Mathayo 24:1-31 NEN

Mathayo 24:1-31

Kubomolewa Kwa Hekalu Kwatabiriwa

(Marko 13:1-2; Luka 21:5-6)

24:1 Mk 13:1; Lk 21:5Yesu akatoka Hekaluni na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya Hekalu. 24:2 Lk 19:44; 1Fal 9:7; Yer 26:18; Mik 3:12Ndipo Yesu akawauliza, “Je, mnayaona haya yote? Amin, nawaambia, hakuna hata jiwe moja hapa litakalobaki juu ya jingine, bali kila moja litabomolewa.”

Ishara Za Nyakati Za Mwisho

(Marko 13:3-23; Luka 21:7-24)

24:3 Mt 21:1Yesu alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia faraghani, wakamuuliza, “Tuambie, mambo haya yatatukia lini, nayo dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia ni gani?”

24:4 Efe 5:6; Kol 2:8, 18; 2The 2:3; 1Yn 4:1Yesu akawajibu, “Jihadharini, mtu yeyote asiwadanganye. 24:5 Mt 24:11, 23-24; 1Yn 2:18Kwa maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye Kristo,’24:5 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. nao watawadanganya wengi. 24:6 Dan 2:26Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado. 24:7 Isa 19:2; Mdo 11:28Taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa utungu.

24:9 Mt 10:17; Yn 16:2“Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu. 24:10 Dan 11:41Wakati huo, wengi wataacha imani yao, nao watasalitiana kila mmoja na mwenzake na kuchukiana. 24:11 Mt 7; 15Watatokea manabii wengi wa uongo, nao watawadanganya watu wengi. Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa, 24:13 Mt 10:22lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa. 24:14 Mt 4:23; Rum 10:18; Ufu 3:10Injili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja.

24:15 Mdo 6:13; Dan 11:31; 12:11“Hivyo mtakapoona lile ‘chukizo la uharibifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu (asomaye na afahamu), basi wale walioko Uyahudi wakimbilie milimani. 24:17 1Sam 9:25; Lk 12:3Yeyote aliye juu ya dari ya nyumba asishuke ili kuchukua chochote kutoka ndani ya nyumba. Aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake. 24:19 Lk 23:29Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! 24:20 Mdo 1:12Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi au siku ya Sabato. 24:21 Eze 5:9; Dan 12:1Kwa maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa: wala haitakuwako tena kamwe. 24:22 Isa 65:8, 9Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeokoka. Lakini kwa ajili ya wateule, siku hizo zitafupizwa. 24:23 Lk 17:23; 21:8Wakati huo kama mtu yeyote akiwaambia, ‘Tazama, Kristo huyu hapa!’ Au, ‘Kristo yuko kule,’ msisadiki. 24:24 Kut 7:11, 22; Ufu 16:14Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara kubwa na maajabu mengi ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule hasa. Angalieni, nimekwisha kuwaambia mapema.

“Kwa hiyo mtu yeyote akiwaambia, ‘Yule kule nyikani,’ msiende huko. Au akisema, ‘Yuko kwenye chumba,’ msisadiki. 24:27 Lk 17:24; Mt 8:20Kwa maana kama vile umeme utokeavyo mashariki na kuonekana hata magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 24:28 Lk 17:37Kwa maana popote ulipo mzoga, huko ndiko wakusanyikapo tai.

Kuja Kwa Mwana Wa Adamu

(Marko 13:24-31; Luka 21:25-33)

24:29 Sef 1:15; Ufu 8:12“Mara baada ya dhiki ya siku zile,

“ ‘jua litatiwa giza,

nao mwezi hautatoa nuru yake;

nazo nyota zitaanguka kutoka angani,

na nguvu za anga zitatikisika.’

24:30 Dan 7:13; Ufu 1:7“Ndipo itakapotokea ishara ya Mwana wa Adamu angani, na makabila yote ya dunia yataomboleza. Nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu. 24:31 Mt 13:41; Zek 9:14; 1The 4:16Naye atawatuma malaika zake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine.

Read More of Mathayo 24