Nehemia 11:22-36, Nehemia 12:1-47 NEN

Nehemia 11:22-36

11:22 1Nya 9:15Afisa mkuu wa Walawi huko Yerusalemu alikuwa Uzi mwana wa Bani, mwana wa Hashabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika. Uzi alikuwa mmoja wa wazao wa Asafu, waliokuwa waimbaji wenye kuwajibika kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu. 11:23 1Nya 15:16; Neh 7:44Waimbaji walikuwa chini ya amri za mfalme, ambazo pia ziliratibu shughuli zao za kila siku.

11:24 Mwa 38:30; 1Nya 23:28Pethahia mwana wa Meshezabeli, mmoja wa wazao wa Zera mwana wa Yuda, alikuwa mwakilishi wa mfalme katika mambo yote kuhusu mahusiano na watu.

11:25 Mwa 35:27; Yos 14:15; Hes 21:30Kuhusu vijiji na mashamba yake, baadhi ya watu wa Yuda waliishi Kiriath-Arba na makazi yaliyokizunguka, katika Diboni na makazi yake, katika Yekabzeeli na vijiji vyake, 11:26 Yos 15:27katika Yeshua, katika Molada, katika Beth-Peleti, 11:27 Mwa 21:14katika Hasar-Shuali, katika Beer-Sheba na makazi yake, 11:28 Isa 27:6katika Siklagi, katika Mekona na makazi yake, 11:29 Yos 15:33-35; Yer 10:3katika En-Rimoni, katika Sora, katika Yarmuthi, 11:30 Yos 10:39; 10:10; 15:28Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, katika Lakishi na mashamba yake, na katika Azeka na makazi yake. Hivyo walikuwa wakiishi kuanzia Beer-Sheba mpaka Bonde la Hinomu.

11:31 Yos 21:17; Isa 10:29; 1Sam 13:2Wazao wa Wabenyamini kutoka Geba waliishi Mikmashi, Aiya, Betheli na makazi yake, 11:32 Isa 10:30; 1Sam 21:1katika Anathothi, Nobu na Anania, 11:33 Yos 11:1; 18:25; 2Sam 4:3katika Hazori, Rama na Gitaimu, 11:34 1Sam 13:18katika Hadidi, Seboimu na Nebalati, 11:35 1Nya 8:12; 4:14katika Lodi na Ono, na katika Bonde la Mafundi.

Baadhi ya makundi ya Walawi wa Yuda waliishi huko Benyamini.

Read More of Nehemia 11

Nehemia 12:1-47

Makuhani Na Walawi Waliorudi Na Zerubabeli

12:1 Neh 10:2-8; Zek 4:6-10; Ezr 3:2Hawa wafuatao walikuwa makuhani na Walawi ambao walirudi na Zerubabeli mwana wa Shealtieli pamoja na Yeshua:

Seraya, Yeremia, Ezra,

Amaria, Maluki, Hatushi,

Shekania, Rehumu, Meremothi,

12:4 Lk 1:5; 1Nya 24:10Ido, Ginethoni, Abiya,

Miyamini, Moadia, Bilga,

12:6 1Nya 24:7Shemaya, Yoyaribu, Yedaya,

12:7 Hag 1:1; Zek 5:1; Ezr 3:2Salu, Amoki, Hilkia na Yedaya.

Hawa walikuwa viongozi wa makuhani na wenzao wakati wa Yeshua.

12:8 Neh 11:17; 1Nya 16:8Walawi walikuwa Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na pia Matania, ambaye pamoja na wenzake, alikuwa kiongozi wa nyimbo za shukrani. Bakbukia na Uni, wenzao, walisimama mkabala nao wakati wa ibada.

12:10 Ezr 10:24; Neh 3:20Yeshua alikuwa baba wa Yoyakimu, Yoyakimu alikuwa baba wa Eliashibu, Eliashibu alikuwa baba wa Yoyada, Yoyada alikuwa baba wa Yonathani, na Yonathani alikuwa baba wa Yadua.

