Mika 1:1-16, Mika 2:1-13, Mika 3:1-12, Mika 4:1-13 NEN

Mika 1:1-16

1:1 Yer 26:18; 2Pet 1:21; 1Nya 3:12-13; Hos 1:1; Isa 1:1Neno la Bwana lilimjia Mika, Mmoreshethi, wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda; ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu.

1:2 Kum 4:26; 32:1; Yer 6:19; Mwa 31:50; Za 11:4; Isa 1:2Sikieni, enyi mataifa, enyi nyote,

sikilizeni, ee dunia na wote mliomo ndani yake,

ili Bwana Mwenyezi ashuhudie dhidi yenu,

Bwana kutoka Hekalu lake takatifu.

Hukumu Dhidi Ya Samaria Na Yerusalemu

1:3 Isa 18:4; 64:1; 26:21; Eze 3:12; Ebr 12:18, 19; Amo 4:13Tazama! Bwana anakuja kutoka mahali pake;

anashuka na kukanyaga

mahali palipoinuka juu pa dunia.

1:4 Za 46:2-6; Hes 16:31; Nah 1:5Milima inayeyuka chini yake

na mabonde yanagawanyika

kama nta mbele ya moto,

kama maji yatiririkayo kasi

kwenye mteremko.

1:5 Amo 8:14; Hos 5:5; Yer 2:18-19Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo,

ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli.

Kosa la Yakobo ni lipi?

Je, sio Samaria?

Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia miungu ni nini?

Je, sio Yerusalemu?

1:6 Kum 20:6; Amo 5:11“Kwa hiyo nitaufanya Samaria kuwa lundo la kokoto,

mahali pa kuotesha mizabibu.

Nitayamwaga mawe yake katika bonde

na kuacha wazi misingi yake.

1:7 Eze 6:6; Kut 32:20; Kum 9:21; 23:17-18Sanamu zake zote

zitavunjwa vipande vipande;

zawadi zake zote za Hekalu

zitachomwa kwa moto;

nitaharibu vinyago vyake vyote.

Kwa kuwa alikusanya zawadi zake

kutokana na ujira wa kahaba,

nazo zitatumika tena

kulipa mishahara ya kahaba.”

Kulia Na Kuomboleza

1:8 Isa 15:3; 20:2Kwa ajili ya hili nitalia na kuomboleza;

nitatembea bila viatu na tena uchi.

Nitabweka kama mbweha

na kuomboleza kama bundi.

1:9 Yer 46:11; 10:19; 2Fal 18:13; Isa 3:26Kwa sababu jeraha lake halitibiki;

limekuja Yuda.

Limefika hasa kwenye lango la watu wangu,

hata Yerusalemu kwenyewe.

Usiliseme hili huko Gathi;

usilie hata kidogo.

Huko Beth-le-Afra

gaagaa mavumbini.

1:11 Eze 23:29Piteni mkiwa uchi na wenye aibu,

ninyi mkaao Shafiri.

Wale waishio Saanani

hawatatoka nje.

Beth-Eseli iko katika maombolezo;

kinga yake imeondolewa kwako.

1:12 Yer 14:19; 40:2Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivu

wakingoja msaada,

kwa sababu maangamizi yamekuja

kutoka kwa Bwana,

hata katika lango la Yerusalemu.

1:13 Yos 10:3; Za 9:14Enyi mkaao Lakishi,

fungeni farasi kwenye magari ya vita.

Mlikuwa chanzo cha dhambi

kwa Binti Sayuni,

kwa kuwa makosa ya Israeli

yalikutwa kwako.

1:14 2Fal 16:8; Yos 15:44; Yer 15:18Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi

zawadi za kuagana.

Mji wa Akzibu utaonyesha wazi udanganyifu

kwa wafalme wa Israeli.

1:15 Yos 15:44; 12:15Nitawaleteeni atakayewashinda

ninyi mnaoishi Maresha.

Yeye aliye utukufu wa Israeli

atakuja Adulamu.

