Mathayo 4:1-22 NEN

Mathayo 4:1-22

Kujaribiwa Kwa Yesu

(Marko 1:12-13; Luka 4:1-13)

4:1 Kut 34:28; 1Fal 19:8Kisha Yesu akaongozwa na Roho Mtakatifu kwenda nyikani ili akajaribiwe na ibilisi. 4:2 Kut 34:28; 1Fal 19:8Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa. 4:3 1The 3:5; Mk 3:11; Ufu 2:18Mjaribu akamjia na kumwambia, “Ikiwa wewe ndiye Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”

4:4 Kum 8:3; Yn 4:34Lakini Yesu akajibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ ”

4:5 Neh 11:1; Mt 27:5Ndipo ibilisi akamchukua Yesu mpaka mji mtakatifu na kumweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu, 4:6 Za 91:11-12; Mt 4:3akamwambia, “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini. Kwa kuwa imeandikwa:

“ ‘Atakuagizia malaika zake,

nao watakuchukua mikononi mwao

ili usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ ”

4:7 Kum 6:16Yesu akamjibu, “Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”

Kwa mara nyingine, ibilisi akamchukua Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonyesha falme zote za dunia na fahari zake, kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukinisujudia na kuniabudu.”

4:10 Ay 1:6-9; Rum 16:20; 6:13Yesu akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’ ”

4:11 Lk 22:43; Ebr 1:14Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumhudumia.

Yesu Aanza Kuhubiri

(Marko 1:14-15; Luka 4:14-15)

4:12 Mt 14:3; Mk 1:14Yesu aliposikia kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ametiwa gerezani, alirudi Galilaya. 4:13 Mk 9:33; Yn 2:12Akaondoka Nazareti akaenda kuishi Kapernaumu, mji ulioko karibu na bahari, katika mipaka ya nchi ya Zabuloni na Naftali, 4:14 Isa 9:1, 2; 9:1; Mt 1:22ili kutimiza unabii wa nabii Isaya, kama alivyosema:

4:15 Isa 9:1, 2“Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,

kwenye njia ya kuelekea baharini,

ngʼambo ya Yordani,

Galilaya ya watu wa Mataifa:

4:16 Isa 9:1-2; Yn 1:4-9watu wale waliokaa gizani

wameona nuru kuu;

nao wale walioishi katika nchi ya uvuli wa mauti,

nuru imewazukia.”

4:17 Mt 3:2; Mk 1:14, 15Tangu wakati huo, Yesu alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.”

Yesu Awaita Wanafunzi Wake Wa Kwanza

(Marko 1:16-20; Luka 5:1-11)

4:18 Mk 7:31; Yn 6:1; Mt 16:17-18Yesu alipokuwa anatembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa wao walikuwa wavuvi. 4:19 Lk 5:28; Yn 1:43Yesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” 4:20 Mk 10:28; Lk 18:28; Mt 19:27Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.

4:21 Mk 3:17; Lk 8:51Alipoendelea mbele kutoka pale, akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakizitengeneza nyavu zao. Yesu akawaita. 4:22 Mt 4:19Nao mara wakaiacha mashua yao, pamoja na baba yao, wakamfuata.

Read More of Mathayo 4