Nehemia 9:38, Nehemia 10:1-39, Nehemia 11:1-21 NEN

Nehemia 9:38

Mapatano Ya Watu

9:38 2Nya 23:16; Isa 44:5“Kwa sababu ya haya yote, tunajifunga katika mapatano, na kuyaandika, nao viongozi wetu, Walawi wetu na makuhani wetu wanatia mihuri yao.”

Read More of Nehemia 9

Nehemia 10:1-39

10:1 Neh 8:9; 1:1Wale waliotia muhuri walikuwa:

Nehemia mtawala, mwana wa Hakalia.

Sedekia, 10:2 Ezr 2:2Seraya, Azaria, Yeremia,

10:3 1Nya 9:12Pashuri, Amaria, Malkiya,

Hatushi, Shebania, Maluki,

10:5 1Nya 24:8Harimu, Meremothi, Obadia,

Danieli, Ginethoni, Baruku,

Meshulamu, Abiya, Miyamini,

10:8 Neh 12:1Maazia, Bilgai na Shemaya.

Hawa ndio waliokuwa makuhani.

10:9 Neh 12:8Walawi:

Yeshua mwana wa Azania, Binui wa wana wa Henadadi, Kadmieli,

na wenzao: Shebania,

Hodia, Kelita, Pelaya, Hanani,

Mika, Rehobu, Hashabia,

Zakuri, Sherebia, Shebania,

Hodia, Bani na Beninu.

Viongozi wa watu:

Paroshi, Pahath-Moabu, Elamu, Zatu, Bani,

Buni, Azgadi, Bebai,

10:16 Ezr 8:6Adoniya, Bigwai, Adini,

Ateri, Hezekia, Azuri,

Hodia, Hashumu, Besai,

Harifu, Anathothi, Nebai,

10:20 1Nya 24:15Magpiashi, Meshulamu, Heziri,

Meshezabeli, Sadoki, Yadua,

Pelatia, Hanani, Anaya,

Hoshea, Hanania, Hashubu,

Haloheshi, Pilha, Shobeki,

Rehumu, Hashabna, Maaseya,

Ahiya, Hanani, Anani,

Maluki, Harimu na Baana.

10:28 Za 135:1; 1Nya 6:26; Neh 9:2; 13:3“Watu wengine wote, wakiwa ni makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, watumishi wa Hekalu,10:28 Yaani Wanethini. na wale wote waliojitenga na mataifa jirani kwa ajili ya Sheria ya Mungu, pamoja na wake zao na wana wao na binti zao wote waliokuwa na uwezo wa kufahamu, 10:29 Hes 5:21; Neh 5:12; Kum 29:12basi hawa wote wanajiunga na ndugu zao na wakuu wao, na kujifunga kwa laana na kwa kiapo kufuata Sheria ya Mungu iliyotolewa kupitia kwa Mose mtumishi wa Mungu, na kutii kwa uangalifu amri zote, maagizo na sheria za Bwana, Bwana wetu.

10:30 Kut 34:16; Kum 7:3; Mwa 6:2“Tunaahidi kutowaoza binti zetu kwa watu wanaotuzunguka, wala kuwaoza wana wetu binti zao.

10:31 Eze 23:38; Amo 8:5; Neh 8:5; 13:15; Kut 23:11; Kum 15:1; Law 25:1-7“Wakati mataifa jirani waletapo bidhaa zao au nafaka kuuza siku ya Sabato, hatutazinunua kutoka kwao siku ya Sabato, wala siku nyingine yoyote takatifu. Kila mwaka wa saba, tutaacha kuilima ardhi na tutafuta madeni yote.

10:32 Mwa 28:22“Tunakubali wajibu wa kutimiza amri za kutoa theluthi ya shekeli10:32 Theluthi ya shekeli hapa kama gramu 4. kila mwaka kwa ajili ya utumishi wa nyumba ya Mungu: 10:33 Law 24:5-6; Hes 10:10; Za 81:3; 2Nya 24:5Kwa ajili ya mikate ya Wonyesho, kwa ajili ya sadaka za kawaida za nafaka na sadaka za kuteketezwa, kwa ajili ya sadaka za siku za Sabato, Sikukuu za Mwandamo wa Mwezi na sikukuu nyingine zilizoamriwa, kwa ajili ya sadaka takatifu, kwa ajili ya sadaka za dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, na kwa ajili ya kazi zote za nyumba ya Mungu wetu.

10:34 Neh 13:31; Law 6:12; 16:8“Sisi makuhani, Walawi na watu, tumepiga kura kuamua kuwa kila mmoja wa jamaa zetu lazima alete katika nyumba ya Mungu wetu kwa nyakati maalum kila mwaka mchango wa kuni za kukokea moto katika madhabahu ya Bwana Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika Sheria.

10:35 Kut 23:19; Hes 18:12; Kum 26:2“Pia tunachukua wajibu wa kuleta malimbuko ya mazao yetu na matunda ya kwanza ya kila mti wa matunda katika nyumba ya Bwana kila mwaka.

10:36 Kut 13:2-12; Hes 18:14-16; Law 27:26-27“Kama pia ilivyoandikwa katika Sheria, tutawaleta wazaliwa wetu wa kwanza wa kiume, na wa mifugo yetu, yaani wa ngʼombe wetu na wa makundi yetu ya kondoo na mbuzi, katika nyumba ya Mungu wetu, kwa ajili ya makuhani wanaohudumu huko.

