Mathayo 5:21-42 NEN

Mathayo 5:21-42

Kuhusu Hasira

(Luka 12:57-59)

5:21 Kut 21:12; 5:17; Law 24:17“Mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiue. Yeyote atakayeua atapaswa hukumu.’ 5:22 1Yn 3:22; Yn 11:47; Mdo 6:12; Lk 16:24; Yak 3:6Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote atakayemkasirikia ndugu yake, atapaswa hukumu. Tena, yeyote atakayemwambia ndugu yake, ‘Raka,’5:22 Raka ni neno la Kiaramu ambalo maana yake ni dharau au dhihaka ya hali ya juu. atapaswa kujibu kwa Baraza la Wayahudi.5:22 Baraza la Wayahudi lilikuwa kundi kuu kabisa la utawala wa Wayahudi lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu. Lakini yeyote atakayesema ‘Wewe mpumbavu!’ atapaswa hukumu ya moto wa jehanamu.

5:23 Mt 8:4; 23:19; Mk 11:25“Kwa hiyo, kama unatoa sadaka yako madhabahuni, ukakumbuka kuwa ndugu yako ana kitu dhidi yako, 5:24 Ay 42:8; 18:19; 1Tim 2:8; 1Pet 3:7iache sadaka yako hapo mbele ya madhabahu. Enda kwanza ukapatane na ndugu yako; kisha urudi na ukatoe sadaka yako.

5:25 Mt 18:35; Lk 12:58-59“Patana na mshtaki wako upesi wakati uwapo njiani pamoja naye kwenda mahakamani, ili mshtaki wako asije akakutia mikononi mwa hakimu, naye hakimu akakutia mikononi mwa askari, nawe ukatupwa gerezani. Amin, nakuambia, hautatoka humo hadi uwe umelipa senti ya mwisho.

Kuhusu Uzinzi

5:27 Kut 20:14; Kum 5:18“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Usizini.’ 5:28 Mit 6:25; 2Pet 2:14Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 5:29 Rum 14:21; 1Kor 8:13Jicho lako la kuume likikusababisha kutenda dhambi, lingʼoe ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima ukatupwa jehanamu. 5:30 Mt 5:29Kama mkono wako wa kuume ukikusababisha kutenda dhambi, ukate, uutupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima utupwe jehanamu.

Kuhusu Talaka

(Mathayo 19:9; Marko 10:11-12; Luka 16:18)

5:31 Kum 24:1-4“Pia ilinenwa kwamba, ‘Mtu yeyote amwachaye mkewe sharti ampe hati ya talaka.’ 5:32 Lk 16:18Lakini mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati, amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na yeyote amwoaye yule mwanamke aliyeachwa, anazini.

Kuhusu Kuapa

5:33 Law 19:12; Hes 30:2; Mt 23:16-22“Tena mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiape kwa uongo, bali timiza kiapo kile ulichofanya kwa Bwana.’ 5:34 Yak 5:12; Isa 66:1; Mt 23:22Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa: iwe kwa mbingu, kwa kuwa ni kiti cha enzi cha Mungu; 5:35 Za 48:2au kwa dunia, kwa kuwa ndipo mahali pake pa kuwekea miguu; au kwa Yerusalemu, kwa kuwa ndio mji wa Mfalme Mkuu. Nanyi msiape kwa vichwa vyenu, kwa kuwa hamwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 5:37 Yak 5:12; Efe 6:16; 1Yn 3:12‘Ndiyo’ yenu iwe ‘Ndiyo,’ na ‘Hapana’ yenu iwe ‘Hapana.’ Lolote zaidi ya hili latoka kwa yule mwovu.

Kuhusu Kulipiza Kisasi

(Luka 6:29-30)

5:38 Law 24:20; Kum 19:21“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ 5:39 1Kor 6:7; 1Pet 3:9Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia. 5:40 1Kor 6:7Kama mtu akitaka kukushtaki na kuchukua joho lako, mwachie achukue na koti pia. 5:41 Mt 27:32; Mk 15:21Kama mtu akikulazimisha kwenda maili moja, nenda naye maili mbili. 5:42 Kum 15:8; Lk 16:30Mpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie kisogo yeye atakaye kukukopa.

Read More of Mathayo 5