakini, watu wawili, ambao majina yao ni Eldadi na Medadi, walibaki kambini. Walikuwa wameorodheshwa miongoni mwa wale wazee sabini, lakini hawakutoka kwenda kwenye Hema. Lakini Roho pia alishuka juu yao, nao wakatabiri huko kambini. Mwanaume mmoja kijana alikimbia na kumwambia Mose, “Eldadi na Medadi wanatoa unabii kambini.”

11:28 Kut 17:9; 33:11; Hes 13:8; 26:65; Yos 14:10; Mk 9:38-40; Mdo 26:29; 1Kor 14:5Yoshua mwana wa Nuni, ambaye alikuwa msaidizi wa Mose tangu ujana wake, akajibu akasema, “Mose bwana wangu, wanyamazishe!”

11:29 1Sam 10:5; 19:20; 2Nya 24:19; Yer 7:25; 44:4; 1Kor 14:5; Hes 27:18Lakini Mose akajibu, “Je, unaona wivu kwa ajili yangu? Ningetamani watu wote wa Bwana wangekuwa manabii na kwamba Bwana angeweka Roho yake juu yao!” Ndipo Mose na wale wazee wa Israeli wakarudi kambini.

11:31 Kut 16:13; Za 78:26-28Kisha ukatokea upepo kutoka kwa Bwana, nao ukawaletea kware kutoka baharini. Ukawaangusha kwenye eneo lote linalozunguka kambi na kujaa ardhini kimo cha mita moja hivi kutoka ardhini kwenye eneo la umbali wa mwendo wa siku moja kila upande. 11:32 Kut 16:36; Eze 45:11Mchana kutwa na usiku kucha pamoja na siku nzima iliyofuata watu walitoka kwenda kuokota kware. Hakuna mtu yeyote aliyekusanya chini ya homeri kumi.11:32 Homeri 10 ni sawa na kilo 1,000. Kisha wakazianika kuzunguka kambi yote. 11:33 Za 78:30; 106:15, 29; Hes 14:18; Kum 9:7; Amu 2:12; 2Fal 22:17; Yer 44:3; Eze 8:17; Isa 10:16Lakini walipokuwa wakila nyama, ilipokuwa ingali kati ya meno yao na kabla hawajamaliza kula, hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya watu, naye akawapiga kwa tauni. 11:34 Hes 33:16; Kum 9:22Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Kibroth-Hataava,11:34 Kibroth-Hataava maana yake Makaburi ya wenye tamaa nyingi. kwa sababu huko ndiko walipowazika watu ambao walitamani sana chakula kingine.

11:35 Hes 33:17; Kum 1:1Kutoka Kibroth-Hataava watu wakasafiri mpaka Haserothi na kukaa huko.

Read More of Hesabu 11

Hesabu 12:1-16

Miriamu Na Aroni Wampinga Mose

12:1 Kut 15:20; 2:21Miriamu na Aroni walianza kuzungumza dhidi ya Mose kwa sababu ya mke wake Mkushi, kwa kuwa alikuwa ameoa Mkushi. 12:2 Hes 16:3; 11:1; Mwa 29:33; Mik 6:4; 2Fal 19:4; Za 94:9; Eze 35:12Waliuliza, “Je, Bwana amesema kupitia Mose peke yake? Je, hajasema kutupitia sisi pia?” Naye Bwana akasikia hili.

12:3 Mt 11:29; 1Tim 6:11; 2Tim 2:25; Za 149:4; 1Pet 3:4(Basi Mose alikuwa mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine yeyote katika uso wa dunia.)

Ghafula Bwana akawaambia Mose, Aroni na Miriamu, “Njooni katika Hema la Kukutania, ninyi nyote watatu.” Kwa hiyo wote watatu wakaenda. 12:5 Kut 13:21; Hes 11:25; Kut 34:5Kisha Bwana akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye ingilio la Hema, akawaita Aroni na Miriamu. Wakati wote wawili waliposogea mbele, 12:6 1Sam 3:7, 21; Mwa 15:1; 20:3; 46:2; Mt 27:19; Ebr 1:1; 1Fal 3:5; Mwa 46:2; Ay 33:15; Lk 1:11; 1:22; Mt 1:20Bwana akasema, “Sikilizeni maneno yangu:

“Akiwapo nabii wa Bwana miongoni mwenu,

nitajifunua kwake kwa maono,

nitanena naye katika ndoto.

12:7 Kum 34:5; Yos 1:1-2; Za 105:26; Ebr 3:2, 5Lakini sivyo kwa mtumishi wangu Mose;

yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.

12:8 Amu 14:12; 1Fal 10:1; Za 17:15; 49:4; 140:13; Mit 1:6; Dan 5:12; Kut 20:4; 24:2; Ay 19:26; Isa 6:1Kwake nitanena naye uso kwa uso,

waziwazi wala si kwa mafumbo;

yeye ataona umbo la Bwana.

Kwa nini basi ninyi hamkuogopa

kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Mose?”

12:9 Kut 4:14; Mwa 17:22Hasira ya Bwana ikawaka dhidi yao, akawaacha.

