Nahumu 1:1-15, Nahumu 2:1-13, Nahumu 3:1-19 NEN

Nahumu 1:1-15

1:1 Isa 13:1; 19:1; Yer 23:33-34; 50:18; Mwa 10:11; Nah 2:8; 3:7Neno alilosema Mungu kuhusu Ninawi. Kitabu cha maono cha Nahumu, Mwelkoshi.

Hasira Ya Mungu Dhidi Ya Ninawi

1:2 Kut 20:5; Mwa 4:24; Kum 32:41; 7:10; Za 94:1Bwana ni mwenye wivu na Mungu mlipiza kisasi;

Bwana hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu.

Bwana hulipiza kisasi juu ya watesi wake,

naye anadumisha ghadhabu yake dhidi ya adui zake.

1:3 Neh 9:17; Kut 34:7; 19:16; Za 103:8; Mik 7:18; 2Sam 22:10; Za 50:3; 104:3Bwana si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu,

Bwana hataacha kuadhibu wenye hatia.

Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani,

na mawingu ni vumbi la miguu yake.

1:4 2Sam 22:16; Kut 14:22; Isa 33:9; Yos 3:15, 16Anakemea bahari na kuikausha,

anafanya mito yote kukauka.

Bashani na Karmeli zinanyauka

na maua ya Lebanoni hukauka.

1:5 Kut 19:18; Ay 9:6; 2Sam 22:8; Yoe 2:10; Eze 38:20; Mik 1:4Milima hutikisika mbele yake

na vilima huyeyuka.

Nchi hutetemeka mbele yake,

dunia na wote waishio ndani yake.

1:6 Za 130:3; Eze 22:14; Isa 5:24-25; 42:25; Yer 10:10; 1Fal 19:11Ni nani awezaye kuzuia hasira yake yenye uchungu?

Nani awezaye kuvumilia hasira yake kali?

Ghadhabu yake imemiminwa kama moto,

na miamba inapasuka mbele zake.

1:7 Yer 33:11; 17:17; Za 22:9; 1:6; 2Tim 2:19Bwana ni Mwema,

kimbilio wakati wa taabu.

Huwatunza wale wanaomtegemea,

1:8 Isa 8:7; Amo 8:8; Dan 9:26lakini kwa mafuriko makubwa,

ataangamiza Ninawi;

atafuatilia adui zake hadi gizani.

1:9 Hos 7:15Shauri baya lolote wapangalo dhidi ya Bwana

yeye atalikomesha;

taabu haitatokea mara ya pili.

1:10 2Sam 23:6; Isa 49:26; 5:24; Mal 4:1Watasongwa katikati ya miiba

na kulewa kwa mvinyo wao.

Watateketezwa kama mabua makavu.

Ee Ninawi, kutoka kwako amejitokeza mmoja,

ambaye anapanga shauri baya

dhidi ya Bwana

na kushauri uovu.

1:12 Isa 10:34; 54:6-8; Mao 3:31-32Hili ndilo asemalo Bwana:

“Ingawa wana muungano nao ni wengi sana,

watakatiliwa mbali na kuangamia.

Ingawa nimekutesa wewe, ee Yuda,

sitakutesa tena.

1:13 Isa 9:4; Ay 12:18; Za 107:14Sasa nitavunja nira zao kutoka shingo yako,

nami nitazivunjilia mbali pingu zako.”

1:14 Isa 14:22; Mik 5:13; Yer 28:8; Eze 32:22-23Hii ndiyo amri Bwana aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi:

“Hutakuwa na wazao

watakaoendeleza jina lako.

Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kuyeyusha

ambazo zipo katika hekalu la miungu yenu.

Nitaandaa kaburi lako,

kwa maana wewe ni mwovu kabisa.”

1:15 Isa 40:9; Rum 10:15; Isa 52:7; Mdo 10:36; Law 23:2-4Tazama, huko juu milimani,

miguu ya huyo mmoja aletaye habari njema,

ambaye anatangaza amani!

Ee Yuda, sherehekea sikukuu zako,

nawe utimize nadhiri zako.

Waovu hawatakuvamia tena;

wataangamizwa kabisa.

Read More of Nahumu 1

Nahumu 2:1-13

Ninawi Kuanguka

2:1 Yer 51:20Mshambuliaji anasogea dhidi yako, Ninawi.