1:16 Law 13:40; Ay 1:20; 2Fal 18:13; Amo 5:27; Kum 4:27Nyoeni nywele zenu katika kuomboleza

kwa ajili ya watoto wenu mnaowafurahia;

jifanyieni upara kama tai,

kwa kuwa watawaacha

na kwenda uhamishoni.

Read More of Mika 1

Mika 2:1-13

Mipango Ya Mwanadamu Na Ya Mungu

2:1 Isa 29:20; 32:7; Es 3:8, 9; Za 36:4; 7:11-14; Hos 7:6; Mwa 31:29Ole kwa wale wapangao uovu,

kwa wale wafanyao shauri la hila vitandani mwao!

Kunapopambazuka wanalitimiza

kwa sababu uko katika uwezo wao kutekeleza.

2:2 Isa 1:23; 5:8; Mit 30:14; Yer 22:17; 1Sam 8:14; Eze 46:18Wanatamani mashamba na kuyakamata,

pia nyumba na kuzichukua.

Wanamlaghai mwanaume nyumba yake,

mwanadamu mwenzake urithi wake.

2:3 Yer 18:11; 8:3; Amo 3:1-2; Isa 2:12Kwa hiyo, Bwana asema:

“Ninapanga maangamizi dhidi ya watu hawa,

ambayo hamwezi kujiokoa wenyewe.

Hamtatembea tena kwa majivuno,

kwa kuwa utakuwa ni wakati wa maafa.

2:4 Law 26:31; Yer 4:13; 6:12Siku hiyo watu watawadhihaki,

watawafanyia mzaha

kwa wimbo huu wa maombolezo:

‘Tumeangamizwa kabisa;

mali ya watu wangu imegawanywa.

Ameninyangʼanya!

Ametoa mashamba yetu kwa wasaliti.’ ”

2:5 Kum 32:8, 9, 13; Yos 18:4; Hes 34:13Kwa hiyo hutakuwa na yeyote katika kusanyiko la Bwana

wa kugawanya mashamba kwa kura.

Manabii Wa Uongo

2:6 Za 44:13; Yer 19:8; 18:16; 25:18; 29:18; Mik 6:16; Amo 2:12Manabii wao husema, “Usitabiri.

Usitabiri kuhusu vitu hivi;

aibu haitatupata.”

2:7 Za 119:65; 15:2; 84:11Je, ingesemwa, ee nyumba ya Yakobo:

“Je, Roho wa Bwana amekasirika?

Je, yeye hufanya vitu kama hivyo?”

“Je, maneno yangu hayamfanyii mema

yeye ambaye njia zake ni nyofu?

Siku hizi watu wangu wameinuka

kama adui.

Unawavua joho la kitajiri wale wanaopita

pasipo kujali,

kama watu warudio kutoka vitani.

2:9 Yer 10:20Unawahamisha wanawake wa watu wangu

kutoka kwenye nyumba zao za kupendeza.

Unaondoa baraka yangu

kwa watoto wao milele.

2:10 Kum 12:9; Law 18:25-29; Za 106:38-39; Mao 4:15Inuka, nenda zako!

Kwa maana hapa sio mahali pako pa kupumzikia,

kwa sababu pametiwa unajisi,

pameharibiwa, wala hapatengenezeki tena.

2:11 2Nya 36:16; Yer 5:31; Law 10:9; Isa 30:10Ikiwa mwongo na mdanganyifu atakuja na kusema,

‘Nitawatabiria divai na pombe kwa wingi,’

angekuwa ndiye nabii

anayekubalika na watu hawa!

Ahadi Ya Ukombozi

2:12 Mik 4:6, 7; 5:7; 7:18; Isa 11:11; Sef 3:19; Neh 1:9“Hakika nitawakusanya ninyi nyote, ee Yakobo,

Hakika nitawaleta pamoja mabaki ya Israeli.

Nitawaleta pamoja kama kondoo ndani ya zizi,

kama kundi kwenye malisho yake,

mahali hapa patakuwa na msongamano wa watu.

2:13 Isa 52:12; 60:11Yeye afunguaye njia atawatangulia;

watapita kwenye lango na kutoka nje.

Mfalme wao atawatangulia,

Bwana atakuwa kiongozi.”

