Nehemia 1:1-11, Nehemia 2:1-20 NEN

Nehemia 1:1-11

Maombi Ya Nehemia

1:1 Neh 10:1; Ezr 7:8; Zek 7:1; Dan 8:2; Neh 2:1; Es 1:2Maneno ya Nehemia mwana wa Hakalia:

Katika mwezi wa Kisleu1:1 Kisleu ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiyahudi; katika kalenda yetu ni Novemba/Desemba (ona pia Zekaria 7:1). katika mwaka wa ishirini, wakati nilikuwa ngomeni katika jumba la kifalme la Shushani, 1:2 Neh 7:2; 2Fal 21:4; Neh 7:6; Yer 52:28Hanani, mmoja wa ndugu zangu, alikuja kutoka Yuda akiwa na watu wengine, nami nikawauliza kuhusu mabaki ya Wayahudi wale walionusurika kwenda uhamishoni na pia kuhusu Yerusalemu.

1:3 Law 26:31; Mao 2:9; Yer 5:10; Law 26:31; 2Fal 25:10; Neh 2:3, 13, 17; Isa 22:9Wakaniambia, “Wale walionusurika kwenda uhamishoni, wale ambao wamerudi kwenye lile jimbo, wako katika taabu kubwa na aibu. Ukuta wa Yerusalemu umebomoka, na malango yake yamechomwa moto.”

1:4 Za 137:1; 2Nya 20:3; Ezr 9:4; Dan 9:3Niliposikia mambo haya, niliketi, nikalia. Kwa siku kadhaa niliomboleza na kufunga na kuomba mbele za Mungu wa mbinguni. 1:5 Kum 7:21; Neh 4:14; Kum 7:9; 1Fal 8:23; Ebr 6:13-18Kisha nikasema:

“Ee Bwana, Mungu wa mbinguni, mkuu na mwenye kuogofya, ambaye hulishika agano lake la upendo na wale wampendao na kutii amri zake, 1:6 2Nya 7:15; 1Fal 8:30; 2Nya 6:40; 1Fal 8:47tega masikio yako, na ufungue macho yako, ili usikie maombi ya mtumishi wako anayoomba mbele yako usiku na mchana kwa ajili ya watumishi wako, watu wa Israeli. Ninaungama dhambi zetu sisi Waisraeli, pamoja na zangu na za nyumba ya baba yangu, tulizotenda dhidi yako. 1:7 Kum 28:14-15; Za 106:6Tumetenda uovu sana mbele zako. Hatukutii amri, maagizo na sheria ulizompa Mose mtumishi wako.

1:8 Mwa 8:1; Law 26:33; Kum 4:25“Kumbuka agizo ulilompa Mose mtumishi wako, ukisema, ‘Kama mkikosa uaminifu, nitawatawanya miongoni mwa mataifa, 1:9 Kum 30:4; Eze 20:34-38; Mik 2:12lakini mkinirudia na kutii amri zangu, ndipo hata kama watu wenu walio uhamishoni wako mbali sana katika miisho ya dunia, nitawakusanya kutoka huko na kuwaleta mahali ambapo nimepachagua kuwa makao kwa ajili ya Jina langu.’

1:10 Kum 9:29; Isa 51:9-11; Dan 9:15“Hawa ni watumishi wako na watu wako, uliowakomboa kwa nguvu zako kuu na mkono wako wenye nguvu. 1:11 2Nya 6:40; Mwa 40:1; 32:11; Isa 26:8Ee Bwana, tega sikio lako na usikie maombi ya huyu mtumishi wako, na maombi ya watumishi wako wanaofurahia kuliheshimu Jina lako. Nipe leo, mimi mtumishi wako, mafanikio kwa kunipa kibali mbele ya mtu huyu.”

Kwa maana nilikuwa mnyweshaji wa mfalme.

Read More of Nehemia 1

Nehemia 2:1-20

Artashasta Amtuma Nehemia Yerusalemu

2:1 Ezr 4:7; 7:1Katika mwezi wa Nisani2:1 Nisani (Abibu) ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiyunani; katika kalenda yetu ni Machi/Aprili. mwaka wa ishirini wa utawala wa Mfalme Artashasta, wakati divai ilipoletwa kwake, niliichukua na kumpa mfalme. Sikuwahi kuonekana mwenye huzuni mbele yake kabla ya hapo. 2:2 Mit 15:13Basi mfalme akaniuliza, “Kwa nini uso wako unaonekana una huzuni wakati wewe si mgonjwa? Jambo hili si kitu kingine bali ni huzuni ya moyo.”

Niliogopa sana, 2:3 1Fal 1:13; Dan 3:9; 5:10; Za 137:6lakini nikamwambia mfalme, “Mfalme na aishi milele! Kwa nini uso wangu usiwe na huzuni wakati mji walipozikwa baba zangu umebaki magofu, na malango yake yameteketezwa kwa moto?”

2:4 1Sam 1:13; Mit 3:6Mfalme akaniambia, “Je, haja yako ni gani?”

