Mathayo 5:43-48, Mathayo 6:1-24 NEN

Mathayo 5:43-48

Upendo Kwa Adui

(Luka 6:27-28, 32-36)

5:43 Law 19:18; Gal 5:14; Kum 23:6; Za 139:21-22“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Mpende jirani yako na umchukie adui yako.’ 5:44 Yn 15:20; Rum 8:35Lakini ninawaambia: Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi, 5:45 Lk 6:35; Rum 8:14; Ay 25:3ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu waovu na watu wema, naye huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 5:46 Lk 6:32Kama mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo? Nanyi kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu wasiomjua Mungu, hawafanyi hivyo? 5:48 Law 19:2; 1Pet 1:16Kwa hiyo kuweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Read More of Mathayo 5

Mathayo 6:1-24

Kuwapa Wahitaji

6:1 Mt 5:16; 23:5; Rum 12:8“Angalieni msitende wema wenu mbele ya watu ili wawaone. Kwa maana mkifanya hivyo, hamna thawabu kutoka kwa Baba yenu aliye mbinguni.

“Hivyo mnapowapa wahitaji, msipige panda mbele yenu kama wafanyavyo wanafiki katika masinagogi na mitaani, ili wasifiwe na watu. Amin nawaambia wao wamekwisha kupokea thawabu yao. 6:3 Rum 12:8Lakini ninyi mtoapo sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kuume unachofanya, 6:4 Mt 6:6, 18; Kol 3:23-24ili sadaka yako iwe ni siri. Ndipo Baba yako wa mbinguni, yeye aonaye sirini atakupa thawabu kwa wazi.

Kuhusu Maombi

(Luka 11:2-4)

6:5 Mk 11:25; Lk 18:10-14“Nanyi msalipo, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Amin nawaambia, wao wamekwisha kupata thawabu yao. 6:6 1Fal 4:33Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Naye Baba yako aonaye sirini atakupa thawabu yako. 6:7 Mhu 5:2; 1Fal 18:26-29Nanyi mnaposali msiseme maneno kama wafanyavyo watu wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani kwamba watasikiwa kwa sababu ya wingi wa maneno yao. 6:8 Mt 6:32Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua kile mnachohitaji kabla hamjamwomba.

6:9 Lk 11:2-4; Yn 17:6“Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba:

“ ‘Baba yetu uliye mbinguni,

Jina lako litukuzwe.

Ufalme wako uje.

Mapenzi yako yafanyike

hapa duniani kama huko mbinguni.

6:11 Mit 30:8Utupatie riziki yetu

ya kila siku.

6:12 Mt 18:21-35Utusamehe deni zetu,

kama sisi nasi tulivyokwisha

kuwasamehe wadeni wetu.

6:13 Yak 1:13; Mt 5:37Usitutie majaribuni,

bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu

[kwa kuwa Ufalme ni wako, na nguvu,

na utukufu, hata milele. Amen].’

6:14 Efe 4:32; Kol 3:13Kwa kuwa kama mkiwasamehe watu wengine wanapowakosea, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi pia. 6:15 Mk 11:25-26; Mt 18:35Lakini msipowasamehe watu wengine makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

Kuhusu Kufunga

6:16 Isa 58:5-9; Zek 8:19“Mnapofunga, msiwe wenye huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kuwaonyesha wengine kwamba wamefunga. Amin, amin nawaambia wao wamekwisha kupata thawabu yao kamilifu. 6:17 Rut 3:3; Dan 10:3Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kunawa nyuso zenu 6:18 Mt 6:4, 6ili kufunga kwenu kusionekane na watu wengine ila Baba yenu aketiye mahali pa siri; naye Baba yenu aonaye sirini atawapa thawabu yenu kwa wazi.

Akiba Ya Mbinguni

(Luka 12:33-34)

6:19 Mt 23:4; Lk 12:16-21; Yak 5:2-3“Msijiwekee hazina duniani, mahali ambapo nondo na kutu huharibu, nao wevi huvunja na kuiba. 6:20 1Tim 6:19; Mt 19:20; Lk 12:33-34; Kol 3:1-3Lakini jiwekeeni hazina mbinguni, mahali ambapo nondo na kutu haviharibu, wala wevi hawavunji na kuiba. 6:21 Lk 12:34Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo pia moyo wako utakapokuwa.

Jicho Ni Taa Ya Mwili

(Luka 11:34-36)

6:22 Lk 11:34-36“Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni nyofu, mwili wako wote utajaa nuru. 6:23 Mt 20:15Lakini kama jicho lako ni ovu, mwili wako wote utajawa na giza. Kwa hiyo basi, kama nuru iliyomo ndani yako ni giza, hilo ni giza kuu namna gani!

Mungu Na Mali

(Luka 16:13; 12:22-31)

6:24 Lk 16:9, 13“Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Kwa kuwa atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau yule mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na Mali.6:24 Mali (au Utajiri) hapa inatoka neno Mamoni kwa Kiaramu au Mamona kwa Kiyunani.

Read More of Mathayo 6