Nehemia 7:4-73, Nehemia 8:1-18 NEN

Nehemia 7:4-73

Orodha Ya Waliorudi Toka Uhamishoni

(Ezra 2:1-70)

7:4 Mit 1:10; Neh 11:1Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu. 7:5 Mit 2:6; Rum 11:36; 1Kor 4:7; 2Kor 8:16; Yak 1:17; Ezr 2:1-70Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:

7:6 Ezr 2:1-10; 2Nya 36:20Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 7:7 1Nya 3:19; Ezr 2:2wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana):

Orodha ya wanaume wa Israeli ilikuwa:

7:8 Ay 13:4; Dan 11:27wazao wa Paroshi 2,172wazao wa Shefatia 372wazao wa Ara 652wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,818wazao wa Elamu 1,254wazao wa Zatu 845wazao wa Zakai 760wazao wa Binui 648wazao wa Bebai 628wazao wa Azgadi 2,322wazao wa Adonikamu 667wazao wa Bigwai 2,0677:20 Ezr 8:6wazao wa Adini 655wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98wazao wa Hashumu 328wazao wa Besai 324wazao wa Harifu 112wazao wa Gibeoni 95

7:26 2Sam 23:28; Mwa 35:6; Rut 2; 4watu wa Bethlehemu na Netofa 1887:27 Yos 21:18; Ezr 2:23watu wa Anathothi 128watu wa Beth-Azmawethi 427:29 Yos 18:25-26watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743watu wa Rama na Geba 6217:31 1Sam 13:2; Isa 10:27watu wa Mikmashi 1227:32 Mwa 12:8watu wa Betheli na Ai 123watu wa Nebo 52wazao wa Elamu 1,254wazao wa Harimu 3207:36 Neh 3:2wazao wa Yeriko 3457:37 1Nya 8:12wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 721wazao wa Senaa 3,930

7:39 1Nya 24:7Makuhani:

wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 9737:40 1Nya 24:14wazao wa Imeri 1,0527:41 1Nya 9:12; 24:9wazao wa Pashuri 1,2477:42 1Nya 24:8; Ezr 10:31wazao wa Harimu 1,017

Walawi:

wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia jamaa ya Hodavia) 74

7:44 Neh 11:23Waimbaji:

wazao wa Asafu 148

7:45 1Nya 9:17Mabawabu wa malango:

wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai 138

7:46 Neh 3:26Watumishi wa Hekalu:7:46 Yaani Wanethini (pia 7:60, 73).

wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,

wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,

wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,

wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,

wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,

wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,

wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,

wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,

wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,

wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,

wazao wa Nesia na Hatifa.

7:57 Mwa 9:25, 26; 1Fal 5:13, 14; 2Nya 2:17, 18Wazao wa watumishi wa Solomoni:

wazao wa Sotai, Soferethi, Perida,

wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,

wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Amoni.

7:60 1Nya 9:2Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni 392

7:61 Ezr 2:59Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:

wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda 642

7:63 2Sam 17:27; 19:31-34; 1Fal 2:7; Ezr 2:61Na kutoka miongoni mwa makuhani:

wazao wa Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).

Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 7:65 Kut 28:30; Neh 8:9; Hes 7:89; 27:18-21Kwa hiyo, mtawala7:65 Au Tirshatha: jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi (pia 7:70). aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.7:65 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.

Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 245. Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245 ngamia 435 na punda 6,720.

7:70 Neh 8:9; 10:1Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,0007:70 Darkoni 1,000 za dhahabu ni sawa na uzito wa kilo 8.6. za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani. 7:71 1Nya 29:7; Ezr 2:69Baadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni 20,000 za dhahabu,7:71 Darkoni 20,000 za dhahabu ni sawa na kilo 172. na mane 2,2007:71 Mane 2,200 za fedha ni sawa na kilo 1,300. za fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

7:72 Ay 34:10; Kut 25:2Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.

7:73 Za 34:20; Neh 11:20; Kut 23:14-17; Law 23:24-44; Ezr 3:1Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe.

Ezra Asoma Sheria

Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,

Read More of Nehemia 7

Nehemia 8:1-18

8:1 Neh 3:28; Ezr 7:6; 2Nya 34:15; Neh 3:26; Kum 28:61; 2Nya 34:15watu wote wakakusanyika kama mtu mmoja kwenye uwanja mbele ya Lango la Maji. Wakamwambia Ezra mwandishi alete Kitabu cha Sheria ya Mose, ambacho Bwana aliamuru kwa ajili ya Israeli.

8:2 Law 23:23-25; Hes 29:1-6; Kum 31:11Basi katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba, kuhani Ezra akaleta Sheria mbele ya kusanyiko, ambamo walikuwamo wanaume, wanawake na watu wote walioweza kufahamu. 8:3 Neh 3:26Akaisoma kwa sauti kubwa tangu mapambazuko mpaka adhuhuri, akiwa ameuelekea uwanja uliokuwa mbele ya Lango la Maji mbele ya wanaume, wanawake na wengine ambao waliweza kufahamu. Watu wote wakasikiliza kwa makini kile Kitabu cha Sheria.