Ndipo nikaomba kwa Mungu wa mbinguni, na nikamjibu mfalme, “Kama ikimpendeza mfalme, na kama mtumishi wako amepata kibali machoni pake, anitume kule mji wa Yuda, mahali baba zangu walipozikwa, ili niweze kuujenga upya.”

2:6 Neh 5:14; 13:6Kisha mfalme, na malkia akiwa ameketi karibu naye, akaniuliza, “Safari yako itachukua muda gani, nawe utarudi lini?” Ilimpendeza mfalme kunituma, kwa hiyo nikapanga muda.

2:7 Ezr 8:36Pia nikamwambia, “Kama ikimpendeza mfalme, naomba nipewe barua kwa watawala wa Ngʼambo ya Frati, ili wanipe ulinzi mpaka nifike Yuda. 2:8 Neh 3:7; Ezr 7:6; Neh 7:2; Mdo 7:10Naomba nipewe barua nipeleke kwa Asafu, mtunzaji wa msitu wa mfalme, ili anipe miti ya kutengeneza boriti kwa ajili ya malango ya ngome ya Hekalu, na ukuta wa mji, na makao yangu nitakapoishi.” Kwa kuwa mkono wenye neema wa Mungu wangu ulikuwa juu yangu, mfalme akanijalia ombi langu. 2:9 Ezr 8:22Basi nilienda kwa watawala wa Ngʼambo ya Frati na kuwapa barua za mfalme. Pia mfalme alikuwa ametuma maafisa wa jeshi na askari wapanda farasi pamoja nami.

2:10 Neh 2:10; 4:1, 7; 6:1-2, 5, 12, 14; 13:28; 4:3; 13:4-7; Es 10:3Sanbalati Mhoroni na Tobia afisa Mwamoni waliposikia juu ya jambo hili, waliudhika sana kwamba amekuja mtu kuinua ustawi wa Waisraeli.

Nehemia Akagua Kuta Za Yerusalemu

2:11 Mwa 40:13Nilienda Yerusalemu, na baada ya kukaa huko siku tatu, nikaondoka wakati wa usiku pamoja na watu wachache. Sikuwa nimemwambia mtu yeyote kile ambacho Mungu wangu alikuwa ameweka moyoni mwangu kufanya kwa ajili ya Yerusalemu. Hapakuwepo na mnyama yeyote pamoja nami isipokuwa yule niliyekuwa nimempanda.

2:13 2Nya 26:9; Neh 12:31; 3:13Nikatoka nje usiku kupitia Lango la Bondeni, kuelekea Kisima cha Joka na Lango la Samadi, nikikagua kuta za Yerusalemu zilizokuwa zimebomolewa, na malango yake yaliyokuwa yameteketezwa kwa moto. 2:14 Neh 12:37; 2Fal 18:17; 20:20Kisha nikaelekea mpaka Lango la Chemchemi na Bwawa la Mfalme, lakini hapakuwepo nafasi ya kutosha kwa ajili ya mnyama wangu kupita, 2:15 2Sam 15:23; Yer 31:40; Yn 18:1kwa hiyo nikapandia bondeni usiku nikikagua ukuta. Mwishoni nikarudi na kuingia tena kupitia Lango la Bondeni. Maafisa hawakujua nilikokwenda wala nilichokuwa nikifanya, kwa sababu mpaka sasa nilikuwa bado sijasema lolote kwa Wayahudi, wala makuhani, wala wakuu, wala maafisa, wala mtu yeyote ambaye angefanya kazi.

2:17 Za 102:16; Isa 30:13; 58:12; Eze 5:14; Neh 1:3Ndipo nilipowaambia, “Mnaona taabu tuliyo nayo: Yerusalemu imebaki magofu na malango yake yameteketezwa kwa moto. Njooni tujenge upya ukuta wa Yerusalemu, nasi hatutakuwa tena katika aibu hii.” 2:18 Ezr 5:5; 2Sam 2:7Pia niliwaambia kuhusu mkono wenye neema wa Mungu wangu uliokuwa juu yangu, na kile mfalme alichokuwa ameniambia.

Wakajibu, “Haya! Tuanze kujenga tena.” Kwa hiyo wakaanza kazi hii njema.

2:19 Neh 6:1-6; Za 44:13-16Lakini Sanbalati Mhoroni, Tobia afisa Mwamoni, na Geshemu Mwarabu waliposikia kuhusu jambo hili, walitudhihaki na kutucheka. Wakauliza, “Ni nini hiki mnachokifanya? Je, mnaasi dhidi ya mfalme?”

2:20 Ezr 4:3; Mdo 8:21; Rum 8:31Nikawajibu kwa kusema, “Mungu wa mbinguni atatufanikisha. Sisi watumishi wake tutaanza kujenga upya, lakini kwenu ninyi, hamna sehemu wala dai lolote wala kumbukumbu la haki katika Yerusalemu.”

Read More of Nehemia 2