Mathayo 26:1-30 NEN

Mathayo 26:1-30

Shauri Baya La Kumuua Yesu

(Marko 14:1-2; Luka 22:1-2; Yohana 11:45-53)

26:1 Mt 7:28Yesu alipomaliza kusema hayo yote, akawaambia wanafunzi wake, 26:2 Yn 11:55; 13:1“Kama mnavyojua, baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, naye Mwana wa Adamu atasalitiwa ili asulubiwe.”

26:3 Za 2:2; Lk 3:2; Mdo 4:6Basi viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakakusanyika katika jumba la utawala la kuhani mkuu, jina lake Kayafa. 26:4 Mt 12:14Wakafanya shauri ili kumkamata Yesu kwa siri na kumuua. 26:5 Mt 27:24Lakini wakasema, “Isiwe wakati wa Sikukuu, kusitokee ghasia miongoni mwa watu.”

Yesu Anapakwa Mafuta Huko Bethania

(Marko 14:3-9; Yohana 12:1-8)

26:6 Mt 21:17Yesu alikuwa Bethania nyumbani mwa Simoni aliyekuwa na ukoma, naye mwanamke mmoja akamjia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya thamani kubwa; akayamimina kichwani mwa Yesu alipokuwa ameketi mezani kula chakula.

26:8 Yn 12:4Lakini wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Upotevu huu wote ni wa nini? Manukato haya yangeuzwa kwa bei kubwa, na fedha hizo wakapewa maskini.”

26:10 Lk 11:7Yesu, akijua jambo hili, akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Yeye amenitendea jambo zuri sana. 26:11 Kum 15:11Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote. 26:12 Yn 19:40Alipomiminia haya manukato kwenye mwili wangu, amefanya hivyo ili kuniandaa kwa ajili ya maziko yangu. Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo hii Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.”

Yuda Akubali Kumsaliti Yesu

(Marko 14:10-11; Luka 22:3-6)

26:14 Mt 26:25, 47; 10:4Kisha mmojawapo wa wale kumi na wawili, aitwaye Yuda Iskariote, alikwenda kwa viongozi wa makuhani 26:15 Kut 21:32; Zek 11:12na kuuliza, “Mtanipa nini nikimtia Yesu mikononi mwenu?” Wakamlipa vipande thelathini vya fedha. 26:16 1Tim 6:9, 10Tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Yesu.

Yesu Ala Pasaka Pamoja Na Wanafunzi

(Marko 14:12-21; Luka 22:7-23; Yohana 13:21-30)

26:17 Kut 12:18-20Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wanafunzi walimjia Yesu wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?”

26:18 Mk 14:35, 41; Yn 17:1Akajibu, “Nendeni kwa mtu fulani huko mjini, mkamwambie, ‘Mwalimu asema hivi: Saa yangu imekaribia. Nitaiadhimisha Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.’ ” Hivyo wanafunzi wakafanya kama vile Yesu alivyokuwa amewaelekeza, nao wakaandaa Pasaka.

26:20 Mk 14:17-21; Lk 22:14Ilipofika jioni, Yesu alikuwa ameketi mezani pamoja na wale wanafunzi wake kumi na wawili. 26:21 Lk 22:21-23; Yn 13:21Nao walipokuwa wakila, Yesu akasema, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.”

Wakahuzunika sana, wakaanza kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi Bwana?”

26:23 Za 41:9; Yn 13:18Yesu akawaambia, “Yule aliyechovya mkono wake katika bakuli pamoja nami ndiye atakayenisaliti. 26:24 Dan 9:24; 1Pet 1:10-11Mwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu. Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa!”

26:25 Mt 23:7Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, akasema, “Je, ni mimi Rabi?”

Yesu akajibu, “Naam, wewe mwenyewe umesema.”

Kuanzishwa Kwa Meza Ya Bwana

(Marko 14:22-26; Luka 22:14-20; 1 Wakorintho 11:23-25)

26:26 Mt 14:9; 1Kor 10:16Walipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega, na kuwapa wanafunzi wake, akisema, “Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu.”

26:27 Mk 14:23Kisha akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, “Nyweni nyote katika kikombe hiki. 26:28 Mal 2:5; Ebr 10:29; Mt 20:28; Mk 1:4Hii ndiyo damu yangu ya Agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. 26:29 Mdo 10:41Lakini ninawaambia, tangu sasa sitakunywa tena katika uzao huu wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu.”

26:30 Mt 21:1; Mk 14:26Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni.

Read More of Mathayo 26