Mathayo 26:69-75, Mathayo 27:1-10 NEN

Mathayo 26:69-75

Petro Amkana Bwana Yesu

(Marko 14:66-72; Luka 22:56-62; Yohana 18:15-18, 25-27)

26:69 Mk 14:66; Lk 22:55; Yn 18:16, 17, 25Wakati huu Petro alikuwa amekaa nje uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia na kumwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.”

Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui hilo usemalo.”

Alipotoka nje kufika kwenye lango, mtumishi mwingine wa kike alimwona, akawaambia watu waliokuwepo, “Huyu mtu alikuwa pamoja na Yesu, Mnazareti.”

Akakana tena kwa kiapo akisema, “Mimi simjui huyo!”

26:73 Lk 22:59Baada ya muda mfupi, wale waliokuwa wamesimama pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana usemi wako ni kama wao.”

26:74 Mk 14:71Ndipo Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, “Mimi simjui mtu huyo!”

Papo hapo jogoo akawika. 26:75 Mt 26:24; Yn 13:38Ndipo Petro akakumbuka lile neno Yesu alilokuwa amesema: “Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi.

Read More of Mathayo 26

Mathayo 27:1-10

Yesu Aletwa Mbele Ya Pilato

(Marko 15:1; Luka 23:1-2; Yohana 18:28-32)

27:1 Mk 15:1; Lk 22:66Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri pamoja dhidi ya Yesu ili kumuua. 27:2 Mt 20:19; Mdo 3:13; 1Tim 6:13Wakamfunga, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato, ambaye alikuwa mtawala wa Kirumi.

Yuda Ajinyonga

(Matendo 1:18-19)

27:3 Mt 10:4; 26:14-15Yuda, ambaye alikuwa amemsaliti Yesu, alipoona kuwa Yesu amehukumiwa, akajuta na akarudisha vile vipande thelathini vya fedha alivyopewa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu. 27:4 Mt 27:24Akasema, “Nimetenda dhambi, kwa maana nimeisaliti damu isiyo na hatia.”

Wakamjibu, “Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako.”

27:5 Lk 1:9, 21; Mdo 1:18-19Basi Yuda akavitupa vile vipande vya fedha ndani ya Hekalu akaondoka akaenda kujinyonga.

27:6 Mk 12:41Wale viongozi wa makuhani wakazichukua zile fedha wakasema, “Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu.” Kwa hiyo baada ya kushauriana, waliamua kuzitumia kununulia shamba la mfinyanzi, liwe mahali pa kuzikia wageni. 27:8 Mdo 1:19Hii ndiyo sababu lile shamba likaitwa Shamba la Damu hadi leo. 27:9 Mt 1:22Ndipo likatimia lile lililonenwa na nabii Yeremia, kwamba, “Walichukua vile vipande thelathini vya fedha, thamani aliyopangiwa na watu wa Israeli, 27:10 Zek 11:12-13; Yer 32:6-9wakanunulia shamba la mfinyanzi, kama vile Bwana alivyoniagiza.”

Read More of Mathayo 27