Read More of Mika 2

Mika 3:1-12

Viongozi Na Manabii Wakemewa

3:1 Yer 5:5Kisha nikasema,

“Sikilizeni enyi viongozi wa Yakobo,

enyi watawala wa nyumba ya Israeli.

Je, hampaswi kujua hukumu,

3:2 Za 53:4; Eze 22:27ninyi mnaochukia mema

na kupenda maovu;

ninyi mnaowachuna watu wangu ngozi

na kuondoa nyama kwenye mifupa yao;

3:3 Za 14:4; Sef 3:3; Ay 24:14; Eze 11:7; 24:4-5; 34:4ninyi mnaokula nyama ya watu wangu,

mnaowachuna ngozi

na kuvunja mifupa yao vipande vipande;

mnaowakatakata kama nyama

ya kuwekwa kwenye sufuria

na kama nyama

ya kuwekwa kwenye chungu?”

3:4 Kum 1:45; 31:17; 1Sam 8:18; Yer 11:11; Isa 58:4; Mit 1:28; Ay 15:31; Eze 8:18Kisha watamlilia Bwana,

lakini hatawajibu.

Wakati huo atawaficha uso wake

kwa sababu ya uovu waliotenda.

3:5 Isa 3:12; 9:16; 53:6; 56:10; Mt 7:15; Yer 4:10Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kuhusu manabii wanaowapotosha watu wangu,

mtu akiwalisha,

wanatangaza ‘amani’;

kama hakufanya hivyo,

wanaandaa kupigana vita dhidi yake.

3:6 Isa 8:19-22; 29:10; Eze 7:26; 12:24Kwa hiyo usiku utawajieni, msiweze kuwa na maono,

na giza, msiweze kubashiri.

Jua litawachwea manabii hao,

nao mchana utakuwa giza kwao.

3:7 Yer 6:15; Mik 7:16; Isa 44:25; Es 6:12; Za 74:9; Amu 8:11; Law 13:45; Eze 20:3Waonaji wataaibika

na waaguzi watafedheheka.

Wote watafunika nyuso zao

kwa sababu hakuna jibu litokalo kwa Mungu.”

3:8 1Kor 2:1, 4; Isa 58:1; 57:12; 61:2Lakini kuhusu mimi, nimejazwa nguvu,

nimejazwa Roho wa Bwana,

haki na uweza,

kumtangazia Yakobo kosa lake,

na Israeli dhambi yake.

3:9 Isa 58:1-2; 1:23Sikieni hili, enyi viongozi wa nyumba ya Yakobo,

enyi watawala wa nyumba ya Israeli,

mnaodharau haki

na kupotosha kila lililo sawa;

3:10 Yer 22:13, 17; Isa 59:7; Mik 7:2; Hab 2:12; Nah 3:1; Eze 22:27mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu

na Yerusalemu kwa uovu.

3:11 Kut 23:8; Law 19:15; Mal 2:9; Eze 22:12; Mik 7:3; Yer 6:13; 1Tim 1:11; 1Sam 4:5-6; Eze 13:19; 34:2; Isa 1:23; 10:20; 56:11; Yer 6:13; 7:4; Mao 4:13; Hos 4:8, 18Viongozi wake wanahukumu kwa rushwa,

na makuhani wake wanafundisha kwa malipo,

nao manabii wake wanatabiri kwa fedha.

Hata hivyo wanamwegemea Bwana na kusema,

“Je, Bwana si yumo miongoni mwetu?

Hakuna maafa yatakayotupata.”

3:12 2Fal 25:9; Isa 6:11; Mik 1:6; Za 79:1; Yer 52:13; 22:6; Mao 5:18; Eze 5:14Kwa hiyo kwa sababu yenu,

Sayuni italimwa kama shamba,

Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto,

na kilima cha Hekalu

kitakuwa kichuguu

kilichofunikwa na vichaka.

Read More of Mika 3

Mika 4:1-13

Mlima Wa Bwana

(Isaya 2:2-4)

4:1 Za 48:1; 86:9; Zek 8:3; Isa 2:2; Dan 2:35; 2:44; Eze 17:22; Yer 3:17; 31:12Katika siku za mwisho

mlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwa

kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote;

utainuliwa juu ya vilima,

na watu wa mataifa watamiminika humo.

