Mika 5:1-15, Mika 6:1-16, Mika 7:1-20 NEN

Mika 5:1-15

Mtawala Aliyeahidiwa Kutoka Bethlehemu

5:1 Ay 16:10; Mt 27:30; Mao 3:30Panga majeshi yako, ee mji wa majeshi,

kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu.

Watampiga mtawala wa Israeli

shavuni kwa fimbo.

5:2 Yn 7:42; Mwa 35:19; 48:7; 1Sam 13:14; Hes 24:19; 2Sam 6:21; 2Nya 7:18; Za 90:2; 132:6; 102:25; Isa 9:6; Mit 8:22; Yn 1:1; Mt 2:6“Lakini wewe, Bethlehemu Efrathi,

ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda,

kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu

yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli,

ambaye asili yake ni kutoka zamani,

kutoka milele.”

5:3 Yer 7:29Kwa hiyo Israeli utaachwa mpaka wakati

mwanamke aliye na utungu atakapozaa

na ndugu zake wengine warudi

kujiunga na Waisraeli.

5:4 Isa 40:11; 49:9; 52:13; Za 72:8; Zek 9:10; Mik 7:14; Eze 34:11-15; Lk 1:32Atasimama na kulichunga kundi lake

katika nguvu ya Bwana,

katika utukufu wa jina la Bwana Mungu wake.

Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huo

ukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia.

5:5 Isa 8:7; 9:6; 10:24-27; Lk 2:14; Efe 2:14; Kol 1:19-20Naye atakuwa amani yao.

Ukombozi Na Uharibifu

Wakati Mwashuru atakapovamia nchi yetu

na kupita katika ngome zetu,

tutawainua wachungaji saba dhidi yake,

hata viongozi wanane wa watu.

5:6 Mwa 10:8; Sef 2:13; Lk 1:71; Nah 2:11-13Wataitawala nchi ya Ashuru kwa upanga,

nchi ya Nimrodi kwa upanga.

Atatuokoa kutoka kwa Mwashuru

atakapoivamia nchi yetu

na kuingia katika mipaka yetu.

5:7 Amo 5:15; Mik 2:12; Isa 44:4; Za 110:3; 133:3Mabaki ya Yakobo yatakuwa

katikati ya mataifa mengi

kama umande kutoka kwa Bwana,

kama manyunyu juu ya majani,

ambayo hayamngoji mtu

wala kukawia kwa mwanadamu.

5:8 Mwa 49:9; Mik 4:13; Zek 10:5; Isa 5:29; Za 50:22; Hos 5:14Mabaki ya Yakobo yatakuwa miongoni mwa mataifa,

katikati ya mataifa mengi,

kama simba miongoni mwa wanyama wa msituni,

kama mwana simba miongoni

mwa makundi ya kondoo,

ambaye anaumiza vibaya na kuwararua

kila anapopita katikati yao,

wala hakuna awezaye kuokoa.

5:9 Za 10:12Mkono wako utainuliwa juu kwa ushindi juu ya watesi wako,

nao adui zako wote wataangamizwa.

5:10 Kut 15:4, 19; Hos 14:3; Hag 2:22; Zek 9:10“Katika siku ile,” asema Bwana,

“nitaangamiza farasi zenu katikati yenu

na kubomoa magari yenu ya vita.

5:11 Kum 29:23; Isa 6:11; Mao 2:2; Hos 10:14; Amo 5:9Nitaiangamiza miji ya nchi yenu

na kuziangusha chini ngome zenu zote.

5:12 Kum 18:10-12; Isa 8:19; 2:9Nitaangamiza uchawi wenu

na hamtapiga tena ramli.

5:13 Nah 1:14; Hos 2:10; Isa 2:8; 2:18; Eze 6:9; Zek 13:2Nitaangamiza vinyago vyenu vya kuchonga

na mawe yenu ya ibada yatoke katikati yenu;

hamtasujudia tena

kazi ya mikono yenu.

5:14 Kut 34:13; Amu 3:7; 2Fal 17:10Nitangʼoa nguzo za Ashera katikati yenu

na kubomoa miji yenu.

5:15 Isa 65:12Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabu

juu ya mataifa ambayo hayajanitii.”

Read More of Mika 5

Mika 6:1-16

Shauri La Bwana Dhidi Ya Israeli

6:1 Za 50:1; Eze 6:2Sikiliza asemalo Bwana:

“Simama, tetea shauri lako mbele ya milima;

vilima na visikie lile unalotaka kusema.

6:2 Kum 32:1; Hos 12:2; Isa 3:13; Za 50:7; Yer 9:7Sikilizeni, ee milima, mashtaka ya Bwana,

sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia.

Kwa kuwa Bwana ana shauri dhidi ya watu wake;

anatoa mashtaka dhidi ya Israeli.

6:3 Za 50:7; Isa 5:3, 4; Yer 2:31; 2:5“Watu wangu, nimewatendea nini?

Nimewalemea kwa jinsi gani? Mnijibu.

