Mathayo 7:24-29, Mathayo 8:1-22 NEN

Mathayo 7:24-29

Msikiaji Na Mtendaji

(Luka 6:47-49)

7:24 Mt 7:21; Yak 1:22-25“Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba. Lakini haikuanguka; kwa sababu msingi wake ulikuwa kwenye mwamba. Naye kila anayesikia haya maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. 7:27 Eze 13:10, 11Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, nao upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.”

7:28 Mt 19:1; 26:1; Mk 11:18; Yn 7:46Yesu alipomaliza kusema maneno haya, makutano ya watu wakashangazwa sana na mafundisho yake, 7:29 Yn 7:46kwa sababu alifundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wao wa sheria.

Read More of Mathayo 7

Mathayo 8:1-22

Yesu Amtakasa Mwenye Ukoma

(Marko 1:40-45; Luka 5:12-16)

Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makutano makubwa ya watu yakamfuata. 8:2 Law 13:45; Lk 17:12; Mt 18:26; 20:22Mtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake, akasema, “Bwana, kama ukitaka, unaweza kunitakasa.”

Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa yule mtu, akamwambia, “Nataka. Takasika!” Mara yule mtu akatakasika ukoma wake. 8:4 Mk 8:30; Lk 4:41; Law 14:2-32Kisha Yesu akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Mose, ili kuwa ushuhuda kwao.”

Yesu Amponya Mtumishi Wa Jemadari

(Luka 7:1-10)

8:5 Lk 7:1; Yn 4:27Yesu alipoingia Kapernaumu, jemadari mmoja alimjia, kumwomba msaada, 8:6 Mt 4:24akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani na amepooza, tena ana maumivu makali ya kutisha.”

Yesu akamwambia, “Nitakuja na kumponya.”

8:8 Za 107:20Lakini yule jemadari akamwambia, “Bwana, mimi sistahili wewe kuingia chini ya dari yangu. Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu atapona. Kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, nikiwa na askari chini yangu. Nikimwambia huyu, ‘Nenda,’ yeye huenda; na mwingine nikimwambia, ‘Njoo,’ yeye huja. Nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ yeye hufanya.”

8:10 Mt 15:28Yesu aliposikia maneno haya, alishangaa, akawaambia wale waliomfuata, “Amin, nawaambia, hata katika Israeli sijapata kuona yeyote mwenye imani kubwa namna hii. 8:11 Za 107:3; Mal 1:11; Lk 13:29Ninawaambia kwamba wengi watatoka mashariki na magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaki na Yakobo katika Ufalme wa Mbinguni. 8:12 Mt 13:38; 25:30; Lk 13:28Lakini warithi wa Ufalme watatupwa katika giza la nje, ambako kutakuwako kilio na kusaga meno.”

8:13 Mt 9:22-29Kisha Yesu akamwambia yule jemadari, “Nenda na iwe kwako sawasawa na imani yako.” Naye yule mtumishi akapona saa ile ile.

Yesu Aponya Wengi

(Marko 1:29-34; Luka 4:38-41)

8:14 1Kor 9:5Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, akiwa ana homa. 8:15 Mk 1:29-34Akamgusa mkono wake na homa ikamwacha, naye akainuka na kuanza kumhudumia.

8:16 Mt 4:23-24Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote. 8:17 Isa 53:4; Mt 1:22Haya yalifanyika ili litimie lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba:

“Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu

na alichukua magonjwa yetu.”

Gharama Ya Kumfuata Yesu

(Luka 9:57-62)

8:18 Mk 4:35; Lk 8:22Yesu alipoona makutano mengi wamemzunguka, aliwaamuru wanafunzi wake wavuke mpaka ngʼambo ya ziwa. 8:19 Lk 9:57, 58Kisha mwalimu mmoja wa sheria akamjia Yesu na kumwambia, “Mwalimu, nitakufuata kokote uendako.”

8:20 Dan 7:13; Mk 2:10Naye Yesu akamjibu, “Mbweha wana mapango, nao ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.”

8:21 1Fal 19:20Mwanafunzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.”

8:22 Mt 4:19; Rum 6:13Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, uwaache wafu wawazike wafu wao.”

Read More of Mathayo 8