4:2 Yer 31:6; Yn 6:45; Eze 20:40; Zek 2:11; 14:16; Isa 54:13; Za 25:8-9; 119:171Mataifa mengi yatakuja na kusema,

“Njooni, twendeni mlimani mwa Bwana,

kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo.

Atatufundisha njia zake,

ili tuweze kuenenda katika mapito yake.”

Sheria itatoka Sayuni,

neno la Bwana litatoka Yerusalemu.

4:3 Isa 2:4; 11:4; Yoe 3:10; Hos 2:18; Za 72:7; Zek 8:20-22; 9:10; Za 46:9Atahukumu kati ya mataifa mengi,

na ataamua migogoro ya mataifa

yenye nguvu na yaliyo mbali.

Watafua panga zao ziwe majembe,

na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi.

Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine,

wala hawatajifunza vita tena.

4:4 1Fal 4:25; Law 26:6; Eze 39:26; Isa 1:20; 36:16; Yer 31:10; Zek 3:10Kila mtu ataketi chini ya mzabibu wake

na chini ya mtini wake,

wala hakuna mtu atakayewaogopesha,

kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amesema.

4:5 2Fal 17:29; Mdo 14:16; Yos 24:14-15; Isa 26:8; Yer 2:11; Zek 10:12Mataifa yote yanaweza kutembea

katika jina la miungu yao;

sisi tutatembea katika jina la Bwana

Mungu wetu milele na milele.

Mpango Wa Bwana

4:6 Yer 31:8; Isa 56:8; Za 147:2; 106:47; Eze 34:13, 16; 37:21; Sef 3:19“Katika siku hiyo,” asema Bwana,

“nitawakusanya walemavu;

nitawakusanya walio uhamishoni

na wale niliowahuzunisha.

4:7 Yoe 2:32; Mik 2:12; Isa 9:6; Mwa 12:2; Dan 2:44; 7:14; Ufu 11:15; Lk 1:33Nitawafanya walemavu kuwa mabaki,

wale waliofukuzwa kuwa taifa lenye nguvu.

Bwana atatawala juu yao katika Mlima Sayuni

kuanzia siku hiyo na hata milele.

4:8 Isa 1:26; Zek 9:9Lakini kuhusu wewe, ee mnara wa ulinzi wa kundi,

ee ngome ya Binti Sayuni,

milki ya awali itarudishwa kwako,

ufalme utakuja kwa Binti Yerusalemu.”

4:9 Yer 8:19; 30:6; 48:41; Mwa 3:16Kwa nini sasa unalia kwa nguvu:

kwani huna mfalme?

Je, mshauri wako amekufa, hata maumivu yakukamate

kama ya mwanamke

aliye na utungu wa kuzaa?

4:10 Kum 21:10; 2Fal 20:18; Isa 43:14; 48:20Gaagaa kwa utungu, ee Binti Sayuni,

kama mwanamke mwenye utungu wa kuzaa,

kwa kuwa sasa ni lazima uuache mji

ukapige kambi uwanjani.

Utakwenda Babeli;

huko utaokolewa.

Huko Bwana atakukomboa

kutoka mikononi mwa adui zako.

4:11 Mao 2:16; Oba 1:12; Mik 7:8Lakini sasa mataifa mengi

yamekusanyika dhidi yako.

Wanasema, “Mwache anajisiwe,

macho yetu na yatazame Sayuni kwa furaha!”

4:12 Mwa 50:20; Isa 55:8; Rum 11:33-34Lakini hawayajui

mawazo ya Bwana;

hawauelewi mpango wake,

yeye awakusanyaye kama miganda

kwenye sakafu ya kupuria.

4:13 Isa 21:10; 23:18; 45:1; Ufu 21:24; Dan 2:44“Inuka upure, ee Binti Sayuni,

kwa kuwa nitakupa pembe za chuma;

nitakupa kwato za shaba

na utavunja vipande vipande mataifa mengi.”

Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwa Bwana,

utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.

Read More of Mika 4