Mathayo 24:32-51, Mathayo 25:1-13 NEN

Mathayo 24:32-51

24:32 Lk 21:29“Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 24:33 Yak 5:9Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yote, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni. 24:34 Mt 16:28; 23:36Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. 24:35 Mt 5:18Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Hakuna Ajuaye Siku Wala Saa

(Marko 13:32-37; Luka 17:26-30, 34-36)

24:36 Mdo 1:7“Kwa habari ya siku ile na saa, hakuna ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake. 24:37 Mwa 6:5; 7:6-23Kama ilivyokuwa wakati wa Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 24:38 Mt 22:30Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Noa alipoingia katika safina. 24:39 Lk 15Nao hawakujua lolote mpaka gharika ilipokuja ikawakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa atakapokuja Mwana wa Adamu. 24:40 Lk 17:34-35Watu wawili watakuwa shambani, naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa. 24:41 Lk 17:30Wanawake wawili watakuwa wanasaga pamoja, naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa.

24:42 Mt 25:13; Lk 12:40“Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni siku gani atakapokuja Bwana wenu. 24:43 Lk 12:39Lakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua ni wakati gani wa usiku ambao mwizi atakuja, angekesha na hangekubali nyumba yake kuvunjwa. 24:44 1The 5:6Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia.

Mfano Wa Mtumishi Mwaminifu

(Luka 12:41-48)

24:45 Mt 25:21-23“Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa? 24:46 Ufu 16:15Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 24:47 Mt 25:21, 23; Lk 22:29Amin, nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote. 24:48 Mhu 8:11Lakini kama huyo mtumishi ni mwovu, naye akasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu atakawia muda mrefu,’ 24:49 Lk 21:34kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, na kula na kunywa pamoja na walevi. Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua. 24:51 Mt 8:12Atamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wanafiki, mahali ambako kutakuwa ni kulia na kusaga meno.

Read More of Mathayo 24

Mathayo 25:1-13

Mfano Wa Wanawali Kumi

25:1 Mt 13:24; Mdo 20:8; Ufu 4:5; 19:7; 21:2“Wakati huo, Ufalme wa Mbinguni utakuwa kama wanawali kumi waliochukua taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi. 25:2 Mt 24:45Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba, lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo. 25:5 1The 5:6Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.

25:6 Mt 24:31; 1The 3“Usiku wa manane pakawa na kelele: ‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!’

25:7 Lk 12:35“Ndipo wale wanawali wote wakaamka na kuzitengeneza taa zao. 25:8 Lk 12:35Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta yenu kidogo; taa zetu zinazimika.’

“Lakini wale wenye busara wakawajibu, ‘Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu.’

25:10 Ufu 19:9“Nao walipokuwa wakienda kununua mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa.

25:11 Lk 13:25, 27; Mt 7:21; 2:23“Baadaye wale wanawali wengine nao wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’

25:12 Mt 7:23; Za 5:5; Hab 1:12; Yn 9:31“Lakini yeye bwana arusi akawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’

25:13 Mk 13:35; Lk 12:40“Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa.

Read More of Mathayo 25