Mathayo 27:11-44 NEN

Mathayo 27:11-44

Yesu Mbele Ya Pilato

(Marko 15:2-15; Luka 23:3-25; Yohana 18:33–19:16)

27:11 Mt 2:2Wakati huo Yesu akiwa amesimama mbele ya mtawala, mtawala akamuuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”

Yesu akasema, “Wewe wasema hivyo.”

27:12 Mk 14:61; Yn 19:9Lakini viongozi wa makuhani na wazee walipomshtaki, hakujibu neno. 27:13 Mt 26:62Ndipo Pilato akamuuliza, “Je, husikii ni mambo mangapi wanayokushtaki nayo?” 27:14 Mk 14:61Lakini Yesu hakumjibu hata kwa shtaka moja, kiasi kwamba mtawala alishangaa sana.

27:15 Yn 18:39Basi ilikuwa ni desturi ya mtawala kumfungua mfungwa mmoja aliyechaguliwa na umati wa watu wakati wa sikukuu. Wakati huo alikuwepo mfungwa mmoja mwenye sifa mbaya, aliyeitwa Baraba. 27:17 Mt 1:16Hivyo umati wa watu walipokusanyika, Pilato akawauliza, “Mnataka niwafungulie nani, Baraba au Yesu yeye aitwaye Kristo?” 27:18 Yn 11:47, 48; 12:19Kwa kuwa alitambua Yesu alikuwa amekabidhiwa kwake kwa ajili ya wivu.

27:19 Yn 19:13; Mt 27:24; Hes 12:6Pilato akiwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mkewe akampelekea ujumbe huu: “Usiwe na jambo lolote juu ya mtu huyu asiye na hatia, kwa kuwa leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake.”

27:20 Mdo 3:14Lakini viongozi wa makuhani na wazee wakaushawishi ule umati wa watu kwamba waombe Baraba afunguliwe, naye Yesu auawe.

Mtawala akawauliza tena, “Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka niwafungulie?”

Wakajibu, “Baraba.”

27:22 Mt 1:16Pilato akawaambia, “Basi nifanye nini na huyu Yesu aitwaye Kristo?”

Wakajibu wote, “Msulubishe!”

Pilato akauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?”

Lakini wao wakazidi kupiga kelele, wakisema, “Msulubishe!”

27:24 Mt 26:5; Za 26:6; Kum 21:6-8Pilato alipoona kwamba hawezi kufanya lolote, lakini badala yake ghasia zilikuwa zinaanza, akachukua maji, akanawa mikono yake mbele ya ule umati wa watu, akasema, “Sina hatia juu ya damu ya mtu huyu, hili ni jukumu lenu!”

27:25 Yos 2:19; Mdo 5:28Watu wote wakajibu, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!”

27:26 Isa 53:5; Yn 19:1Basi akawafungulia Baraba. Lakini baada ya kuamuru Yesu achapwe mijeledi, akamtoa ili asulubishwe.

Askari Wamdhihaki Yesu

(Marko 15:16-20; Yohana 19:2-3)

27:27 Yn 18:28-33; 19:9Kisha askari wa mtawala wakampeleka Yesu kwenye Praitorio27:27 Praitorio maana yake ni makao makuu ya mtawala, jumba la kifalme lililokuwa linakaliwa na Pontio Pilato huko Yerusalemu, palipokuwa na kiti cha hukumu. na wakakusanya kikosi kizima cha askari kumzunguka. 27:28 Yn 19:2Wakamvua nguo zake na kumvika vazi la rangi nyekundu, kisha 27:29 Isa 53:3; Yn 19:2-3wakasokota taji ya miiba, wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, na wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki, wakisema, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!” 27:30 Mt 16:21; 26:27; 27:31; Isa 53:7Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga kichwani tena na tena. 27:31 Mk 15:20-41; Lk 23:26Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka ili wakamsulubishe.

Yesu Asulubishwa

(Marko 15:21-32; Luka 23:26-43; Yohana 19:17-27)

27:32 Ebr 13:12; Mdo 11:20; Mk 15:21; Lk 23:26Walipokuwa wakienda, wakakutana na mtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba. 27:33 Yn 19:17Wakafika mahali palipoitwa Golgotha (maana yake ni Mahali pa Fuvu la Kichwa). 27:34 Mt 27:18; Za 69:21Hapo wakampa Yesu divai iliyochanganywa na nyongo ili anywe; lakini alipoionja, akakataa kuinywa. 27:35 Za 22:18Walipokwisha kumsulubisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura. [Hili lilifanyika ili litimie lile neno lililonenwa na nabii, “Waligawa nguo zangu miongoni mwao na vazi langu wakalipigia kura.”] 27:36 Mt 27:54Kisha wakaketi, wakamchunga. 27:37 Mk 15:26; Lk 23:38; Yn 19:19Juu ya kichwa chake, kwenye msalaba, wakaandika shtaka lake hivi: Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi. 27:38 Isa 53:12Wanyangʼanyi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wa kushoto. 27:39 Za 109:25; Mao 2:15Watu waliokuwa wakipita njiani wakamtukana huku wakitikisa vichwa vyao 27:40 Mt 26:61; Yn 2:19; Mt 4:3-6na kusema, “Wewe ambaye utalivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe mwenyewe basi! Kama wewe ni Mwana wa Mungu, shuka kutoka msalabani.”

Vivyo hivyo, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamdhihaki wakisema, 27:42 Yn 1:49; 12:13; 3:15“Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe! Yeye ni Mfalme wa Israeli! Ashuke sasa kutoka msalabani, nasi tutamwamini. 27:43 Za 22:8Anamwamini Mungu, basi Mungu na amwokoe sasa kama anamtaka, kwa maana alisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu.’ ” 27:44 Mk 15:32; Lk 23:39Hata wale wanyangʼanyi waliosulubiwa pamoja naye wakamtukana vivyo hivyo.

Read More of Mathayo 27