Linda ngome,

chunga barabara,

jitieni nguvu wenyewe,

kusanya nguvu zako zote!

2:2 Eze 37:23; Isa 60:15Bwana atarudisha fahari ya Yakobo,

kama fahari ya Israeli,

ingawa waangamizi wamewaacha ukiwa

na wameharibu mizabibu yao.

2:3 Eze 23:14-15Ngao za askari wake ni nyekundu,

mashujaa wamevaa nguo nyekundu.

Chuma kwenye magari ya vita chametameta,

katika siku aliyoyaweka tayari,

mikuki ya mierezi inametameta.

2:4 Yer 4:13; Eze 23:24Magari ya vita yanafanya msukosuko barabarani,

yakikimbia nyuma na mbele uwanjani.

Yanaonekana kama mienge ya moto;

yanakwenda kasi kama umeme.

2:5 Yer 46:12Anaita vikosi vilivyochaguliwa,

lakini bado wanajikwaa njiani.

Wanakimbilia haraka kwenye ukuta wa mji,

ile ngao ya kuwakinga imetayarishwa.

2:6 Isa 45:1; Nah 3:13Malango ya mto yamefunguliwa wazi,

na jumba la kifalme limeanguka.

2:7 Mwa 8:8; Isa 59:11; 32:12Imeagizwa kwamba mji uchukuliwe

na upelekwe uhamishoni.

Vijakazi wake wanaomboleza kama hua

na kupigapiga vifua vyao.

Ninawi ni kama dimbwi,

nayo maji yake yanakauka.

Wanalia, “Simama! Simama!”

Lakini hakuna anayegeuka nyuma.

Chukueni nyara za fedha!

Chukueni nyara za dhahabu!

Wingi wake hauna mwisho,

utajiri kutoka hazina zake zote!

2:10 Yos 2:11; 7:5; Isa 29:22Ameharibiwa, ametekwa nyara, ameachwa uchi!

Mioyo inayeyuka, magoti yanalegea,

miili inatetemeka,

na kila uso umebadilika rangi.

2:11 Isa 5:29Liko wapi sasa pango la simba,

mahali ambapo waliwalisha watoto wao,

ambapo simba dume na simba jike walikwenda

na ambapo wana simba walikwenda

bila kuogopa chochote?

2:12 Yer 51:34; 4:7; Isa 37:18Simba aliua mawindo ya kutosha watoto wake,

alinyonga mawindo kwa ajili ya mwenzi wake,

akijaza makao yake kwa alivyoua

na mapango yake kwa mawindo.

2:13 Isa 10:5-13; Yer 21:13; Nah 3:5; Za 46:9; 2Sam 2:26; Mik 5:6Bwana Mwenye Nguvu Zote anatangaza,

“Mimi ni kinyume na ninyi.

Magari yenu ya vita nitayateketeza kwa moto,

na upanga utakula wana simba wako.

Sitawaachia mawindo juu ya nchi.

Sauti za wajumbe wako

hazitasikika tena.”

Read More of Nahumu 2

Nahumu 3:1-19

Ole Wa Ninawi

3:1 Eze 22:2; Mik 3:10; Za 12:2Ole wa mji umwagao damu,

uliojaa uongo,

umejaa nyara,

usiokosa kuwa na vitu vya kuteka nyara.

3:2 Isa 34:3; Yer 47:3Kelele za mijeledi,

vishindo vya magurudumu,

farasi waendao mbio

na mshtuo wa magari ya vita!

Wapanda farasi wanaenda mbio,

panga zinameremeta,

na mikuki inangʼaa!

Majeruhi wengi,

malundo ya maiti,

idadi kubwa ya miili isiyohesabika,

watu wanajikwaa juu ya mizoga:

3:4 Isa 47:9; 23:17; 2The 2:9, 10; Dan 2:2; Ufu 9:20, 21; Eze 16:25-29yote haya kwa sababu ya wingi wa tamaa za kahaba,

anayeshawishi, bibi wa mambo ya uchawi,

anayewatia utumwani mataifa kwa ukahaba wake

na pia jamaa za watu kwa ulozi wake.

3:5 Nah 2:13; Isa 47:2-3; 20:4; Yer 13:22Bwana Mwenye Nguvu Zote anasema,

“Mimi ni kinyume na ninyi.