6:4 Kum 7:8; Kut 3:10; 6:6; 4:16; 15:20; Hes 33:1; Za 77:20Nimewatoa kutoka Misri na kuwakomboa

kutoka nchi ya utumwa.

Nilimtuma Mose awaongoze,

pia Aroni na Miriamu.

6:5 Hes 22:2-6Watu wangu, kumbukeni jinsi Balaki mfalme wa Moabu

alivyofanya shauri

na kile Balaamu mwana wa Beori alichojibu.

Kumbukeni safari yenu kutoka Shitimu mpaka Gilgali,

ili mfahamu matendo ya haki ya Bwana.”

6:6 Yn 6:28; Za 15:1; 40:6-8; 95:2; 51:16-17Nimjie Bwana na kitu gani na kusujudu

mbele za Mungu aliyetukuka?

Je, nije mbele zake na sadaka za kuteketezwa,

nije na ndama za mwaka mmoja?

6:7 Isa 1:11; 40:16; Law 18:21; Za 50:8-10; 2Fal 3:27; 16:3; Amo 5:22; Hos 5:6Je, Bwana atafurahishwa na kondoo dume elfu,

au mito elfu kumi ya mafuta?

Je, nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu,

mtoto wangu mwenyewe

kwa ajili ya dhambi ya nafsi yangu?

6:8 Isa 1:17; Yer 22:3; 23:23; 2Fal 22:19; Isa 57:15; Mwa 5:22; 1Sam 15:22; Kum 10:12-13; Zek 7:9-10; Mt 9:13; Mk 12:33; Lk 11:42Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu.

Bwana anataka nini kwako?

Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema,

na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.

Hatia Na Adhabu Ya Israeli

6:9 Mwa 17:1; Isa 11:4Sikiliza! Bwana anauita mji:

kulicha jina lako ni hekima:

“Tii hiyo fimbo na yeye aliyeiamuru.

6:10 Eze 45:9-10; Amo 3:10; 8:4-6Je, bado nisahau, ee nyumba ya uovu,

hazina yako uliyopata kwa udanganyifu

na vipimo vilivyopunguka,

ambavyo vimelaaniwa?

6:11 Law 19:36; Hos 12:7; Amu 3:10; Kum 25:13Je, naweza kuhukumu kuwa

mtu mwenye mizani ya udanganyifu hana hatia,

aliye na mfuko wa mawe ya kupimia ya uongo?

6:12 Isa 1:23; 3:8; Za 35:20; 116:11; Yer 9:5Matajiri wake ni wajeuri;

watu wake ni waongo

na ndimi zao zinazungumza

kwa udanganyifu.

Kwa hiyo, nimeanza kukuharibu,

kuwaangamiza kwa sababu ya dhambi zenu.

6:14 Isa 9:20; 30:6; Hos 4:10Mtakula lakini hamtashiba;

matumbo yenu bado yatakuwa matupu.

Mtaweka akiba lakini hamtaokoa chochote,

kwa sababu mtakachoweka akiba

nitatoa kwa upanga.

6:15 Kum 28:36-38; Yer 12:13; Ay 24:11; Amo 5:11; Sef 1:13Mtapanda lakini hamtavuna;

mtakamua zeituni lakini

hamtatumia mafuta yake.

Mtakamua zabibu

lakini hamtakunywa hiyo divai.

6:16 1Fal 16:25, 29-33; Yer 7:24; 25:9; 51:51; Mik 2:6Mmezishika sheria za Omri

na matendo yote ya nyumba ya Ahabu,

tena umefuata desturi zao.

Kwa hiyo nitakutoa kwa maangamizi

na watu wako kuwa dhihaka;

mtachukua dharau za mataifa.”

Read More of Mika 6

Mika 7:1-20

Taabu Ya Israeli

7:1 Yer 2:3; Hos 9:10; Wim 2:13Taabu gani hii niliyo nayo!

Nimefanana na yule akusanyaye

matunda ya kiangazi,

aokotaye masazo baada ya kuvunwa

shamba la mizabibu;

hakuna kishada chenye matunda ya kula,

hakuna hata ile tini ya mwanzoni ninayoitamani.

7:2 Za 10:8; 12:1; 57:6; Yer 2:29; 8:6; 5:26; Mit 6:17; 1Sam 24:11; Hab 1:15; Mik 3:10; Isa 3:5Wanaomcha Mungu wameondolewa kutoka nchi;

hakuna mtu mnyofu hata mmoja aliyebaki.

Watu wote wanavizia kumwaga damu,

kila mmoja anamwinda ndugu yake kwa wavu.

7:3 Mit 4:16; Kut 23:8; Hos 4:18; Isa 1:23; Eze 22:12Mikono yote miwili ni hodari katika kufanya ubaya,

mtawala anadai zawadi,

hakimu anapokea rushwa,

wenye nguvu wanaamuru wanachotaka:

wote wanafanya shauri baya pamoja.