10:37 Law 23:17; Hes 15:19; Law 27:30; Hes 18:21; Kum 14:22-29“Zaidi ya hayo, tutaleta katika ghala za nyumba ya Mungu wetu, kwa makuhani, vyakula vya kwanza vya mashamba yetu, sadaka zetu za nafaka, matunda ya miti yetu yote, divai yetu mpya na mafuta. Nasi tutaleta zaka za mazao yetu kwa Walawi, kwa kuwa Walawi ndio ambao hukusanya zaka katika miji yote tunakofanya kazi. 10:38 Hes 18:26; 2Nya 31:11Kuhani atokanaye na uzao wa Aroni atashirikiana na Walawi wakati wanapopokea zaka, nao Walawi itawapasa kuleta sehemu ya kumi ya zaka katika nyumba ya Mungu wetu katika ghala za hazina. 10:39 Neh 13:10-12; Kum 12:6; Mt 18:20Watu wa Israeli pamoja na Walawi itawapasa kuleta michango yao ya nafaka, divai mpya na mafuta katika vyumba vya ghala, mahali vifaa vya mahali patakatifu vinapohifadhiwa, na wanapokaa makuhani wanaohudumu, na mabawabu na waimbaji.

“Hatutaacha kuijali nyumba ya Mungu wetu.”

Read More of Nehemia 10

Nehemia 11:1-21

Wakazi Wapya Wa Yerusalemu

11:1 Isa 48:2; Neh 7:4; Isa 64:10; Zek 14:20-21Basi viongozi wa watu walikaa Yerusalemu, nao watu wale wengine walipiga kura ili kuleta mtu mmoja kati ya watu kumi aje kuishi Yerusalemu, mji mtakatifu, nao wengine tisa waliobaki wakae katika miji yao wenyewe. 11:2 Amu 5:9Watu waliwasifu wale wote waliojitolea kuishi Yerusalemu.

11:3 1Nya 9:29; Ezr 2:44-45Hawa ndio viongozi wa majimbo waliokuja kuishi Yerusalemu (baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi, watumishi wa Hekalu,11:3 Yaani Wanethini (pia 11:21). na wazao wa watumishi wa Solomoni waliendelea kuishi katika miji ya Yuda, kila mmoja katika milki yake mwenyewe katika miji mbalimbali, 11:4 Ezr 1:5; Mwa 38:29; Ezr 2:70; 1Nya 9:3ambapo watu wengine kutoka Yuda na Benyamini waliishi Yerusalemu).

Kutoka wazao wa Yuda:

Athaya mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli, mzao wa Peresi. Naye Maaseya mwana wa Baruku, mwana wa Kolhoze, mwana wa Hazaya, mwana wa Adaya, mwana wa Yoyaribu, mwana wa Zekaria, mzao wa Mshiloni. Wazao wa Peresi walioishi Yerusalemu walikuwa 468, watu wenye uwezo.

Kutoka wazao wa Benyamini:

Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Yoedi, mwana wa Pedaya, mwana wa Kolaya, mwana wa Maaseya, mwana wa Ithieli, mwana wa Yeshaya na wafuasi wake, Gabai na Salai watu 928. Yoeli mwana wa Zikri alikuwa afisa wao mkuu, naye Yuda mwana wa Hasenua alikuwa msimamizi juu ya Mtaa wa Pili katika mji.

11:10 1Nya 9:10Kutoka makuhani:

Yedaya, mwana wa Yoyaribu, Yakini, 11:11 2Fal 25:18; Ezr 7:2Seraya mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, msimamizi katika nyumba ya Mungu, pamoja na wenzao waliofanya kazi hekaluni: watu 822. Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia, mwana wa Amsi, mwana wa Zekaria, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya, na wenzao, waliokuwa viongozi wa jamaa: watu 242. Amashisai mwana wa Azareli, mwana wa Azai, mwana wa Meshilemothi, mwana wa Imeri, na wenzao waliokuwa wenye uwezo: watu 128. Afisa wao mkuu alikuwa Zabdieli mwana wa Hagedolimu.

Kutoka Walawi:

Shemaya mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, mwana wa Buni; 11:16 Ezr 10:15; 2Nya 34:13; Ezr 8:33Shabethai na Yozabadi, viongozi wawili wa Walawi, ambao walisimamia kazi za nje za nyumba ya Mungu; 11:17 1Nya 9:15; Neh 12:8; 2Nya 5:12Matania mwana wa Mika, mwana wa Zabdi, mwana wa Asafu, kiongozi aliyeongoza kutoa shukrani na maombi; Bakbukia aliyekuwa msaidizi wake kati ya wenzake; na Abda mwana wa Shamua, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni. 11:18 Ufu 21:2; Ezr 9:8; Mt 24:15Jumla ya Walawi waliokaa katika mji mtakatifu walikuwa watu 284.

11:19 1Nya 9:17; Neh 7:45; 12:25Mabawabu:

Akubu, Talmoni na wenzao, waliolinda malango: watu 172.

Waisraeli waliosalia, pamoja na makuhani na Walawi, walikuwa katika miji yote ya Yuda, kila mmoja katika urithi wa baba yake.

11:21 Ezr 2:43; Neh 3:26; 2Nya 27:3Watumishi wa Hekalu waliishi katika kilima cha Ofeli. Siha na Gishpa walikuwa wasimamizi wao.

Read More of Nehemia 11