Katika siku za Yoyakimu, kulikuwa na wakuu wa jamaa za kikuhani:

wa jamaa ya Seraya, Meraya;

wa jamaa ya Yeremia, Hanania;

wa jamaa ya Ezra, Meshulamu;

wa jamaa ya Amaria, Yehohanani;

wa jamaa ya Maluki, Yonathani;

wa jamaa ya Shebania, Yosefu;

wa jamaa ya Harimu, Adna;

wa jamaa ya Meremothi, Helkai;

12:16 Neh 12:4wa jamaa ya Ido, Zekaria;

wa jamaa ya Ginethoni, Meshulamu;

12:17 1Nya 24:10wa jamaa ya Abiya, Zikri;

wa jamaa ya Miniamini na ya Maazia, Piltai;

wa jamaa ya Bilgai, Shamua;

wa jamaa ya Shemaya, Yehonathani;

wa jamaa ya Yoyaribu, Matenai;

wa jamaa ya Yedaya, Uzi;

wa jamaa ya Salu, Kalai;

wa jamaa ya Amoki, Eberi;

wa jamaa ya Hilkia, Hashabia;

wa jamaa ya Yedaya, Nethaneli.

Wakuu wa jamaa za Walawi katika siku za Eliashibu, Yoyada, Yohanani na Yadua, pia wale jamaa za makuhani, waliandikishwa wakati wa utawala wa Dario, Mwajemi. 12:23 1Nya 9:14Wakuu wa jamaa miongoni mwa wazao wa Lawi hadi wakati wa Yohanani mwana wa Eliashibu waliandikishwa katika kitabu cha kumbukumbu. 12:24 Ezr 2:40; 3:11; 1Nya 23:1Viongozi wa Walawi walikuwa: Hashabia, Sherebia, Yeshua mwana wa Kadmieli na wenzao, waliosimama mkabala nao kusifu na kushukuru, sehemu moja ikipokezana na nyingine kama ilivyoagizwa na Daudi mtu wa Mungu.

Mabawabu waliokuwa wakilinda kwenye malango ya ghala ni: Matania, Bakbukia, Obadia, Meshulamu, Talmoni na Akubu. 12:26 Neh 8:9; Ezr 7:6, 11Walihudumu siku za Yoyakimu mwana wa Yeshua, mwana wa Yosadaki, na katika siku za mtawala Nehemia, na za Ezra kuhani na mwandishi.

Kuwekwa Wakfu Ukuta Wa Yerusalemu

12:27 Kum 20:5; 2Sam 6:5; 1Nya 25:6; Za 81:1-3; 92:3Wakati wa kuwekwa wakfu ukuta wa Yerusalemu, Walawi walitafutwa kule walikokuwa wakiishi, nao wakaletwa Yerusalemu kuadhimisha kwa shangwe huko kuweka wakfu kwa nyimbo za shukrani na kwa uimbaji wakitumia matoazi, vinubi na zeze. 12:28 1Nya 2:54; 9:16Pia waimbaji walikusanywa pamoja kutoka maeneo yaliyozunguka Yerusalemu, kutoka vijiji vya Wanetofathi, kutoka Beth-Gilgali, na kutoka eneo la Geba na Azmawethi, kwa kuwa waimbaji walikuwa wamejijengea vijiji kuzunguka Yerusalemu. 12:30 Kut 19:10; Ay 1:5Wakati makuhani na Walawi walipokuwa wamekwisha kujitakasa kwa kufuatana na desturi, waliwatakasa watu, malango na ukuta.