8:4 2Nya 6:13Mwandishi Ezra alikuwa amesimama juu ya jukwaa la miti lililojengwa kwa kusudi hilo. Karibu naye upande wa kuume alisimama Matithia, Shema, Anaya, Uria, Hilkia na Maaseya. Upande wake wa kushoto walikuwepo Pedaya, Mishaeli, Malkiya, Hashumu, Hashbadani, Zekaria na Meshulamu.

8:5 Amu 3:20Ezra akakifungua kile kitabu. Watu wote waliweza kumwona kwa sababu alikuwa amesimama juu zaidi, naye alipokifungua watu wote wakasimama. 8:6 Kut 4:31; Hes 5:22; Neh 5:13; 1Tim 2:8; Ezr 9:5; 1Tim 2:8Ezra akamsifu Bwana, Mungu mkuu, nao watu wote wakainua mikono yao na kuitikia, “Amen! Amen!” Kisha wakasujudu na kumwabudu Bwana hali nyuso zao zikigusa ardhi.

8:7 Ezr 10:23; Law 10:11; 2Nya 17:1Watu wakiwa wamesimama pale, Walawi wafuatao waliwafunza ile Sheria: Yeshua, Bani, Sherebia, Yamini, Akubu, Shabethai, Hodia, Maaseya, Kelita, Azaria, Yozabadi, Hanani na Pelaya. 8:8 Hab 2:2; Mdo 8:30-35Walisoma kutoka kile Kitabu cha Sheria ya Mungu, wakiifafanua na kuwapa maelezo ili watu waweze kufahamu kile kilichokuwa kikisomwa.

8:9 Ezr 2:63; Neh 7:65; Kum 12:7-12; 16:14-15Ndipo Nehemia aliyekuwa mtawala,8:9 Au Tirshatha: jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi. Ezra kuhani na mwandishi, pamoja na Walawi waliokuwa wakiwafundisha watu wakawaambia wote, “Siku hii ni takatifu kwa Bwana Mungu wenu. Msiomboleze wala msilie.” Kwa kuwa watu wote walikuwa wakilia walipokuwa wakisikiliza maneno ya ile Sheria.

8:10 Es 9:22; Lk 14:12-14; Law 23:40; Kum 12:18Nehemia akasema, “Nendeni mkafurahie chakula kizuri na vinywaji vitamu, na mpeleke sehemu kwa wale ambao hawana chochote cha kula. Siku hii ni takatifu kwa Bwana. Msihuzunike, kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.”

Walawi wakawatuliza watu wote wakisema, “Kuweni watulivu, kwa kuwa hii ni siku takatifu. Msihuzunike.”

8:12 Es 9:22Kisha watu wote wakaondoka kwenda kula na kunywa, na kupeana sehemu ya chakula, na wakaadhimisha kwa furaha kubwa, kwa sababu sasa walifahamu maneno yale waliyokuwa wameelezwa.

Katika siku ya pili ya mwezi, wakuu wa mbari zote, pamoja na makuhani na Walawi, walikusanyika wakimzunguka Ezra mwandishi ili wapate kusikiliza kwa makini maneno ya Sheria. 8:14 Mwa 33:17; Law 23:34Wakakuta imeandikwa katika ile Sheria, ambayo Bwana aliiamuru kupitia kwa Mose, kwamba Waisraeli walipaswa kukaa katika vibanda wakati wa sikukuu ya mwezi wa saba, 8:15 Law 23:4; Kum 16:16; Law 23:40na kwamba walipaswa kutangaza neno hili na kulieneza katika miji yao na katika Yerusalemu wakisema: “Enendeni katika nchi ya mlima na kuleta matawi kutoka miti ya mizeituni, mizeituni mwitu, mihadasi, mitende na miti ya kivuli, ili kutengeneza vibanda,” kama ilivyoandikwa.

8:16 Kum 22:3; 2Fal 14:13; 2Nya 25:23Basi watu wakaenda na kuleta matawi, nao wakajijengea vibanda juu ya paa za nyumba zao, katika nyua zao, katika nyua za nyumba ya Mungu, na katika uwanja karibu na Lango la Maji na uwanja wa Lango la Efraimu. 8:17 1Fal 8:2; 2Nya 7:8Jamii yote ya watu waliorudi kutoka utumwani wakajenga vibanda na kuishi ndani yake. Tangu wakati wa Yoshua mwana wa Nuni mpaka siku ile, Waisraeli hawakuwahi kuiadhimisha namna hii. Furaha yao ilikuwa kubwa sana.

8:18 Kum 33:10; Hes 29:35; Law 23:36Siku baada ya siku, kuanzia siku ya kwanza hadi ya mwisho, Ezra alisoma kutoka kwenye kile Kitabu cha Sheria ya Mungu. Wakaiadhimisha sikukuu ile kwa siku saba, nayo siku ya nane, kufuatana na maagizo, kulikuwa na kusanyiko maalum.

Read More of Nehemia 8