12:10 Kut 4:6; 40:2; Kum 24:9; Law 13:11; 2Fal 5:1, 27; 2Nya 16:12; 21:12Wakati hilo wingu liliinuka kutoka juu ya Hema, Miriamu akawa tayari ana ukoma, mweupe kama theluji. Aroni akamgeukia, akaona ana ukoma. 12:11 2Sam 19:19; 24:10Kisha Aroni akamwambia Mose, “Tafadhali, bwana wangu, usituhesabie dhambi hii ambayo tumeifanya kwa upumbavu. 12:12 Za 88:4; Efe 2:1-5; Kol 2:13; 1Tim 5:6Usimwache awe kama mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa mfu, ambaye nusu ya mwili wake imeharibika hapo atokapo katika tumbo la mama yake.”

12:13 Kut 15:26; Za 6:2; 147:3; Isa 1:6; 30:26; 53:5; Yer 17:14; Hos 6:1Hivyo Mose akamlilia Bwana akisema, “Ee Mungu, nakuomba umponye!”

12:14 Kum 25:9; Ay 17:6; 30:9-10; Isa 50:6; Law 13:46; Hes 5:2-3; Ebr 12:9; 2Nya 26:20, 21Bwana akamjibu Mose, “Je, kama baba yake angemtemea usoni, asingeona aibu kwa siku saba? Mfungie nje ya kambi kwa siku saba; baada ya hapo anaweza kurudishwa kambini.” 12:15 Law 14:8; 13; Kum 24:9Kwa hiyo Miriamu akafungiwa nje ya kambi kwa siku saba, nao watu hawakuendelea na safari mpaka aliporudishwa kambini.

12:16 Hes 10:12; 11:35; 15:32; Mwa 21:21Baada ya hayo, watu waliondoka Haserothi, wakapiga kambi katika Jangwa la Parani.

Read More of Hesabu 12

Hesabu 13:1-25

Kupeleleza Kanaani

(Kumbukumbu 1:19-33)

Bwana akamwambia Mose, 13:2 Hes 13:16; Kum 1:22; Law 14:34; 24:11; Yos 1:3“Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi ya Kanaani, ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka kwa kila kabila la baba zao, tuma mmoja wa viongozi wao.”

13:3 Hes 14:6; 24; 34:19; Kum 1:36; Amu 1:12-15Hivyo kwa agizo la Bwana Mose akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli. Haya ndiyo majina yao:

kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri;

kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;

13:6 Hes 14:6; 24; 34:19; Kum 1:36; Amu 1:12-15; Yos 14:6kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;

kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu;

13:8 Hes 11:28kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;

kutoka kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu;

kutoka kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi,

kutoka kabila la Manase (kabila la Yosefu), Gadi mwana wa Susi;

kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali;

kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli;

kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi;

kutoka kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki.

13:16 Kum 32:44; Kut 17:9Haya ndiyo majina ya watu ambao Mose aliwatuma kuipeleleza nchi. (Mose akampa Hoshea mwana wa Nuni jina Yoshua.)

13:17 Yos 14:7; Mwa 12:9; Kum 1:7; Yos 9:1; Mwa 14:10; Kum 1:19; Amu 1:9-10Mose alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema, “Pandeni kupitia Negebu, mwende mpaka nchi ya vilima. Mwone nchi ni ya namna gani, na kama watu waishio humo wana nguvu au ni wadhaifu, iwapo ni wachache au wengi. Wanaishi katika nchi ya namna gani? Je, ni nzuri au mbaya? Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au ngome? 13:20 Kum 1:25; Law 25:5; Kum 8:7, 8; Neh 9:25-35; Eze 20:6; 34:14; Kum 31:6; Yos 1:6, 9; Ebr 13:6Ardhi iko aje? Ina rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la? Jitahidini kadiri mwezavyo kuleta baadhi ya matunda ya nchi.” (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.)

13:21 Hes 20:1; 27:14; 33:36; 34:8; Kum 32:51; Yos 15:1; 19:28; 13:5; Amu 1:31; 18:28; 2Sam 10:6; 1Nya 6:75; 13:5; 1Fal 8:65; 2Fal 14:25; 2Nya 7:8; Yer 52:7; Eze 47:16-20; Amo 6:14Hivyo wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo-Hamathi. 13:22 Hes 13:28; Mwa 13:18; 23:19; Yos 15:14; Amu 1:10; Kum 2:10; 9:2; Yos 11:21; 15:13; Za 78:12; Isa 19:11-13; 30:4; Eze 30:14Wakapanda kupitia Negebu hadi wakafika Hebroni, mahali ambapo Ahimani, Sheshai na Talmai, wazao wa Anaki, waliishi. (Hebroni ulikuwa umejengwa miaka saba kabla ya mji wa Soani ulioko Misri.) 13:23 Mwa 14:13; Kut 28:33; Mwa 3:7; Hes 20:5; Kum 8:8; 2Fal 18:31; Neh 13:15Walipofika katika Bonde la Eshkoli, walivunja tawi lililokuwa na kishada kimoja cha zabibu. Wawili wao wakalichukua lile tawi kwenye mti, pamoja na komamanga na tini. Eneo lile likaitwa Bonde la Eshkoli kwa sababu ya kile kishada cha zabibu ambacho Waisraeli walikikata huko. 13:25 Mwa 7:4; Hes 14:34Mwishoni mwa siku arobaini wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.

Read More of Hesabu 13