Mathayo 26:31-46 NEN

Mathayo 26:31-46

Yesu Atabiri Petro Kumkana

(Marko 14:27-31; Luka 22:31-34; Yohana 13:36-38)

26:31 Mt 11:6; 13:21; Zek 13:7; Yn 16:32Kisha Yesu akawaambia, “Usiku huu, ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa:

“ ‘Nitampiga mchungaji,

nao kondoo wa hilo kundi watatawanyika.’

26:32 Mt 28:7, 10, 16Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”

Petro akajibu, “Hata kama wote watakuacha, kamwe mimi sitakuacha.”

26:34 Yn 13:38Yesu akamjibu, “Amin, nakuambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”

26:35 Yn 13:37Lakini Petro akasisitiza, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wanafunzi wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.

Yesu Anaomba Gethsemane

(Marko 14:32-42; Luka 22:39-46)

26:36 Mk 14:32, 35; Lk 22:39; Yn 18:1Kisha Yesu akaenda pamoja na wanafunzi wake mpaka kwenye bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia, “Kaeni hapa, nami niende kule nikaombe.” 26:37 Mt 4:21Akamchukua Petro pamoja na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kufadhaika. 26:38 Yn 12:27Kisha Yesu akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe pamoja nami.”

26:39 Mt 20:22; Za 40:6-8; Yn 4:34Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniondokee. Lakini si kama nipendavyo mimi, bali kama upendavyo wewe.”

26:40 Mt 26:38Kisha akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamuuliza Petro, “Je, ninyi hamkuweza kukesha pamoja nami hata kwa saa moja? 26:41 Mt 6:13Kesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu.”

26:42 Mt 26:39Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, basi mapenzi yako yafanyike.”

Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 26:44 2Kor 12:8Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale.

26:45 Mt 26:18Kisha akarudi kwa wanafunzi wake, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Tazameni, saa imefika ambapo Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi. 26:46 Yn 14:31Inukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!”

Read More of Mathayo 26