7:4 Hes 33:55; Eze 2:6; Ay 31:14; 2Sam 23:6; Isa 22:5; Hos 9:7Aliye mwema kupita wote kati yao

ni kama mchongoma,

anayeonekana mnyofu zaidi miongoni mwao

ni mbaya kuliko uzio wa miiba.

Siku ya walinzi wako imewadia,

siku atakayokutembelea Mungu.

Sasa ni wakati wao

wa kuchanganyikiwa.

Usimtumaini jirani;

usiweke matumaini kwa rafiki.

Hata kwa yule alalaye kifuani mwako

uwe mwangalifu kwa maneno yako.

7:6 Eze 22:7; Mwa 9:22-24; Mt 10:21, 35-36; Mk 13:12Kwa kuwa mwana humdharau baba yake,

naye binti huinuka dhidi ya mama yake,

mkwe kuwa kinyume na mama mkwe wake:

adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake hasa.

7:7 Isa 21:8; 25:9; Za 4:3; 130:5Lakini mimi, namtazama Bwana kwa matumaini,

namngoja Mungu Mwokozi wangu;

Mungu wangu atanisikia mimi.

Israeli Atainuka

7:8 Za 20:8; 22:17; 37:24; 37:5, 6; Mit 24:17; Mik 4:11; Mao 4:21; 2Sam 22:29; Isa 9:2Usifurahie msiba wangu, ee adui yangu!

Ingawa nimeanguka, nitainuka.

Japo ninaketi gizani,

Bwana atakuwa nuru yangu.

7:9 Mao 3:39-40; Za 107:10; 119:154; Isa 46:13Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake,

nitabeba ghadhabu ya Bwana,

mpaka atakaponitetea shauri langu

na kuithibitisha haki yangu.

Atanileta nje kwenye mwanga,

nami nitaiona haki yake.

7:10 Za 35:26; 42:3; Isa 5:5; 51:23; Ay 40:12; Zek 10:5; 2Sam 22:43Kisha adui yangu ataliona

naye atafunikwa na aibu,

yule aliyeniambia,

“Yu wapi Bwana Mungu wako?”

Macho yangu yataona kuanguka kwake,

hata sasa atakanyagwa chini ya mguu

kama tope barabarani.

7:11 Amo 9:11; Isa 54:11Siku ya kujenga kuta zako itawadia,

siku ya kupanua mipaka yako.

7:12 Isa 19:23-25; 11:11; 60:4Siku hiyo watu watakuja kwako

kutoka Ashuru na miji ya Misri,

hata kutoka Misri hadi Frati

na kutoka bahari hadi bahari

na kutoka mlima hadi mlima.

7:13 Isa 3:10-11; Eze 12:19; 33:28-29Dunia itakuwa ukiwa kwa sababu ya wakazi wake,

kwa sababu ya matunda ya matendo yao.

Sala Na Sifa

7:14 Za 23:4; 28:9; 95:7; Mik 5:4; 7:14; Hes 23:9; Kum 33:28; Wim 4:1; Isa 33:9; Yer 50:19; Eze 36:11Wachunge watu wako kwa fimbo yako,

kundi la urithi wako,

ambalo linaishi peke yake msituni,

katika nchi ya malisho yenye rutuba.

Waache walishe katika Bashani na Gileadi

kama ilivyokuwa siku za kale.

7:15 Kut 3:20; Za 78:12“Kama siku zile mlipotoka Misri,

nitawaonyesha maajabu yangu.”

7:16 Isa 26:11; Amu 18:19Mataifa yataona na kuaibika,

waliondolewa nguvu zao zote.

Wataweka mikono yao kwenye vinywa vyao

na masikio yao yatakuwa na uziwi.

7:17 Mwa 3:14; 2Sam 22:46; Isa 25:3; 59:19Wataramba mavumbi kama nyoka,

kama viumbe vitambaavyo juu ya ardhi.

Watatoka nje ya mapango yao wakitetemeka;

watamgeukia Bwana Mungu wetu kwa hofu

nao watakuogopa.

7:18 Kut 10:8; 1Sam 2:2; Isa 43:25; 54:9; 57:16; Zek 3:4; Yer 31:20; 50:20; Kut 15:11; 34:6, 7, 9; Za 89:6-8; 103:9; 2Nya 6:21; 30:9; Za 103:8-13; Yoe 2:32; Amo 5:15; Mik 2:12Ni nani Mungu kama wewe,

ambaye anaachilia dhambi

na kusamehe makosa

ya mabaki ya urithi wake?

Wewe huwi na hasira milele,

bali unafurahia kuonyesha rehema.

7:19 Isa 43:25; Rum 6:6; Yer 31:34Utatuhurumia tena,

utazikanyaga dhambi zetu

chini ya nyayo zako,

na kutupa maovu yetu yote

katika vilindi vya bahari.

7:20 Gal 3:16; Kum 11:29; 7:8; Lk 1:72; Za 108:4Utakuwa wa kweli kwa Yakobo,

nawe utamwonyesha Abrahamu rehema,

kama ulivyowaahidi kwa kiapo baba zetu

siku za kale.

Read More of Mika 7