12:31 Neh 2:13; Ezr 3:10; Hes 10:2; 2Nya 5:12Niliwaagiza viongozi wa Yuda wapande juu ya ukuta. Pia niliagiza makundi mawili makubwa ya waimbaji waimbe nyimbo za kumshukuru Mungu. Kundi moja lilipanda juu ya ukuta upande wa kuume, kuelekea Lango la Samadi. Hoshaya na nusu ya viongozi wa Yuda wakawafuata, pamoja na Azaria, Ezra, Meshulamu, 12:34 Ezr 1:5Yuda, Benyamini, Shemaya, Yeremia, 12:35 Ezr 3:10pamoja na baadhi ya makuhani wenye tarumbeta, na pia walikuwa na Zekaria mwana wa Yonathani, mwana wa Shemaya, mwana wa Matania, mwana wa Mikaya, mwana wa Zakuri, mwana wa Asafu, 12:36 1Nya 23:5; 15:16; 2Nya 8:14pamoja na wenzake, Shemaya, Azareli, Milalai, Gilalai, Maai, Nethaneli, Yuda na Hanani, wakiwa na vyombo vya uimbaji, kama ilivyoagizwa na Daudi mtu wa Mungu. Mwandishi Ezra aliongoza maandamano. 12:37 Neh 2:14; 3:3-15; 3:26; 2Sam 5:7-9Kwenye Lango la Chemchemi waliendelea moja kwa moja mpaka kwenye ngazi za Mji wa Daudi, kwenye mwinuko wa ukuta, na kupitia juu ya nyumba ya Daudi mpaka kwenye Lango la Maji upande wa mashariki.

12:38 Neh 3:8-11Kundi la pili la waimbaji lilielekea upande wa kushoto. Niliwafuata juu ya ukuta, pamoja na nusu ya watu kupitia Mnara wa Tanuru mpaka kwenye Ukuta Mpana, 12:39 2Fal 14:13; Neh 8:16; 2Nya 33:14; Neh 3:1-6juu ya Lango la Efraimu, Lango la Yeshana, Lango la Samaki, Mnara wa Hananeli, na Mnara wa Mia, mpaka kwenye Lango la Kondoo. Walipofika kwenye Lango la Ulinzi wakasimama.

12:40 Za 42:4Kisha yale makundi mawili ya waimbaji yaliyoshukuru yakachukua nafasi zao katika nyumba ya Mungu. Nami pia nikafanya hivyo, pamoja na nusu ya maafisa, na makuhani wafuatao: Eliakimu, Maaseya, Miniamini, Mikaya, Elioenai, Zekaria na Hanania wakiwa na tarumbeta zao, na pia Maaseya, Shemaya, Eleazari, Uzi, Yehohanani, Malkiya, Elamu na Ezeri. Makundi haya yaliimba chini ya uongozi wa Yezrahia. 12:43 Za 9:2; 92:4Siku hiyo watu walitoa dhabihu nyingi, wakishangilia kwa sababu Mungu aliwapa furaha kuu. Wanawake na watoto walishangilia pia. Sauti ya kushangilia huko Yerusalemu iliweza kusikika mbali sana.

12:44 Neh 13:4, 13; Law 27:30; Kum 18:8Wakati huo watu walichaguliwa kuwa wasimamizi wa vyumba vya ghala kwa ajili ya matoleo, malimbuko na zaka. Kutoka kwenye yale mashamba yaliyozunguka miji walipaswa walete kwenye ghala mafungu kama sheria ilivyoamuru kwa ajili ya makuhani na Walawi, kwa kuwa Yuda alifurahishwa na huduma ya makuhani na Walawi. 12:45 1Nya 25:1; 2Nya 8:14; 1Nya 6:31; 23:5Walifanya ibada ya Mungu wao na ibada ya utakaso, nao waimbaji na walinzi wa lango wakafanya hivyo pia, kufuatana na amri za Daudi na Solomoni mwanawe. 12:46 2Nya 35:15; 29:27Muda mrefu uliopita, katika siku za Daudi na Asafu, walikuwepo viongozi wa waimbaji na wa nyimbo za sifa na za kumshukuru Mungu. 12:47 Hes 18:21; Kum 18:8Kwa hiyo katika siku za Zerubabeli na za Nehemia, Israeli wote walitoa mafungu kila siku kwa ajili ya waimbaji na mabawabu. Pia walitenga fungu kwa ajili ya Walawi wengine, nao Walawi walitenga fungu kwa ajili ya wazao wa Aroni.

Read More of Nehemia 12