Nitafunika uso wako kwa gauni lako.

Nitaonyesha mataifa uchi wako

na falme aibu yako.

3:6 Kut 29:14; Ay 9:31; 1Sam 2:30; Yer 51:37; Isa 14:16Nitakutupia uchafu,

nitakufanyia dharau

na kukufanya kioja.

3:7 Isa 13:14; 31:9; Nah 1:1; Ay 3:14; Yer 51:37Wote wanaokuona watakukimbia na kusema,

‘Ninawi ipo katika kuangamia:

ni nani atakayeomboleza kwa ajili yake?’

Nitampata wapi yeyote wa kukufariji?”

3:8 Amo 6:2; Yer 46:25; Isa 19:6-9Je, wewe ni bora kuliko No-Amoni,

uliopo katika Mto Naili,

uliozungukwa na maji?

Mto ulikuwa kinga yake,

nayo maji yalikuwa ukuta wake.

3:9 Mwa 10:6; 2Nya 12:3; Eze 27:10; 30:5Kushi3:9 Kushi ni Ethiopia. na Misri walikuwa nguvu zake zisizo na mpaka;

Putu na Libia walikuwa miongoni mwa wale walioungana naye.

3:10 Isa 20:4; 2Fal 8:12; Isa 13:16; Hos 13:16; Ay 6:26-27; Eze 24:6; Yer 40:1; Yoe 3:3; Oba 1:11Hata hivyo alichukuliwa mateka

na kwenda uhamishoni.

Watoto wake wachanga walivunjwa vunjwa vipande

kwenye mwanzo wa kila barabara.

Kura zilipigwa kwa watu wake wenye heshima,

na watu wake wote wakuu walifungwa kwa minyororo.

3:11 Isa 49:26; 2:10Wewe pia utalewa;

utakwenda mafichoni

na kutafuta kimbilio kutoka kwa adui.

3:12 Wim 2:13; Ufu 6:13; Isa 28:4Ngome zako zote ni kama mitini

yenye matunda yake ya kwanza yaliyoiva;

wakati inapotikiswa,

tini huanguka kwenye kinywa chake alaye.

3:13 Isa 19:16; 45:2; Yer 50:37; Nah 2:6Tazama vikosi vyako:

wote ni wanawake!

Malango ya nchi yako

yamekuwa wazi kwa adui zako;

moto umeteketeza mapingo yake.

3:14 2Nya 32:4; Nah 2:1Teka maji kwa ajili ya kuzingirwa kwako,

imarisha ulinzi wako,

Ufanyie udongo wa mfinyanzi kazi,

yakanyage matope,

karabati tanuru la kuchomea matofali!

3:15 Isa 27:1; 2Sam 2:26; Yer 51:14; Yoe 1:4Huko moto utakuteketeza,

huko upanga utakuangusha chini

na kama vile panzi, watakumaliza.

Ongezeka kama panzi,

ongezeka kama nzige!

3:16 Kut 10:13Umeongeza idadi ya wafanyabiashara wako

mpaka wamekuwa wengi kuliko nyota za angani,

lakini kama nzige wanaacha nchi tupu

kisha huruka na kwenda zake.

3:17 Ufu 9:7; Yer 51:17Walinzi wako ni kama nzige,

maafisa wako ni kama makundi ya nzige

watuao kwenye kuta wakati wa siku ya baridi:

lakini wakati jua linapotokea wanaruka kwenda zao,

na hakuna ajuaye waendako.

3:18 Za 76:5-6; Yer 25:27; 50:18; Eze 31:3; Isa 56:10; 1Fal 22:17Ee mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wanasinzia;

wakuu wako wanalala chini mavumbini kupumzika.

Watu wako wametawanyika juu ya milima

bila kuwa na mtu yeyote wa kuwakusanya.

3:19 Yer 30:13; Mik 1:9; Ay 27:23; Mao 2:15; Sef 2:15; Isa 14:8; 37:18Hakuna kitu kinachoweza kuponya jeraha lako;

jeraha lako ni la kukuua.

Kila anayesikia habari zako,

hupiga makofi kwa kuanguka kwako,

kwa kuwa ni nani ambaye hajaguswa

na ukatili wako usio na mwisho?

Read More of Nahumu 3